Haijalishi Mtu wa Dini au Mpagani, Mtu asiye mwaminifu Hana mwisho mzuri ktk kila jambo

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,722
Kuna baadhi ya vitu vinapita katikati ya Dini na upagani na vinamilikiwa pande zote.

Mwizi au fisadi hata awe na mamillioni mangapi maisha yake yanautofauti mkubwa na mtu mwaminifu anaejitambua hata kama anaishi chini ya dola moja.

Watu waongowaongo mara nyingi wanaishi maisha ya kutangatanga na hata akifanikiwa hafurahii maisha katika ukamilifu wake.

Matapeli mara nyingi hata kama akitapeli Trillion wanaishia kuishi maisha ya kungaunga na wasiwasi.

Watu wasio waaminifu kwenye mahusiano wengi wanaishi maisha yaliyo chini ya kiwango. Anakuwa na Furaha za Muda mfupi na maisha yanazungukwa na matatizo mengi yakujiongezea.

Watu wasio waaminifu kwenye Ajira zao, Shuguli zao za kila siku hara kama wakifanikiwa kupitia kutegea,Kudokoa uwezo wa kutunza hayo mafanikio na kuyafurahia mara nyingi ni wa chini. Furaha aliyonayo iko hatarini kukata muda wowote akibainika,

Uaminifu Uaminifu Uaminifu
 
Uaminifu na tabia njema ni dawa.baraka na nuru ya mafanikio,wengine tuna lower class tu lakini nafasi tuliyopewa kazini we acha tu.Poleni mliokosa uaminifu maana mtakosa mengi mazuri na mwisho wenu lazima uwe mbaya tu
kweli mkuu mafanikio ya kudumu na furaha ya uhakika haiwezi vkutenganishwa na uaminifu wa wako
 
wote bado waongo ikiwemo na mimi kwa kutumia I D fake kama mnataka kuwa wakweli tutumie verified account
 
Uaminifu na tabia njema ni dawa.baraka na nuru ya mafanikio,wengine tuna lower class tu lakini nafasi tuliyopewa kazini we acha tu.Poleni mliokosa uaminifu maana mtakosa mengi mazuri na mwisho wenu lazima uwe mbaya tu
mharage ya ukweni
 
kwa mawazo ya jamii ya kitanzania siwezi kuwa mwaminifu hata kidogo, usipo iba kazini uka staafu ukiwa na maisha ya kawaida unachekwa na kudharaulika.

matokeo yake ni kilio cha nafsi kwa dharau za jamii, wala sio furaha kama usemavyo.

ntakuwa mwaminifu kwenye biashara ama mahusiano na watu (sio mapenzi) ila kwa serikali ni wizi tu
 
Kuna baadhi ya vitu vinapita katikati ya Dini na upagani na vinamilikiwa pande zote.

Mwizi au fisadi hata awe na mamillioni mangapi maisha yake yanautofauti mkubwa na mtu mwaminifu anaejitambua hata kama anaishi chini ya dola moja.

Watu waongowaongo mara nyingi wanaishi maisha ya kutangatanga na hata akifanikiwa hafurahii maisha katika ukamilifu wake.

Matapeli mara nyingi hata kama akitapeli Trillion wanaishia kuishi maisha ya kungaunga na wasiwasi.

Watu wasio waaminifu kwenye mahusiano wengi wanaishi maisha yaliyo chini ya kiwango. Anakuwa na Furaha za Muda mfupi na maisha yanazungukwa na matatizo mengi yakujiongezea.

Watu wasio waaminifu kwenye Ajira zao, Shuguli zao za kila siku hara kama wakifanikiwa kupitia kutegea,Kudokoa uwezo wa kutunza hayo mafanikio na kuyafurahia mara nyingi ni wa chini. Furaha aliyonayo iko hatarini kukata muda wowote akibainika,

Uaminifu Uaminifu Uaminifu
Umeeleza jambo la ukweli sana mdau ambalo nimeliona sana hapa tanzania hasa kwa vijana kwenye sekta ya utalii.Vijana kwa unjanjaujanja wa kijinga na tamaa za 'kupiga' hela ataongozana na mtalii kutoka ulaya na kumdanganya bei za huduma mbalimbali ili kijana apate cha juu.Mtalii anamwamini analipa alivyoelekezwa. Kweli kijana baada ya mtalii kuondoka anajikuta ana dola 2000 mfukoni kiasi ambacho angekipata kwa kazi ya miezi miwili au tatu.
Mtalii naye katika kuulizauliza na 'kushare experience' na wenzake anagundua kwamba aliliwa vibaya sana.Anachukia, anaandikia wenzake kukwepa huo mji na huyo kijana.
Kijana anashangaa kuona watalii wanamkwepa hawataki kufanya kazi naye.Kijana anaanza kumfikiria vibaya mwenzake waliogombana juzi kwamba kamfanyia kitu mbaya.
Waweza endeleza hii stori mwenyewe. Uaminifu ni muhimu mno mno katika shughuli zetu.
 
Naunga mikono na akili Hoja.

Umenikumbusha jamaa alihama nyumba kwa USD 1000 akakimbilia kusikojulikana na familia.
Kuna bosi mmoja amewahi kufukuzwa kazi na kuacha mshahara wa mamillioni kwa kosa la kutokuwa mwaminifu na ghalama ya kosa lililopelekea kufukuzwa ni chini ya millioni.
 
kwa mawazo ya jamii ya kitanzania siwezi kuwa mwaminifu hata kidogo, usipo iba kazini uka staafu ukiwa na maisha ya kawaida unachekwa na kudharaulika.

matokeo yake ni kilio cha nafsi kwa dharau za jamii, wala sio furaha kama usemavyo.

ntakuwa mwaminifu kwenye biashara ama mahusiano na watu (sio mapenzi) ila kwa serikali ni wizi tu
Kuna jukumu utakuwa unalikwepa mkuu kwa kuamua kujichimbia kwenye wizi wa kodi za wananchi masikini kama mbadala.
 
Back
Top Bottom