Hadithi; The girls in island -10

chiqutitta

JF-Expert Member
Nov 13, 2015
1,160
3,124
SEHEMU YA KUMI
THE GIRLS IN ISLAND 10

“nshukuru kama una uwezo wa kukumbuka kwa kiwango hicho. Hivi unafikiri mimi nipo kwenye hali gani toka uliponionjesha asali yako?... unafikiri moyo wangu unaumia kiasi gani kwa kuwaona wewe na malikia mkiwa mnaongozana na kulala chumba kimoja?..umeshawahi kufikiria kuwa naumia kiasi gani?.. naomba unipende ili niweze kuishi na wewe milele daima. Nilikupenda toka siku ya kwanza na mpaka kesho nitaendelea kukupenda. Naomba usikatae kwakua uliyekuwa naye kwa sasa anakutumia tu na kama atapatikana mwengine wa kuushida mtihani huu, basi utakuwa huna thamani. Nakupenda sana na naomba ukubali ili nikuonyeshe njia za kujinasua katika mikono ya malikia Trizza.” Aliongea yule dada maneno yaliyoniacha mdomo wazi. Sikua najua kuwa hata hawa viumbe nao walikua na mioyo ya kupenda. Nilibaki nimeduwaa tu kutokana na mitihani mizito niliyoipata kwa siku hiyo.

“kwani mlishawahi kuishi na wanaume hapo zamani?.. mbona mnaonekana mpo jinsia moja tu na vipi mnaweza kupendana na kuzaliana?” nilijikuta nimemuuliza swali hilo baada ya kona wananichanganya. Maana mwanzoni nilikisoma kisiwa hicho kwenye kitabu cha The girls in island cha mwanasayansi pekee aliyefanikiwa kurudi kutoka kwenye kisiwa hicho mr. Mac Donald, alielezea kuwa kisiwa hicho kilikuwa kina watu jinsia moja tu. Na kilikua kinamilikiwa na majini ambao nao walikuwa wanawake. Swali hilo lilikua swali muhimu sana ambalo nilikosa nafasi ya kumuuliza mtu yoyote kwenye kisiwa hicho.

“huwezi kujua mambo yote yaliyomo kwenye kisiwa hiki kama hautakaa kwa muda mrefu. Ila cha kukuambia ni kwamba tu. Wanaume tunaowategemea ni wanaume wageni kutoka sehemu mbali mbali za duniani. Ila kwakua wanaume wengi wanashidwa mitihani, ndio maana wanashidwa kurudi huko. Ila kuhusu kuzaa, huwa wanakuja majini wa kuime na kutuingilia mara moja kwa mwezi. Ikitokea umeshka mimba basi huyo ndio anakuwa mume wako na hukutembelea wakati wote wa kulala. Kwa hiyo wapo wanaume majini wanaishi huku lakini wewe binaadamu wa kawaida huwezi kuwaona.” Aliongea yule msichna na kufumbua macho.

“ningependa kufahamu jina lako… maana nahisi unanifaa sana.” Niliongea hivyo baada ya kuona kuna haja ya kuwa karibu na dada huyo ili niweze kutimiza malengo yangu.

“naitwa Shenaiza.. mbona umechelewa kuniuliza?” alijibu na kuniuliza swali lililonifanya nitabasamu.

“nilikosa nafasi.. nadhani hata wewe unahitaji kujua jina langu kwa sasa.” Niliongea na kujaribu kumzoea Shenaiza.

“hapana,.. ningekua silijui jina lako ningekuuliza hata kabla sijaongea chochote na wewe.” Alijibu Shenaiza na kunifanya nishangae kidogo. Ila nilijipa imani kuwa jina langu alilijua kupitia malikia Trizza.

“nimekuelewa Shenaiza.. naomba nipe siku mbili ili nilitafakari hili.. maana kuanzisha uhusiano na nyinyi ni hatari sana kwakua mna uhusiano mkubwa na majini.” Niliongea na kunyanyuka .

“bora uwe na mimi kwakua nitakufanya uweze kuwaona hao majini na nitakulinda pia.. kuliko hivi sasa kwakua hujua wana mikakati gani na wewe.” Alijibu Shenaiza na yeye akanyanyuka.

“nakutakia usiku mwema.” Aliongea na punde tu akapotea katika macho yangu. Nilifumbua macho na kujikuta nipo kitandani. Sikujua nilifikaje pale, ila kutokana na mazingira ya asubuhi, ndio niligundua kua nilikua naota.

