Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,746
- 25,638
HADITHI: .. JOTO LA MAPENZI
SEHEMU: 01
MTUNZI: Ally Mbetu ‘DrAmbe’
SIMU: 0713 646500
UTANGULIZI
Kutokana na wingi wa watu kuwaorodhesha kabla ya kuwaingiza kwenye kundi la Whatsapp mtaendelea na hadithi kwenye FB likiwa tayari tutahamia huko kila aliyetuma namba ataingia msihofu. Leo tunaanza na kitu kipya tuwe pamoja.
JASHO LA MOYO
Kutokana na maji kuingia kwa kasi katika shimo alilokuwemo kijana Ambe yalimzindua kutokana na kutereza na kudondokea humo wakati wakiwakimbia askari magereza na kupoteza fahamu. Ilikuwa katika jaribio la kutoroka kwa bahati mbaya aliangukia kwenye shimo.
Rafiki ya Aloys Mabina hakutaka kumwacha alijitahidi kumwamsha ili amtoe shimoni, lakini aligundua amepoteza fahamu hivyo asingeweza kuendelea kuwepo eneo lile kwa kuhofia askari wanaowatafutakumkuta eneo lile.
Aliona kama angeendelea kuwepo pale lazima askari wanao wakimbiza wangefika eneo lile na kumkamata. Hivyo aliendelea na safari kuwakimbia na kumwacha rafiki yake ndani ya shimo.
Ambe baada ya kuzinduka taratibu alijitoa kwenye shimo huku mvua ikiendelea kupiga kwa kasi, shimo halikuwa refu sana hiyo ilimsaidia kutoka nje kwa urahisi. Alijikuta akiwa njia panda na kushindwa afanye nini arudi gerezani au aendelee kukimbia.
Wazo la kurudi lilimtisha kidogo kutokana kuogopa kuulizwa juu ya mwenzake Mabina aliyekuwa swahibu wake mkubwa gerezani. Walikuwa wamefanya tukio baya la kutoroka na siraha baada ya kumkaba askari magereza na kukimbia na bunduki ambayo ilikuwa inakwenda kutimiza azima ya rafiki yake Mabina ya kuua ili kutimiza kisasi.
Ambe na Mabina walikuwa na matukio ya kufanana yaliyowafanya waingie gerezani na kila mmoja kufungwa miaka saba. Lakini kila mmoja alikuwa na njia yake iliyomwingiza gerezani Mabina aliapa akitoka lazima alipe kisasi kwa kuwaua wabaya wake na ndiyo sababu ya kutoroka na siraha.
Lakini ilikuwa tofauti kwa Ambe, pamoja na kufanyiwa unyama mkubwa lakini aliapa hata lipiza zaidi ya kumuachia Mungu. Mabina hakuwa hivyo hakutaka kabisa kusikia eti mtu anakutendea unyama unamshtakia Mungu wakati una uwezo wa kulipa kisasi.
Baada ya kumweleza rafiki yake sababu iliyomwingiza gerezani ambayo ilikuwa ni uonevu aliapa akitoka lazima aue tena kwa risasi. Ambe pamoja na kumsihi rafiki yake asilipe kisasi hakusikilizwa. Mabina alisema toka alipofanyiwa unyama ule na mwisho wa yote kufungwa bila kosa miaka saba. Asinge msamehe mtu aliapa lazima atalipa kisasi tena cha damu.
Ambe akiwa anatoka kwenye shimo huku mvua ikiendelea kumnyeshea. Moyoni alijikuta akijilaumu maamuzi wa rafiki yake wa kumpiga askari na kuichua bunduki ambayo alimwambia ndiyo siraha aliyoitafuta kwa muda mrefu.
Katika muda wote waliokuwa gerezani Mabina aliapa akitoka gerezani lazima aue ili anyonge na kuamini kile ndicho kitakuwa kifungo cha kweli kwake. Matatizo ya rafiki yake hayakuwa na tofauti na yake ya kutendewa unyama na familia ya rafiki yake wa kike na mwisho wa yote kufungwa gerezani miaka saba bila kosa lolote kisa mapenzi.
Tofauti ya kuingia gerezani kwa Ambe na Mabina ilitofautiana, Mabina alitangulia kuingia kwa mwezi mmoja hivyo hata muda wao wa kutoka ungepishana kwa mwezi mmoja.
Ambe akiwa bado yupo njia panda aelekee wapi kwa vile pori lile lilikuwa geni kwake japokuwa hakutaka kurudi gerezani. Alikumbuka kauli za rafiki yake baada ya kumsimulia mkasa uliomwingiza gerezani:
“Ambe nakuhakikishi siwezi kuwasamehe wote walionifanyia unyama, hawezi kutudhurumu mali yetu, wamuue baba yangu na mimi kufungwa miaka saba bila kosa kisa tu nilikuwa nikijua mengi juu ya ugomvi wa baba na jirani yake juu ya mpaka wa nyumba.
“Najua sina uwezo wa kipesa, lakini lazima nimuue kwa risasi kama alivyomuua baba yangu.”
“Atapata wapi bunduki?” Ambe alimuuliza rafiki yake.
“Hapa hapa gerezani.” Mabina alijibu kwa kujiamini.
“Hapa hapa gerezani! Utaipata vipi?” Ambe alishtuka.
“Utaona tu.”
Siku ilipofika walikuwa kwenye kazi za nje kutokana na kubakiza muda mchache wa kuwepo gerezani. Wafungwa wengi walipewa kazi za nje, yeye akiwa amebakiza miezi miwili na Mabina mwezi mmoja wa kutoka gerezani. Wakiwa eneo lililojificha walilopangiwa Ambe na Mabina kukate miti huku askari magereza akiwa mbali kidogo.
Mabina alimwambia Ambe amwite askari kwa sauti ya juu, naye alifanya hivyo kwa kupaza sauti kumwita askari. Askari alifika haraka eneo aliloitiwa alipofika alishangaa kumuona Mabina akigaagaa chini kama mtu aliyekuwa akiumwa kitu. alipomuuliza Ambe ambaye hakuwa na jibu. Alipomwinamia ili kutaka kujua anaumwa nini, Mabina alinyanyuka na kukaba askari huku Ambe akishangaa. Baada ya kumkaba mpaka kupoteza fahamu alichukua bunduki na kumlazimisha Ambe waondoke.
“Twende wapi?” Ambe aliuliza.
“Ukibaki shauri yako utaulizwa nimekwenda wapi, najua hautakuwa na jibu kwa vile sisi ni marafiki wakubwa watajua nawe unahusika hivyo itaozea gerezani.”
Ambe alijikuta akimfuata Mabina aliyeanza kukimbia kuingia porini, kwa vile hakuwa amejiandaa baada ya mwendo wa masaa matatu bila kupumzika pumzi ilikata na kujikuta akianza kuona kizunguzungu kwa bahati mbaya pembeni na sehemu aliyokuwa amesimama kulikuwa na shimo aliangukia ndani.
Mabina alijaribu kumsaidia kumtoa shimoni lakini aligundua amepoteza fahamu hakuwa na jinsi zaidi ya kumwacha ili asije kukamatwa na askari watakao kuwa wakimtafuta. Baada ya saa saba kupita mvua zilianza kunyesha, maji ya mvua yaliyokuwa yakiingia shimoni ndiyo yaliyomzindua Ambe.
Muda aliotoka shimoni ilikuwa saa usiku kiza kilianza kuimeza nuru ya mchana. Alikumbuka maneno ya Mabina kuwa kama atakamatwa atafia gerezani, aliamua kuendelea na safari yake japo hakujua anaelekea sehemu gani. Wakati huo mvua ilikuwa akiendelea kunyesha, alijiona ni kiumbe kilichoandamwa na mikosi baada ya kunyang’anywa mchumba wake na kuozwa mtu mwingine bila idhini yake bado ameishia kufungwa gerezani.
Akiamini baada ya miezi miwili atakuwa uraiani na kuuapia moyo wake pamoja na yote aliyotendewa aliusihi moyo wake usilipe kisasi. Lakini mtu aliyemtegemea kuwa rafiki na msiri wake, mwisho wa siku amemwingiza kwenye matatizo makubwa ya kutafutwa na serikali kwa makosa matatu kuua kutoroka gerezani na wizi wa siraha.
Moyo ulimuuma na kutani kulia, alijiuliza pale alipo atatokea wapi na atawezaje kuikwepa serikali ambayo ina mkono mrefu. Alijua kama rafiki yake Mabina atatimiza adhima yake ya kuua na kunyongwa atakuwa ametimiza ametimiza kile alichokipanga kwa muda mrefu.
Lakini kwa upande wake, baada ya kufungo alipanga kuishi maisha mapya.
Alizidi kutembea kuingia ndani ya msitu ambao kwa upande wake ulikuwa mgeni kwake. Ghafla alijikuta akipata wazo la kijasiri la kurudi gerezani kuwaeleza ukweli kuwa si yeye bali rafiki yake ambaye wamejuana gerezani tu.
Baada ya kutembea kwa hatua kama kumi alishangaa kuona mianga ya tochi zaidi ya nne ikisogea sehemu aliyokuwepo. Wasiwasi ulimjaa na kushindwa kuelewa wale ni kina nani na mbona kama watu wanaotafuta kitu. Mwanga ulipokuwa unakimkaribia aliamua kujificha kwa kupanda juu ya mti uliokuwa karibu.
Alitulia juu ya mti ili watu wale wapite kwa kuhofia huenda ni askari waliokuwa wakiwatafuta. Watu wale walipofika chini ya mti ule aligundua kweli walikuwa askari magereza ambao walionesha walipita kitambo kuwatafuta na kumpita alipokuwa ameangukia kwenye shimo na kupoteza fahamu.
Aliwasikia wakizungumza:
“Tumefanya kazi ya ziada bila hivyo tungekufa wote.”
“Lakini katutia hasara kifo cha mtu mmoja hakilingani na askari wetu wawili.”
“Lakini rafiki yake ndiye anaonekana amekimbia na siraha lazima tumsake kwa udi na uvumba.”
Maneno yale kidogo yamfanya Ambe aanguke juu ya mti aliokuwa amepanda, aliamini kabisa rafiki yake kipenzi Mabina ameuawa na kuwaua askari magereza wawili. Kilichomshangaza ni kauli yao kuhusu kutoonekana kwa bunduki aliyochukua Mabina. Ile ilimshtua kidogo na kujiuliza rafiki yake atakuwa ameificha wapi.
Kauli ya kwanza anatafutwa yeye ambaye ndiye anayesadikiwa ameficha siraha ilimvunja nguvu sana na kuamini kama atarudi gerezani basi atakuwa amejiingiza mwenyewe kwenye kinywa mamba.
Alitulia juu ya mti akimuomba Mungu amuepushie mbali balaa lile, askari wale walichelewa chini ya mti ule kutokana na mmoja kujisaidia haja ndogo, baada ya kumaliza aliendelea na safari yao. Twambe hakuteremka mpaka ya nusu saa na kuona hakuna haja ya kwenda kujisalimisha baada ya kuonekana kuwa ndiye aliyeficha siraha hivyo wasinge muelewa.
Kila lililokuwa mbele yake aliona ni mtihani mzito ambao kwake aliamini haukuwa na jibu la mara moja. Muda ulikuwa umekwenda na kiza kilikuwa kimeingia ambacho hakikuwa kikali sana, mwezi ulikuwa umemezwa kidogo na mawingu. Hali ile ilimfanya aone kidogo sehemu aliyokuwa akienda.
Alitembea kuelekea mbele bila kujua anakwenda wapi kutokana na eneo lote kuwa mbuga yenye miti mingi. Kwa vile hakuwa na saa hakuja muda ule ilikuwa saa ngapi , alipata ujasiri na kuamua kusonga mbele na kuwa tayari kwa lolote kwa kuamini hakufanya jambo lolote baya na Mungu angemsaidia.
Alitembea asiku kucha na kujikuta akichoka sana kutokana na kutembea kwenye baridi kali kutokana na mvua kunyesha sehemu kubwa. Sehemu moja aliyokuwa na bonde alisikia watu wakizungumza:
“Sasa jamani tutakaa mpaka saa ngapi tukitafuta mtu tusiyejua amekimbilia wapi?” Ilikuwa kauli iliyoonesha kumbe askari wengi walikuwa wamesambaa eneo kubwa la pori lile kumtafuta.
“Hivi angalie tumeisha poteza watu wawili kwa mtu asiye na siraha sasa mwenye siraha si tutakufa wote. Kama mtu ametoroka alitakiwa atafutwe kwa njia nyingine,” alimsikia askari mwingine akizungumza.
Ambe alijikuta kwenye wakati mgumu baada ya kugundua anatafutwa kila kona na kama atakamatwa atakufa kwa kipigo kutoka kwa askari wenye hasira hasa baada ya kuuawa askari wawili kutokana na maelezo yao. Alijiuliza kote alipopita huenda aliwapita wengine ambao walikuwa wamepitiwa na usingizi hivyo kupita bila kumuona.
Kauli za wale askari ilionesha wameisha kata tamaa wapo pale kwa kutimia wajibu lakini aliamini hawezi kumuoa. Aliachana na njia iliyokuwa na sauti ya askari na kuanza kuifuata iliyokuwa ikielekea bondeni ambako kulikuwa kunatisha sana.
Itaendelea Ijumaa