Nilienda bafuni kuoga na baada ya hapo nikarudi kuungana na malikia kwenye meza ya chakula cha usubuhi.

Japokua niliamini kua ile ilikua ndoto, lakini sikuipuuzia. Nilizidi kuihifadhi kichwani na kujipa kazi ya kuitafakari kwa kina. Nilimuangalia malikia na kuanza kumchunguza na kujaribu kusoma mawazo yak e juu yangu baada ya wiki moja kama sitampa jibu sahihi. Nilitafakari kutoroka, ila hakukua na njia yoyote itakayoniwezesha mimi kupata boti ya kunirudisha nyumbani kwetu.

Nilishusha pumzi na kumuachia Mungu kwa chochote kitakachonitokea. Baada ya kunywa chai, nilitoka na kwenda kwenye bustani na kukaa. Nilipunga upepo pale kwa muda kidogo. Ghafla nikahisi kuna mtu amekuja kukaa pembeni yangu. Niligeuza shingo na kumkuta yule dada niliyemuota kuwa anaitwa Shenaiza ndiye aliyekaa pale.

“kipi kilichokushangaza mfalme.” Aliongea yule dada baada ya kuinama na kunpa heshima yangu.

“unaweza kunitajia jina lako?” niliuliza baada ya kuona kama alikua anajua kitu nilichokiota usiku.

“nilishakutajia mfalme,…. Huwezi kuwa umesahau muda huu.” Alinijibu na kunifanya nipatwe na mshangao.

“Shenaiza!?” niliuliza kwa mshangao huku nikilisubiria jibu lake kwa hamu.

“nashukuru kwa kulikumbuka jina langu.” Alinijibu na kuniweka njia panda kwa mara nyingine.

“haya maajabu sasa…. Unaweza kuniambia kuwa usiku wa kuamkia leo nilikua nakuota au tulikua wote?” niliuliza na kumtolea macho yule dada.

“ulikua unafanya yote kwa pamoja.” Alinijibu yule dada na kunifanya nisimuelewe alikua anamaanisha nini.

“nifafanulie tafadhali.”niliongea huku macho yangu yakiwa hayabandukki kwa mrembo huyo aliyejaa maajabu.

“nilishakuambia kua huwezi kujua mambo yote kwa siku moja. Isitoshe kwa sasa umefumbwa mambo mengi ambayo huwezi kuyaona bila ya kwa na mimi… cha umuhimu ukumbuke ahadi yako tu uliyoniahidi usiku uliopita… tumebakiwa na siku moja tu kabla ya kuanza mahusiano yetu.” Aliongea yule na dada na hakunipa nafasi ya kujibu chochote. Nilliona tu ghafla kapotea kwenye upeo wa macho yangu. Nilitamani nitumbukie ndani kwa jinsi wasichana hao walivyokua wababe hadi katika maamuzi ya mtu binafsi.

Sikuona haja ya kuendelea kukaa nje zaidi ya kurudi ndani ambapo nilienda kulala. Sikuweza kupata usingizi zaidi ya kuyatafakari majibu ya Shenaiza na malikia kwa kua wote nilikua siwahitaji zaidi ya kuhitaji kuondoka tu kwenye kisiwa hicho.

Jioni ya siku hiyo nilipanga ziara ya kuwatembelea marafiki zangu katika vyumba vyao walivyopewa.

Hakuna niliyeweza kuonana nae kwa jinsi walivyochoka. Booker ndio kabisa, nilihisi atakua amekufa kwakua hata kauli yake sikuisikia. Nilirudi ndani na kukaa tu huku ladha yote ya kukaa kwnye kile kisiwa ikiwa imenipotea.

Usiku nililala na kuamshwa na malikia kwa ajili ya kupata chakula cha usiku. Nilifurahi baada ya kuona hajanigusa wala kuniambia kuwa alikua anahitaji tufanye mapenzi. Alipolala tu, niliamka na kwenda tena nje kwa ajili ya kumtega Shenaiza kwa sababu nilihisi kuwa na msichana huyo kuna uwezekano mkubwa sana wa kupata nafasi ya kuondoka kisiwani hapo.

Haikuchukua muda mrefu toka nimekaa hapo, upepo mkali ulivuma na ulipotulia nilishtuka baada ya kuguswa bega, nilipogeuka nilimuona Shenaiza akiwa amevaa mavazi kama ya kihindi huku mpasuo mkubwa uliokua unanionyesha paja lake ukinifanya nishtuke kidogo. Aliachia tabasamu baada ya kuniona na kunifanya nikiri moyoni kuwa yule dada alikua ni mzuri sana.

“usiniambie kuwa upo hapa kwa ajili yangu.” Aliongea maneno hayo na kuzidi kutabasamu.

“ni kweli……..”

kabla sijamalizia sentensi yangu niliyokua nataka kuongea, aliniziba mdomo na kunishika mkono. Ghafla nikajikuta katika mazingira mengine mazuri yaliyokua na maua yawakayo taa.

Alionekana ni mwenyeji huko kwakua alikua anaruka ruka huku mimi nikibaki nimeduwaa. Hakika ile sehemu ilikua nzuri na ya kupendeza sana.

“njoo.” Ainiita baada ya kwenda kukaa kwenye jiwe moja kubwa lilikua pembeni ya maji yatiririkayo kutokea kwenye makorongo yaliyokua juu.

Nilimfuata bila kusita na kukaa nae karibu.

“toka nimeanza kukutana na wavulana kutoka sehemu mbali mbali duniani waliokuja kukitembelea kisiwa hiki, sijawahi kumuona mwanaume aliyenivutia zaidi yako wewe.” Aliongea yule dada na kuniangalia kisha akaina chini kama vile alikua ananionea aibu.

“sielewi ni msukumo gani ulionipata mpaka nikajikuta nakupenda Hijja…. Mpaka kuna wakari mwengine huwa natami nikuchukue bila ridhaa yako. Ila huwa nahofia kuchukiwa na wewe. Nakuhitaji sana katika maisha yangu. Nakupenda sana kutoka kwenye moyo wangu… naomba usinikatili hata kama mimi sio kiumbe kama wewe.” Aliongea na kuanza kulia. Nilimtazama na kuingiwa na imani. Nilihisi ukweli uliokua moyoni mwake kwa jinsi alivyokua naziwasilisha hisia zake kwangu mimi. Nilijikuta natamani kumshika. Ila uoga ulinizuia kufanya hivyo. Machozi yake yalinifanya nimuinue na kumtazama msichana huyo mzuri aliyekua analia kwa ajili ya penzi langu.

“nimekuelewa Shenaiza,..ila mimi sina mamlaka yoyote kwenye kisiwa hiki,.. sijui hata kama safari ya maisha yangu itaishia wapi nikiwa huku. Sina raha kabisa. Sitamani kuishi huku ila kuondoka tu ndio siwezi. .. unafikiri utaniweka katika hali gani kama malikia atagundua kama nina uhusiano na wewe?” nilijibu kwa upole huku nikimfuta machozi kwa viganja vyangu.

“usijali kuhusu usalama wako.. pia hata kama hutaki kuishi huku,.. nipo tayari kukurudisha ulipotoka kama utakubali tu kuishi na mimi.” Aliongea maneno yaliyonifanya ninyanyuke na kuanza kuchekelea.

“kweli?.... hata leo tunaweza kutoroka?” niliongea huku nikionyesha shauku ya kuondoka pale.

“wewe kubali kuwa na mimi.. yote hayo yanawezekana.” Aliongea na kunifanya nizidi kufurahi.

Sikmjibu chochote zaidi ya kumfuata pale alipo na kunaza kumpa mabusu matakatifu pande zote za mwili wake.

Miitiko ya mahaba aliyokua ananiitikia ilizidi kunipa mshawasha wa kufanya tendo hilo bila kufosiwa.

Kwa ridhaa yangu na yake, tulianza kula tunda taratibu huku I love you, I love you too zikiwa nyimbo zetu mimi na yeye. Hatukujua tulitumia muda gani, ila tulikuja kukurupuka wote pakiwa peupe.

Tulipatwa na mshtuko kwakua tulijua kutakua kumeshawaka huko kwa malikia.

“tutafanyaje?” niliuliza kwa uwoga baada ya kuona mpaka Shenaiza mwenyewe ameshika kichwa kama ishara ya kutoelewa nini afanye.

“tunatakiwa kutoroka haraka sana… hakuna njia nyingine.” Aliongea Shenaiza huku akiwa anavaa nguo zake haraka kuashiria kua kulikua kuna haja ya kuharakisha jambo hilo.
 
hongera best,nani kakufundisha?ila 9 sijaiona
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom