Hadithi: Bruno the Fisherman

Hadithi: Bruno the Fisherman

HaMachiach

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2015
Posts
3,444
Reaction score
6,201
Bruno The Fisherman (Mvuvi Bruno)
Mtunzi. Nyemo Chilongo
Epsod 1

Hali ya hewa angani ilibadilika ghafla, jua kali lililokuwa likiwaka lilifunikwa na mawingu mazito ya kijivu yaliyokuwa yametanda angani. Kwa jinsi hali ilivyokuwa ikionekana, kila mmoja aliamini kwamba mvua kubwa ingekwenda kunyesha.
Mawimbi makubwa kiasi yalianza kupiga kwa nguvu ufukweni, kila mtu aliyekuwa akiiona hali hiyo aliogopa na kuona kwamba siku hiyo mvua hiyo ingekuwa kubwa kuliko hata zile ambazo ziliwahi kunyesha katika Kijiji cha Guolduvai kilichokuwa nchini Kenya pembezoni mwa bahari ya Hindi.
Watu waliokuwa wakiogelea, wakatoka majini na kuelekea nyumbani kwao, kila mmoja alionekana kuwa na hofu kwani hali iliyokuwa ikionekana siku hiyo ilikuwa ni ya hatari tupu.
Wavuvi waliokuwa wakivua samaki kama kawaida yao kwa nyakati za mchana, haraka sana wakaanza kurudisha mitumbwi yao kijijini kwani kwa kuwa walikuwa wakitumia mitumbwi ambayo haikuwa na nguvu ya kupambana na mawimbi makubwa, wakahisi kabisa kwamba kama mvua hiyo kubwa ingewakuta baharini basi hali ingekuwa mbaya zaidi.
Wakati kila mtu akiogopa mvua kubwa iliyokuwa ikitarajiwa kunyesha, kijana masikini, aliyevalia fulana iliyokuwa imechanika ambayo kwa mbele iliandikwa 50 Cent huku ikiwa na picha kubwa ya mwanamuziki huyo alikuwa amesimama katika kichaka kilichokuwa kijijini hapo huku akiangalia huku na kule.
Kwa muonekano wake tu haikuwa kazi kubwa kugundua kama kijana huyo alikuwa masikini wa kutupwa. Mbali na fulana yake hiyo iliyoonekana kuchakaa, chini alivalia pensi, kandambili zilizokuwa tofauti huku nywele zake zikiwa timtim.
Kijana huyu aliitwa Bruno. Alikuwa kijana mkimya kijijini hapo, alimheshimu kila mtu aliyekuwa akiishi mahali hapo. Hakuwa mtu aliyekuwa na furaha, maisha yalimpiga, wazazi wake ambao walifariki miaka miwili iliyopita kwa kuzama na mtumbwi uliokuwa ukielekea Mombasa hawakumuachia kitu, alikuwa mikono mitupu huku akiendelea kufanya kazi ya uvuvi katika bahari ya Hindi.
Alisimama mahali hapo huku macho yake yakiendelea kuangalia huku na kule. Hakuonekana kuogopa mvua kubwa iliyokuwa ikitarajiwa kunyesha, kile alichokuwa akikitaka ni kuongea na msichana aliyekuwa akimpenda kwa moyo wa dhati, Sharifa ambaye alimwambia kwamba angefika mahali hapo muda si mrefu.
Mpaka mvua kubwa inaanza kunyesha bado msichana huyo hakuwa ametokeza. Mvua iliyoambatana na upepo mkali ilimnyeshea lakini hakukubali kuondoka, aliendelea kusubiri mahali pale mpaka alipomuona msichana huyo akija kutoka kule kijijini huku akikimbia.
Uso wake ukajawa na tabasamu, kumuona Sharifa mahali hapo ndiyo lilikuwa lengo lake. Kila alipomwangalia, uzuri wa msichana huyo ulikichanganya kichwa chake. Sharifa akamsogelea mpaka pale alipokuwa, kama alivyokuwa Bruno, hata naye alikuwa amelowanishwa na mvua iliyokuwa ikiendelea kunyesha.
Sharifa alipomfikia Bruno, akamsogelea, akamkumbatia na kuangaliana pasipo kuzungumza kitu chochote kile. Bruno alikuwa na mambo mengi ya kuzungumza na msichana huyo aliyekuwa amesuka mabutu kichwani mwake na viatu vyake ya chachacha vikiwa miguuni mwake.
“Nimekusubiri sana!” alisema Bruno huku akimwangalia Sharifa, walipokuwa wamesimama, bado mvua kubwa iliendelea kuwanyeshea.
“Pole sana! Nimechelewa kidogo lakini sidhani kama umekasirika,” alisema Sharifa kwa sauti ndogo huku akimwangalia mpenzi wake huyo kwa jicho lililoonyesha mahaba yote kwake.
“Hakuna! Siwezi kukasirika! Ulizungumza na wazazi wako?” aliuliza Bruno.
“Ndiyo! Nilizungumza nao, waliniambia vilevile.”
“Kwamba?”
“Hawataki kuona nikisimama na kuongea nawe. Kiukweli wanakuchukia, wanasema kwamba huna kitu, utanilisha nini? Utanipa nini? Huna chochote kile,” alisema Sharifa huku akimwangalia Bruno ambaye nguvu zilimuisha baada ya kuambiwa hivyo.
Moyo wake ulikuwa na hasira tele, alimpenda sana Sharifa lakini kipingamizi kikubwa kilikuwa ni nyumbani kwa msichana huyo. Hakukubalika kwa sababu tu alikuwa masikini, wazazi wa msichana huyo walimchukia kupita kawaida.
Sharifa alikuwa mzuri wa sura, alipendwa na kila mtu kijijini hapo, wanaume walimfuatilia, tena wale waliokuwa na mitumbwi yao ambao kila siku walipata pesa nyingi baada ya kuvua samaki.
Wote hao, Sharifa hakuwakubali, kwake, moyo wake ulikuwa kwa mtu mmoja tu, Bruno ambaye alikuwa masikini wa kutupwa. Alichokuwa akikiangalia Sharifa hakikuwa pesa wala mali, hakuangalia mambo mengine zaidi ya mapenzi. Aliamini kwamba penzi lilikuwa kila kitu, hata kama Bruno hakuwa na kitu lakini aliamini kwamba angeweza kumpa furaha aliyokuwa akiihitaji.
“Niambie tufanye nini! Sitaki kuolewa na mtu yeyote, ninataka kuolewa na wewe tu. Niambie Bruno unataka tufanye nini?” aliuliza Sharifa huku akitokwa na machozi yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwake ila ilikuwa vigumu kuyaona kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha.
“Sijui tufanye nini! Labda unipe muda wa kujifikiria!”
“Hatuna muda! Sema tufanye nini! Au tutoroke?”
“Tutoroke?”
“Ndiyo!”
“Kwenda wapi?”
“Popote pale. Nitahitaji kuwa nawe, sitaki kuona nikikukosa. Bruno, ninakupenda sana, wewe ndiye kila kitu katika maisha yangu, siwezi kuishi bila wewe,” alisema Sharifa, hapohapo akamkumbatia tena Bruno.
“Sharifa! Sina pesa, sina kitu chochote kile. Nipo mtupu kama unavyoniona, hata tukitoroka, itakuwaje huko tutakapokwenda?” aliuliza bruno.
“Vyovyote itakavyokuwa. Naomba tutoroke. Sitaki kukupoteza,” alisema Sharifa.
Kwa jinsi alivyoonekana, Sharifa alikuwa tayari kutoroka mahali hapo. Moyo wake ulichoka na alihitaji kuendelea kuishi na mpenzi wake huyo. Hakutaka kubaki kijijini pale, wazazi wake walikataa yeye kuolewa na Bruno kwa kuwa tu alikuwa masikini. Hilo lilimuumiza mno na kitu alichokuwa amekifikiria ni kutoroka kijijini hapo.
Kwa Bruno ilikuwa ngumu kukubaliana naye. Hakuwa na kitu, kilichomuumiza kichwa si kutoroka kijijini hapo bali ni maisha baada ya kutoroka. Alimwambia wazi Sharifa kwamba huo haukuwa uamuzi mzuri, walitakiwa kubaki hapohapo kijijini huku wakiamini kwamba kuna siku maisha yangekuwa kama wanavyotaka yawe.
“Hatutakiwi kutoroka. Kama tatizo ni pesa, tutatafuta pesa, tutakuwa na pesa na kufanikiwa. Sharifa! Sitaki nikupoteze, kama kweli wazazi wako wanasema siwezi kukuoa kwa sababu sina pesa. Nitatafuta pesa tu, tena kwa nguvu zote,” alisema Bruno huku akimwangalia mpenzi wake huyo.
Japokuwa ilikuwa vigumu kumshawishi msichana huyo lakini mwisho wa siku wakakubaliana kwamba hakukuwa na sababu ya kutoroka zaidi ya Bruno kupambana mpaka kuhakikisha kwamba anapata pesa na kumuoa msichana huyo.
Walizungumza kwa dakika kadhaa, walipomaliza, Sharifa akaondoka kurudi nyumbani kwao. Huku nyuma Bruno alichanganyikiwa, bado hakufahamu ni kitu gani alitakiwa kufanya.
Hali iliyokuwa ikiendelea ilimtisha mno, hakutamani kuona akimkosa msichana huyo kisa tu hakuwa na pesa. Alitaka kupambana mpaka kuhakikisha anapata pesa na kumchukua msichana huyo.
Maisha yaliendelea, kama kawaida kila siku alikuwa akiondoka kuelekea baharini na rafiki yake, Abdul huku wakiwa kwenye mtumbwi wao. Huko, hasa nyakati za usiku walikuwa wakivua samaki na kwenda kuwauza kijijini kwao.
Abdul alikuwa akifahamu kila kitu. Huyo ndiye alikuwa rafiki yake wa karibu, walipendana na kupeana siri ya kila kitu kilichokuwa kikiendelea katika maisha yake. Abdul alimuonea huruma Bruno, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alimpenda Sharifa, alijitahidi kufanya kila liwezekanalo kwa msichana huyo lakini bado wazazi wake hawakutaka kabisa kumuona binti yao akiwa na kijana masikini kama yeye.
“Ila kuna siku nitapata pesa tu na kumuoa Sharifa,” alisema Bruno huku akimwangalia rafiki yake huyo, wakati huo walikuwa kwenye mtumbwi wao, chemli ilikuwa ikiwaka, walikuwa wakielekea mbali kabisa na bahari.
“Unahisi utafanikiwa kwa kupitia hawa samaki?” aliuliza Abdul.
“Inawezekana! Pia nitaanza kuangalia mpango wa kuelekea mjini Nairobi kwenda kuuza huko. Abdul, hujui ni kwa kiasi gani nampenda Sharifa,” alisema Bruno.
“Najua. Unampenda sana. Ila hili suala la wazazi wake linaniumiza sana kichwa,” alisema Abdul.
“Najua! Ila nitapambana tu!”
Walikuwa wakipiga stori huku wakiwa safarini kuvua. Hayo ndiyo yalikuwa maisha yao ya kila siku. Walivua usiku kucha, walipigwa na maji, walipigwa na baridi na asubuhi walirudi kijijini huku wakiwa na samaki wa kuwauza kwa siku mbili.
Mtu wa kwanza kabisa aliyekuwa akiwapokea na kuwasaidia kutoa samaki kwenye mtumbwi alikuwa Sharifa. Alikatazwa kuwa karibu na Bruno lakini hilo halikumfanya kumsaidia kazi hiyo. Wazazi wake walisema sana lakini hakutaka kusikia, alijitoa kwa kila kitu, kama kupigwa kwa ajili hiyo, alipigwa leo na kesho kama kawaida alifanya vilevile.
“Pole sana mpenzi,” alisema Sharifa huku akimsogelea Bruno alipokuwa. Alionekana kuwa hoi.
“Ahsante sana!”
Wakawachukua samaki, wakamuita dalali na kwenda kutafuta wateja huku wakiwa wamekwishaelewana naye kabisa. Wakaondoka mahali hapo na kwenda nyumbani kwake, katika nyumba ya nyasi, ndani kitanda cha teremka tukaze na kutulia hapo.
Walibaki wakiwa wameshikana mikono, waliangaliana kwa bashasha huku kila mmoja akionekana kuwa na hamu na mwenzake. Sharifa akaanza uchokozi kwa kukichezea kifua cha Bruno aliyekuwanaye kitandani hapo.
“Ushaanza...” alisema Bruno huku akitoa tabasamu pana.
“Kwani kuna tatizo mpenzi?” aliuliza msichana huyo, hapohapo akaanza kumvua fulana Bruno.
Huku tayari akiwa amekwishavuliwa fulana yake, mara wakaanza kusikia sauti ya Adul kutoka nje ikimuita.
“Bruno...Bruno fungua mlango...” ilisikika sauti ya Abdul.
Wote wakashtuka, haraka sana Bruno akafungua mlango na kumwangalia rafiki yake huyo. Alikuwa akihema kwa nguvu, akamuuliza tatizo lilikuwa nini.
“Mzee Jumanne anakuja na panga. Kimbia! Anakuja kukumaliza,” alisema Abdul. Bruno alivyosikia hivyo tu, haraka sana akachukua fulana yake lakini hata kabla hajatoka tu ndani ya kijumba chake cha nyasi, mzee huyo akatokea na kusimama mlangoni. Jasho lilikuwa likimtoka, alionekana kuvimba kwa hasira, mwili ulikuwa ukimtetemeka.
Kitandani pale, alimuona binti yake akiwa amekaa, hasira zikamzidi zaidi, akalishikilia vizuri panga lake tayari kwa mashambulizi. Bruno aligundua hilo, akaona kabisa kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake kwani kwa jinsi mzee huyo alivyoonekana, hakuwa na masihara hata kidogo.
***
Mzee Jumanne alisimama mbali kidogo na nyumba yake, macho yake yalikuwa yakiangalia baharini namna mitumbwi ilivyokuwa ikiingia kijijini hapo baada ya wavuvi kutoka kuvua samaki. Moyo wake ulikuwa na hasira kali, alimchukia Bruno, kati ya watu wote aliotokea kuwafahamu maishani mwake, mwanaume huyo alikuwa mtu wa kwanza kumchukia kwa chuki kubwa moyoni mwake.
Alimchukua binti yake, hakupendezwa na jambo hilo kwa sababu tu alikuwa kijana masikini ambaye alikuwa na uhakika kwamba angempeleka mtoto wake kwenye mzigo mzito wa umasikini kitu ambacho hakuwa radhi kukiona kikitokea.
Alimkataza Sharifa kuwa na Bruno lakini binti huyo hakutaka kukubali hata mara moja, alimwambia baba yake wazi kwamba kuachana na Bruno lilikuwa jambo lisilowezekana hata kidogo na alikuwa tayari hata kufa lakini si kumwacha mwanaume huyo.
Maneno hayo yalimchoma mno mzee Jumanne kiasi kwamba akaona kitu pekee cha kumfanya binti yake aachane na Bruno kilikuwa ni kumuua mwanaume huyo tu. Hakuogopa, alikuwa tayari kukaa gerezani hata kifungo cha maisha lakini si kuvumilia kumuona Bruno akiendelea kuvuta pumzi ya dunia na binti yake aliyekuwa akipendwa na wanaume wengi.
Sharifa alimpenda sana Bruno, hakuwa radhi kuona akichukuliwa na mwanaume mwingine, katika maisha yake kila siku alimwambia wazi kwamba ilikuwa ni bora kufa lakini si kuona akiingia kwenye mapenzi na mwanaume mwingine.
Mzee Jumanne alijaribu kwa nguvu zote kuwaleta wanaume waliokuwa na pesa kwa lengo la kumchukua binti yake lakini wote hao walishindwa kuuteka moyo wa binti huyo, kwake, hakukuwa na kitu kilichokuwa na thamani zaidi ya moyo wake kwa Bruno.
Mzee Jumanne alipanga siku hiyo kuwa ya mwisho kumuonya binti yake kutembea na Bruno, alikuwa na uamuzi mmoja tu kichwani mwake, kumuua mwanaume huyo na yeye kuondoka zake hapo kijijini.
Alitulia pembeni kabisa mwa bahari, macho yake hayakuacha kuangalia kule ambapo mitumbwi ilikuwa ikiingia. Alitulia, alimuona binti yake, Sharifa akiwa karibu na bahari, macho ya msichana huyo yalikuwa yakiangalia baharini.
Alijua kabisa kwamba Sharifa alikuwa akimsubiri Bruno ili ampokee na kuondoka naye. Wala hazikupita dakika nyingi, mtumbwi wa Bruno ukaanza kuonekana kwa mbali, alijitahidi kujizuia kwani tayari hasira zilikuwa zimempanda na hata panga alilokuwa amelishika lilikuwa likitetemeka kwa kuwa mkono wake ulikuwa ukitetemeka kwa hasira.
Akamuona Bruno akiteremka, akamuacha rafiki yake, Abdul na yeye kuondoka na binti yake. Moyo wake ukachoma, hasira zikampanda, akajipa nguvu kwamba alitakiwa kusubiri mpaka watakapoondoka na kwenda huko walipotaka kwenda.
Baada ya dakika tano, naye akatoka mahali pale alipokuwa na kuanza kwenda nyumbani kwa Bruno ambapo aliamini kwamba binti yake alikuwa humo.
Abdul alimuona mzee Jumanne, hakutaka kuchelewa, akaanza kukimbia kuelekea kwa Bruno kwa lengo la kumwambia kwamba mzee huyo alikuwa njiani akija na panga.
Wakati Bruno akijiandaa kukimbia, tayari mzee huyo alikuwa amekwishafika ndani ya kibanda kile huku akiwa na panga lake mkononi.
Bruno akabaki akitetemeka, alishikwa na hofu, kwa jinsi mzee Jumanne alivyokuwa akionekana ilionyesha kabisa alikuwa na hasira kali na kama asingefanya harakati za kukimbia mahali hapo basi angeweza hata kumkatakata kwa panga.
Hakukuwa na sehemu ya kukimbilia, alitakiwa kupitia palepale mlangoni aliposimama mzee huyo. Alijua kuwa kwa nguvu alizokuwanazo mzee Jumanne asingeweza kumzuia hata kidogo. Hakutaka kujiuliza sana, hapohapo akamvamia kwa kasi, wote wakadondoka, haraka sana Bruno akasimama na kuanza kukimbia. Mzee Jumanne hakutaka kukubali, akasimama na kuanza kumkimbiza kwa panga.
Ulionekana kama mchezo au filamu fulani hivi. Bruno alikuwa akikimbia kwa kasi kubwa kwani alijua dhahiri kwamba kama angesimama basi angeweza kukatwakatwa na lile panga. Akaongeza kasi zaidi, kasi ambayo mzee Jumanne hakuweza kumfikia hata kidogo.
Mzee huyo akasimama, akashika kiuno huku akihema kama mbwa, macho yake yalikuwa yakimwangalia Bruno aliyezidi kukimbia kuelekea mtaani.
Watu wote waliokuwa wakifuatilia tukio lile walishangaa na wengine kucheka kabisa. Walifurahishwa na jinsi mzee Jumanne alivyoinama na kushika magoti, panga lilikuwa chini huku akihema kwa nguvu.
Bruno aliendelea kukimbia mpaka alipofika sehemu ambayo alihisi kwamba ilikuwa salama, akasimama na kupumzika. Hakujua ni mahali gani alitakiwa kwenda, alitulia huku akiangalia kila kona kuona kama mzee huyo alikuwa akija au la.
Maumivu aliyokuwanayo moyoni mwake hayakuelezeka hata kidogo. Aliumia kuona akimpenda msichana ambaye wazazi wake walimchukia kwa sababu tu ya umasikini aliokuwanao.
Siku hiyo hakurudi nyumbani, aliondoka na kuelekea nyumbani kwa rafiki yake, James ambapo akakaa huko na kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea.
Hakutaka kurudi nyumbani kwake kwani alijua kwamba piga ua mzee Jumanne ilikuwa ni lazima kurudi nyumbani hapo kumtafuta. Alikaa huko kwa siku hiyo na baadaye kuonana na Abdul na kutaka kusikia kilichotokea.
“Sharifa alipigwa sana na baba yake,” alisema Abdul huku akionekana kuumizwa na kile kilichotokea.
“Acha masihara!”
“Yule mzee anapiga. Angemuua bila watu kumpoza,” alisema Abdul.
“Daah!”
“Ila ana msimamo mno. Alipigwa na kupigwa lakini bado alimwambia baba yake kwamba anakupenda na kamwe asingeweza kukuacha, yaani kila mtu alikuwa akishangaa,” alisema Abdul.
Moyo wa Bruno ukauma zaidi, kitendo cha kuambiwa kwamba mpenzi wake alipigwa mno na baba yake kisa yeye, kiliuvuruga kabisa moyo wake kwani miongoni mwa vitu ambavyo hakutaka kabisa kuona vikitokea ni kuliona chozi la mpenzi wake.
Japokuwa alikuwa nje ya nyumba yake lakini aliendelea kufanya kazi ya uvuvi kama kawaida. Kila siku jioni aliondoka na mtumbwi wa mvuvi mwenzake, James ambapo walikwenda mpaka baharini ambapo huko walikutana na Abdul na kisha kuingia kwenye mtumbwi wake na kwenda kuvua kama kawaida.
Akawa akiishi kwa namna hiyo, hata alipokuwa akirudi, alipofika njiani kabisa alikuwa akikutana na akina James, anaingia kwenye mtumbwi wao na kurudi.
Alifanya hivyo kwa wiki nzima. Mzee Jumanne hakuwa akijua kilichokuwa kikiendelea, alichoamini ni kwamba Bruno alikuwa amekimbia baada ya kumkosakosa kumkata kwa panga kama alivyokuwa amepanga.
Wakati akijipa uhakika kwamba mwanaume huyo alikuwa amekimbia akapata maneno kwamba Bruno alikuwa akiendelea na shughuli zake za uvuvi kama kawaida.
“Anafanyaje?” alimuuliza mvuvi mmoja aliyekuwa akiusimamia mitumbwi yake.
“Watu wanasema kwamba anaonekana sana tu akivua,” alisema kijana huyo na kuanza kumwambia jinsi Bruno alivyokuwa akiingia baharini.
Hilo lilitosha kabisa kumwambia kwamba Bruno aliendelea kuwepo kijijini hapo, alichokifanya ni kumtafuta James na kumwambia kwamba alitaka kufanya naye kazi moja kwa malipo makubwa ambayo asingeamini.
“Kazi gani?” aliuliza James.
“Umuue Bruno!”
“Nimuue Bruno?”
“Ndiyo!”
“Nitamuuaje?”
“Utamchukua kama unavyomchukuaga kwenda baharini, ukifika huko, mtupe baharini!” alisema mzee huyo.
“Mmh!”
“Unaogopa?”
“Hapana! Ila si ataweza kuogelea, sasa akifika nchi kavu itakuwaje?” aliuliza.
“Hakikisha siku ya tukio hauonani na huyo Abdul. Mnaondoka naye kwenda mbali kabisa, sehemu ambayo hata mkimtosa baharini, hawezi kupona,” alisema mzee huyo.
“Hakuna shida. Kwa hiyo vipi kuhusu mfuko?”
“Nawapeni elfu ishirini!”
“Sawa.”
Hilo halikuwa tatizo, akachukua shilingi elfu ishirini ya Kenya ambayo ilikuwa ni zaidi ya laki nne kwa shilingi ya Tanzania na kumpa.
“Basi sawa. Hiyo kazi inafanyika usiku wa leo. Hutoweza kumuona tena,” alisema James.
“Sawa. Nitashukuru sana!” alisema mzee Jumanne na kuondoka huku moyo wake ukiwa na furaha tele.
***
James alikuwa na furaha, hakuamini kama mzee Jumanne angetoa kiasi kikubwa cha pesa kwa kazi ndogo namna ile. Pesa alizopewa kwa upande wake zilikuwa nyingi mno kiasi cha kufanya utekelezaji haraka sana.
Huyo Bruno aliyeambiwa amuue wala hakuwa ndugu yake, urafiki wao ulikuwa wa juujuu tu. Hakuona kama kulikuwa na tatizo lolote lile, kwake, kazi hiyo ilikuwa ni ya kutekeleza haraka sana pasipo kujiuliza.
Akamwambia mwenzake aliyeitwa Kitula kwamba walitakiwa kufanya kazi ile huku pesa ile wangegawana. Maisha yao walijitahidi kufanya kazi kwa bidii mno, usiku na mchana kwa lengo la kupata pesa, leo huu, pesa ilikuja yenyewe na ni utekelezaji tu ndiyo uliokuwa ukitakiwa kufanyika.
Walichokifanya ni kukubaliana kuifanya kazi ile kwa usiku wa siku hiyo kwa kumchukua Bruno na kuondoka naye mpaka mbali kabisa ambapo huko wangemtosa ndani ya maji na wao kuendelea na kazi yao ya uvuvi.
Ilipofika jioni, kama kawaida wakamchukua Bruno na kuondoka naye. Hawakutaka kuonekana tofauti, walikuwa wacheshi vilevile, tabasamu yalitawala nyusoni mwao kiasi kwamba Bruno hakuona tatizo lolote lile wala kuhisi kwamba siku hiyo watu hao walitaka kumfanyia kitu kibaya.
Wakaondoka mpaka mbali kabisa. Siku hiyo hali ilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, kulikuwa na mawimbi mengi yaliyokuwa yakipiga hali iliyoonyesha kwamba bahari ingechafuka baada ya muda mchache. Waliendelea kupiga stori kama kawaida huku James na Kitula wakijifikiria ni kwa jinsi gani wangeweza kumtupa Bruno ndani ya maji na kuondoka zao.
Siku hiyo hawakutaka kwenda upande wa Mashariki kama ilivyokuwa siku nyingine, waliondoka na kwenda upande wa Kaskazini ambapo waliamini kwamba wasingeweza kukutana na Abdul.
Mtumbwi ulikwenda kwa umbali kama wa kilometa ishirini ndipo wakafika sehemu ambayo ilikuwa na kina kirefu mpaka zaidi ya mita elfu tatu. Waliona sehemu hiyo kuwa sahihi kwa kufanyia ule umafia waliotaka kufanya.
Mpaka kufika hapo tayari Bruno alionekana kuwa na hofu, akahisi kabisa kulikuwa na kitu kilichotaka kutokea. Walikuwa wamekwenda kwa umbali mrefu sana pasipo kukutana na Abdul. Haikuwa kawaida, alijua kabisa kwamba kwa umbali fulani hivi walikuwa wakikutana na Abdul na kuingia katika mtumbwi wake lakini kwa siku hiyo mambo yalionekana kuwa tofauti kabisa.
“Jamani! Huku tumekuja wapi?’ aliuliza Bruno huku akiwaangalia kwa uso uliokuwa na hofu nzito.
“Baharini! Abdul mbona haonekani leo?” alijibu James na kujiuliza, yeye mwenyewe akajifanya hajui.
Walizidi kwenda mbele kabisa, walipoona kwamba wamefika sehemu ambayo ni nzuri, hapohapo wakamgeukia Bruno na kuanza kumwangalia. Muonekano wao ulibadilika, hawakuwa kama wale ambao aliwazoea kipindi cha nyuma, walibadilika na kuwa watu wenye muonekano mwingine kabisa.
Hilo likamtia hofu Bruno na kuhisi kwamba kulikuwa na kitu kilichotaka kutokea. Hata kabla hajafanya kitu chochote kile, wakamsogelea, wakamshika kinguvu na kumtosa baharini.
Bruno alishangaa, hakujua sababu ya watu hao kufanya hivyo. Akabaki akielea ndani ya maji huku akiwaona James na Kitula wakiondoka mahali hapo na mtumbwi wao.
Aliwaita, aliwaomba msaada lakini hakukuwa na mtu aliyerudi, wote waliondoka na mtumbwi huku wakipiga kasia ya nguvu kuondoka mahali hapo.
Hilo lilimuuma, hakuamini kile kilichokuwa kikiendelea, hakuamini kama watu wale ambao kila siku alikuwa akiwaamini ndiyo waliokuwa wamemfanyia kitu kama kile.
Hakutaka kukata tamaa, ilikuwa ni usiku sana, bahari ilitisha, mawimbi makubwa yalikuwa yakipiga kwa nguvu. Alipiga kelele lakini hakukuwa na msaada wowote ule. Kutokana na giza zito lililokuwa mahali hapo ilikuwa vigumu kuona hata hatua saba kutoka pale alipokuwa.
Alijua kabisa kwamba siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wake, alipiga mbizi mpaka mikono ikachoka na kubaki akiwa amekata tamaa kabisa. Alitulia hapo, wakati mwingine alizama, akaibuka na kuendelea kuelea juu ya maji tu.
Muda ulizidi kwenda, kikafika kipindi bahari ikaanza kuchafuka, mawimbi makubwa yakaanza kupiga. Akapiga kelele lakini bado hakukuwa na mtu aliyetokea na kumpa msaada wowote ule. Alikuwa peke yake baharini, alipoangalia pande zote, hakukuwa na msaada wowote ule kitu kilichomfanya kuhisi kwamba siku hiyo ndiyo ungekuwa mwisho wake.
“Mungu nisaidie,” alisema huku akiwa amekata tamaa.
Alimuomba Mungu sana lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote yale. Mawimbi yalimpeleka huku na kule, alizamishwa na kuibuliwa, alikunywa maji mengi, alijitahidi kujiokoa lakini akashindwa kabisa mpaka kufikia hatua akajiweka tayari kwa kufa.
Alimkumbuka mpenzi wake, Sharifa, hakuamini kama huo ndiyo ungekuwa mwisho wa kumuona msichana huyo mrembo. Yaani kitendo cha kuchukuliwa na kuelekea baharini kilimaanisha kwamba huo ndiyo ulikuwa mwisho wake.
“Sharifa mpenzi! Ninakufa pasipo kukuona. Bebi! Ninakufa,” alisema Bruno kwa uchungu mkubwa.
Mawimbi yaliendelea kupiga, alikosa nguvu na baada ya dakika kadhaa, akaanza kuzama, alijitahidi kuibuka juu lakini ilishindikana kabisa, baada ya dakika tatu, mwili ukaishiwa nguvu, macho yakaanza kuwa mazito na hatimaye yakaanza kufumba, alijitahidi kujitingisha ili kuona kama alikuwa hai, akashindwa kabisa. Giza likaendelea kujaa machoni mwake na hakujua ni kitu gani kiliendelea baada ya hapo.
***
Abdul alikuwa ndani ya mtumbwi wake, macho yake hayakutulia, yalikuwa yakiangalia huku na kule ili kuona kama mtumbwi wa akina James ungefika mahali hapo au la.
Mitumbwi mingi ilikuwa ikipita mahali hapo, aliitolea macho kuona kama ilikuwa ni mtumbwi wa akina James lakini haikuwa huo. Moyo wake ulikuwa na hofu tele, kwa jinsi bahari ile ilivyokuwa imechafuka ilionyesha kabisa kwamba hali haikuwa nzuri hata mara moja.
Hakwenda kuvua, alikuwa akisubiri, dakika zilizidi kwenda mbele kama kawaida huku akiendelea kuwasubiri watu hao lakini hakukuwa na mtu yeyote ambaye alitokea mahali hapo.
Alihisi kwamba kulikuwa na tatizo, akajua kulikuwa na mchezo uliokuwa umefanyika ambao uliwafanya watu hao kuchelewa namna hiyo. Hakukata tamaa, aliendelea kusubiri mpaka ulipofika usiku mkubwa ambapo akaamua kuondoka zake huku akiwa na maswali mengi juu ya nini kilichokuwa kimetokea.
Asubuhi ilipofika, alirudi kijijini kama kawaida. Alitaka kuonana na akina James, alitaka kujua ni kitu gani kilikuwa kimetokea mpaka watu hao kutokukutana nao usiku uliopita.
Wakati akiwa ameweka mtumbwi wake pembezoni mwa bahari na kuufunga, kwa mbali akauona mtumbwi wa akina James ukija kule alipokuwa. Haraka sana akawafuata huku akiwa na shauku ya kutaka kufahamu ni kitu gani kilitokea.
Alipowafikia tu na kuuwaangalia usoni, akabaini kwamba kulikuwa na tatizo lililokuwa limetokea kwani nyuso zao zilionekana kuwa tofauti na siku nyingine, zilikuwa ni sura zenye majonzi tele.
“Msiniambie kama kuna jambo baya limetokea,” alisema hata kabla ya salamu.
Wanaume hao hawakujibu, walibaki wakimwangalia tu huku kila mmoja akiwa kimya. Ukimya wao ukazidi kudhihirisha kwamba kulikuwa na jambo baya lililokuwa limetokea. Akawauliza kwa mara ya pili ambapo James akaanza kumwambia kwamba Bruno alikufa baharini.
“Alikufa baharini?” aliuliza Abdul kwa mshtuko.
“Ndiyo! Bahari ilichafuka, si uliona?”
“Ndiyo!”
“Mtumbwi ukapelekwa huku na kule na hatimaye ukapinduka. Tulijaribu kuogelea, tukaupindua na kuuweka sawa. Yeye alishindwa kuungana nasi, akapelekwa na maji, tulimuita lakini hakutumuona te...” alisema James hata kabla hajamaliza sentensi yake, akanyamza, machozi ya kinafiki yakaanza kujikusanya na kutiririka mashavuni mwake.
Abdul hakuamini alichokuwa amekisikia, moyo wake ulikuwa kwenye maumivu makali mno, aliwaangalia akina James, maneno aliyokuwa akiambiwa yalionekana kama si katika ulimwengu halisi uliokuwa ukitokea, alihisi kwamba yupo ndotoni ambapo baada ya dakika kadhaa angeamka na kujikuta akiwa kitandani.
Hakujua ni kwa jinsi gani alitakiwa kumwambia Sharifa. Msichana huyo alikuwa akimpenda Bruno kupita kawaida, kitendo cha kumfuata na kumwambia kwamba mpenzi wake, Bruno alikufa baharini aliona kabisa angesababisha maumivu makali moyoni mwa msichana huyo.
Hakutaka kabisa kumfuata na kumwambia ukweli lakini baada ya kujifikiria sana, hakuwa na jinsi, alichokifanya ni kumtafuta Sharifa na kumwambia juu ya kile kilichotokea.
Hakumwambia moja kwa moja kwamba alikufa baharini, alimwambia kama alivyoambiwa kwamba bahari ilichafuka, alitumbukia ndani ya maji na kupotelea huko kitu kilichomaanisha kwamba mwanaume huyo alikufa humo baharini.
“Brunoooo...” Sharifa alijikuta akiita, akaufumba mdomo wake kwa viganja vyake na kuanza kulia kwa maumivu makali.
Hakukuwa na kitu kilichotokea kumuumiza kama kitu hicho, kifo cha mpenzi wake kilikuwa na maumivu makali hata zaidi ya ambavyo wangekufa wazazi wake wote wawili. Alilia kwa sauti kiasi kwamba mpaka watu wengine wakabaki wakishangaa.
Akaelekea chumbani kwake, hakunyamaza, aliendelea kulia mfululizo mpaka mafua yakampata. Alisikia kitu chenya ncha kali kikiuchoma moyo wake, maumivu aliyokuwa akiyasikia kipindi hicho hayakusimulika hata kidogo.
Wakati Sharifa akiwa analia, upande wa pili baba yake baada ya kupewa taarifa kwamba Bruno alikuwa amekufa baharini moyo wake ukawa na furaha, hakuamini alichokisikia, alitabasamu na kumpongeza James kwa kazi nzuri aliyokuwa ameifanya.
“Amekufa kweli?” aliuliza.
“Ndiyo! Usiku bahari ilichafuka sana, mawimbi makubwa, yaani sikuwahi kuona hali kama ile tangu nizaliwe. Kwenye mawimbi hayohayo, mbali kabisa na bahari, tukamtosa majini, ataponaje hapo,” alisema James na wote kuangua kicheko.
Kwao ilikuwa ni furaha tele, hakukuwa na mtu aliyehuzunika, mioyo yao ilikuwa na furaha kwamba hatimaye walikuwa wamefanikiwa kummaliza mwanaume huyo aliyeonekana kuwa mwiba mkali moyoni mwa mzee Jumanne.
Hicho ndicho kilikuwa kipindi kibaya kwa Sharifa, kila siku alikuwa mtu wa kulia tu, moyo wake ulichoma, kila siku asubuhi alipokuwa akiamka alikwenda mpaka ufukweni na kusimama karibu kabisa na bahari na kuanza kuyaangalia maji.
Hakuamini kama bahari hiyo ndiyo iliyommeza mpenzi wake aliyempenda kwa mapenzi ya dhati. Kifo cha Bruno kilisikika kila kona, kila mtu alimuonea huruma msichana huyo kwani mapenzi aliyokuwanayo moyoni mwake yalikuwa makubwa mno.
Wengi hawakutaka kukutana naye kwani kwa jinsi alivyokuwa na huzuni, kila aliyekutana naye alikuwa akilia, Sharifa alisikitisha kupita kawaida.
Wiki ya kwanza ikakatika, ya pili, ya tatu mpaka mwezi. Bado mwili wa Bruno haukupatikana. Alichokifanya Sharifa ni kwenda kuchimba kaburi kisha kuzizika nguo za mpenzi wake, Bruno kama ishara ya kumzika mwanaume huyo.
“Nitakupenda maisha yangu yote hata kama umekufa. Siwezi kuolewa, siwezi kuwa na mwanaume mwingine tena,” alisema Sharifa huku akiwa kwenye kaburi hilo la mpenzi wake ambapo ndani yake kulikuwa na nguo tu.
***
Biashara ya madawa ya kulevya iliyokuwa imeshamiri duniani kote ilianza kuyumba. Kila mtu aliyekuwa akiifanya biashara hiyo alishangaa, mizigo mingi ilikuwa ikikamatwa, watu waliokuwa wakisafirisha ambao walijulikana zaidi kama punda walikamatwa na kufungwa gerezani huku wakipewa mateso makubwa.
Marekani iliamua kuingia kazini, haikutaka kuona biashara hiyo ikiendelea kufanyika kwa kuwa watu waliokuwa wakiathiriwa zaidi walikuwa vijana ambao ndiyo walikuwa nguvu kazi ya taifa.
Iliingia kazini rasmi, wasafirishaji waliokuwa wakipitia mipakani walikuwa wakikamatwa, Wamexico ambao kazi yao kubwa ilikuwa ni kusafirisha madawa na kuingiza nchini humo walikamatwa na kufungwa gerezani tena huku wakipewa mateso makali.
Hali ilitisha, biashara iliyumba kupita kawaida. Wamarekani walichukiwa kwa kuwa walijifanya kimbelembele kuhakikisha kwamba wanazilaghai serikali za nchi nyingine kuhakikisha biashara hiyo inapotea haraka sana vinginevyo nchi ambayo ingepuuzia ingetolewa katika Umoja wa Mataifa.
Hilo ndilo lililozifanya nchi nyingine kuwa makini na kutumia nguvu kubwa katika kuhakikisha wanatokomeza biashara hiyo iliyokuwa ikiwatesa sana vijana waliokuwa wakitumia. Ndani ya miezi sita tu, biashara ililala kwa kiasi kikubwa sana kiasi kwamba kila mmoja akahisi kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wa biashara hiyo haramu.
Miongoni mwa wafanyabiashara wakubwa waliokuwa wakifanya biashara hiyo walikuwa Samuel Maxwell aliyekuwa na umri wa miaka hamsini na mbili na Richard Todd aliyekuwa na miaka hamsini na nane.
Wawili hao walikuwa mabilionea wakubwa nchini Marekani, Todd alikuwa na utajiri wa dola bilioni ishirini na nne ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni arobaini na nane huku Maxwell akiwa na utajiri wa dola bilioni ishirini ambazo zilikuwa ni zaidi ya shilingi trilioni arobaini.
Japokuwa walikuwa na biashara nyingi zilizokuwa zikiwaingizia pesa lakini biashara kubwa zaidi ambayo iliwafanya utajiri wao kukua kila siku ni biashara ya madawa ya kulevya waliyokuwa wakiifanya.
Waliuziana madawa, walifanya biashara kama ndugu, walipendana kiasi kwamba mpaka mabilionea wengine wakashangaa kwani hawakuwahi kuwaona mabilionea ambao walikuwa wakishirikiana vizuri katika biashara zao kama wawili hao.
Wakati Marekani ilipoanza kuleta figisufigisu katika biashara hiyo ndipo wawili hao wakatokea kugombana na kuonana kama paka na panya na chanzo kikubwa kikiwa ni biashara hiyohiyo ya madawa ya kulevya.
Wakati watu wakihitaji sana madawa hayo na Todd kujiona kwamba hana kitu, haraka sana akawasiliana na Maxwell na kumwambia kuhusu mkakati wake ambao angeufanya kuhakikisha anapata mzigo na kuupeleka barani Afrika ambapo kulikuwa na uhitaji mkubwa wa madawa hayo.
Maxwell hakuona kama kulikuwa na tatizo, alimwamini Todd, walikuwa wakifanya biashara hiyo kwa miaka mingi. Akampa mzigo wa dola bilioni mbili kwa lengo la kuupeleka Afrika na kufanya biashara hiyo na kumpelekea pesa zake.
Todd akachukua mzigo na kwenda nao Afrika. Hakutaka kumwamini mtu yeyote, alitaka kuusafirisha yeye kama yeye na kuufikisha nchini Msumbiji salama kabisa. Akawasambazia watu wake na kuondoka zake.
Alitegemea kupata pesa zake baada ya wiki mbili ambapo biashara hiyo ingekuwa imefanyika kikamilifu lakini kitu cha kushangaza kabisa, mpaka wiki mbili zinakatika bado hakuwa amepata pesa hizo alizoambiwa kwamba angepata.
Kuwaamini watu wengine kukamgharimu, alikuwa akiwasiliana nao kwenye simu lakini bado watu hao hawakuwa wakipokea, hilo lilimchosha sana, lilimfanya kufadhaika kwa kuwa mzigo ule haukuwa wake, alikopeshwa na kuahidi kulipa pesa hizo mara baada ya biashara kufanyika.
Waafrika wakamuingiza choo cha kike, hawakumlipa pesa zake. Kila siku Maxwell alikuwa akimpigia simu na kumwambia kuhusu pesa zake, hakujua ni kitu gani alitakiwa kumwambia kwani kama angemwambia ukweli kuwa hakuwa amelipwa, angeonekana tapeli na muongo mkubwa.
Baada ya kukatika mwezi, Maxwell akachoka kufuatilia, japokuwa walikuwa marafiki lakini kwenye ishu ya pesa akaamua kuuweka urafiki pembeni na kuanza kumdai kibabe.
Hilo halikumshangaza Todd, alijua dhahiri kwamba kuna siku kitu kama hicho kingetokea, alichomwambia ni kuendelea kusubiri kwani bado aliendelea kuwakumbusha watu hao kuhusu pesa zake.
Akili yake ikavurugika, miezi miwili bila kulipwa kukamfanya kupaniki na hivyo kupanga kusafiri mpaka nchini Msumbiji kwa lengo la kwenda kuwaambia watu wake wamlipe.
Wakati yeye akipanga kusafiri kwenda huko, Maxwell hakutaka kumuacha, aliona kabisa kwamba alikuwa akienda kutapeliwa. Hakuangalia tena urafiki, hakuangalia ni kwa kipindi gani walikuwa pamoja, alichokifanya ni kutuma watu kwenda kumteka, wamtese sana na awahamishie kiasi cha pesa alichokuwa akidaiwa katika akaunti yake.
Vijana wakaondoka mpaka nchini Msumbiji. Walipofika, wakamwambia Todd kwamba aandae meli ambayo hapo ingewachukua mpaka Nigeria ambapo huko ndipo walipopanga kufanya mauaji hayo.
Hilo halikuwa tatizo kwani kabla ya wao kwenda huko, tayari meli yake ya mizigo ilikuwa imeandaliwa kwa kufanya kazi hiyo na kipindi hicho ilikuwa ikitoka Afrika Kusini. Ilipofika, wakaambiwa kwamba imefika na hivyo kilichotakiwa kufanywa ni utendaji kazi kuhakikisha kwamba wanampata mwanaume huyo.
“Mtafuteni mtu anayeitwa Robson Mautinho, huyo ndiye mtu aliyepewa mzigo huo, hakikisheni mwanaume huyo anapatikana,” ilisikika sauti ya Maxwell kwenye simu.
Hilo ndilo lililofanyika, kumpata mwanaume huyo halikuwa jambo gumu kwa kuwa alijulikana kutokana na utajiri wake mkubwa. Walipoonana naye, hawakutaka kumficha, walimwambia kuhusu mpango wao wa kummaliza mwanaume huyo.
Kwa Mautinho ilikuwa habari njema kwake, alikuwa akidaiwa pesa nyingi na hakuwa na mpango wa kuumlipa mzee Todd hivyo alivyoambiwa kwamba watu hao walikuwa na mpango wa kumteka, kwake ilikuwa ni furaha tele kwani kama wangemuua ilimaanisha kuwa asingesumbuliwa tena na mwanaume huyo.
“Hakuna tatizo. Ameniambia kwamba kesho atakuja tuzungumze,” alisema Mautinho.
“Basi sawa. Waambie vijana wako wamteke, wamfunge sehemu na tutakuja kumchukua mtu wetu,” alisema kijana mmoja aliyeitwa Phillip.
“Sawa.”
Hilo ndilo lililofanyika, siku iliyofuata, wakati mzee Todd amefika mahali hapo, akaanza kuzungumza na Mautinho na baada ya kumaliza mazungumzo, akajikuta akizungukwa na vijana wa mwanaume huyo, cha kwanza kilikuwa ni kuwaua walinzi wake aliokwenda naye na yeye kufunikwa uso wake na kitambaa kilichokuwa na umbo la kikapu.
Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alijaribu kuuliza lakini mwanaume huyo hakumwambia kitu chochote kile. Akaamrisha apelekwe kwenye chumba kimoja cha giza na kuhifadhiwa humo.
Alichanganyikiwa, alijiona kugeukiwa, akilini mwake hakuhisi kabisa kama Maxwell ndiye aliyefanya hivyo, alichoamini ni kwamba Mautinho ndiye aliyeamua kuucheza mchezo ule ili amtapeli pesa zake alizokuwa akimdai.
Usiku mzima alikuwa akilia tu, moyo wake ulimuuma mno, akahisi kabisa kwamba watu hao walikuwa wakitaka kumuua. Kufa kwake halikuwa tatizo, ila tatizo lilikuwa ni kuiga familia yake tu.
Alikuwa na mke aliyeitwa Juddie na mtoto wake wa kike aliyeitwa Martha. Kwake, kufa pasipo kuiaga familia yake alihisi ni maumivu mazito mno.
Katika chumba alichokuwa amewekwa, hakikuonekana kuwa kizuri hata kidogo. Kilikuwa kichafu kilichokuwa na harufu ya damu. Hakupigwa, hakufanywa lolote lile lakini kukaa ndani ya chumba kile kulimfanya kuhisi mateso makubwa kupita kawaida.
Ilipofika usiku, mlango ukafunguliwa na wanaume wawili kuingia, wakamchukua huku wakiwa wamemfunga kitambaa machoni na kuondoka naye. Hakujua alipokuwa akipelekwa ila alijua kwamba hakukuwa sehemu nzuri na kwa katika kipindi hicho ilikuwa ni lazima kuuawa.
Aliingizwa ndani ya gari na kuondoka mahali hapo. Baada ya dakika kadhaa, akashushwa na kupelekwa sehemu huku akiwa ameshikwa na watu wawili kushoto na kulia.
Akapelekwa sehemu iliyokuwa na ngazi na kuanza kupandishwa. Mlango ukafunguliwa na kuingizwa ndani ya chumba kimoja na kuwekwa humo.
Hapo, kwa mbali alisikia kelele za watu wakicheka huku wengine wakigongesheana glasi, kwa jinsi vicheko vilivyokuuwa vikisikika ilionyesha kabisa kwamba walikuwa kwenye maisha ya raha kupita kawaida.
Baada ya dakika kadhaa, honi ikaanza kupigwa, haikuwa ya gari wala treni, aliposikia vizuri ilikuwa ni honi ya meli, hapo akagundua kwamba alikuwa ndani ya meli ambayo hakujua ilikuwa ikielekea wapi, ndani ya dakika chache akaisikia ikianza kuondoka mahali hapo.
Alichokifanya ni kutoa kitambaa kile usoni mwake. Chumba kilikuwa na mwanga hafifu, alibaki akiangalia huku na kule, hakujua mlango ulikuwa mahali gani. Akasimama na kuanza kuzunguka huku na kule, bahati nzuri kwake akagusa kitu ambacho alijua kabisa kilikuwa ni kama kitasa cha kufungua mlango wa kutokea ndani ya chumba hicho.
Humo ndipo alipotakiwa kukaa mpaka atakapofikishwa mbali kabisa, Nigeria ambapo alitakiwa kuuawa. Hakujua mahali alipokuwa, na wala hakujua mahali ambapo meli hiyo ilipokuwa ikielekea.
“Mungu naomba uniokoe! Naomba uniokoe Mungu,” alisema mzee Todd ndani ya chumba kile. Moyo wake uliogopa na muda wowote ule alihisi kwamba angeuawa na watu waliokuwa wamemchukua.
***
Maisha ya Sharifa yalibadilika na kuwa kama mtu aliyekumbwa na msiba mzito. Hakuwa na furaha, maisha yake aliyaona kuwa na giza kubwa mbele yake, moyo wake uliuma na kuuma, alilia usiku na mchana lakini machozi yake hayakuweza kumrudisha Bruno katika upeo wa macho yake.
Kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye kaburi la mpenzi wake na kukaa huko, alikuwa mtu wa kulia huku muda mwingi akimlaumu baba yake kwamba ndiye aliyesababisha hayo yote.
Bruno kutokuwa na pesa, kikabadilisha kila kitu, maisha yake yakaonekana kuwa si lolote na hata yule mpenzi aliyekuwa akimpenda aliambiwa aachane naye.
Yote aliyokuwa akiyakumbuka yaliuumiza moyo wake, Sharifa aliumia kupita kawaida. Wakati mwingine alimuuliza Mungu kwamba kwa nini alizaliwa na baba yake, alitamani hata angezaliwa na mtu mwingine ambaye angemsapoti katika uhusiano wake na Bruno.
Hakutaka kula, alikuwa kwenye maombolezo mazito. Mzee Jumanne hakujali, alichokuwa akikiangalia ni kuona mtoto wake akiachana na Bruno ambaye tayari muda huo alihesabika kama marehemu.
Siku zikakatika, baada ya miezi mitatu, nyumbani kwa mzee Jumanne kukatokea ugeni kutoka jijini Nairobi, ugeni wa mzee Mohammed Olioh na ulifika hapo kwa kuwa walitaka kuzungumza mambo mengi kuhusu watoto wao.
Mzee Olioh alikuwa mtu mwenye pesa zake jijini Nairobi. Alimiliki mabasi kadhaa yaliyokuwa yakifanya safari zake kwenda Tanzania, Uganda na mengine kwenda mpaka Rwanda. Alikuwa na pesa nyingi, aliheshimika kupita kawaida.
Maishani mwake alibahatika kupata mtoto mmoja tu, aliyeitwa Rahman ambaye kipindi hicho alikuwa nchini Marekani akisomea sheria katika Chuo cha Kikuu cha Mississippi.
Kipindi hicho Rahman alikuwa akijiandaa kurudi kutoka chuoni na kitu kimoja alichohitaji ni kutafutiwa mwanamke wa kuishi naye. Mtu ambaye alikuja kichwani mwa mzee Olioh ni msichana Sharifa aliyekuwa akiishi katika Kijiji cha Guolduvai kilichokuwa pembeni mwa bahari ya Hindi.
Alimfahamu msichana huyo, alikuwa mrembo na baba yake alikuwa na heshima kubwa huko alipokuwa akiishi. Alichokifanya ni kuondoka na kuelekea huko. Alipofika, akaonana naye na kuanza kuzungumza naye.
Alimwambia ukweli kuhusu mtoto wake aliyekuwa akitarajiwa kurudi nchini Kenya. Mzee Jumanne alipoambiwa hivyo, alishtuka, hakuamini kama mzee huyo angemfuata na kumwambia kitu kama hicho.
Kumshawishi mtoto wake halikuwa tatizo, aliamini kwamba angekubaliana naye kwa sababu mtu aliyekuwa akimpenda, Bruno wakati huo alikuwa marehemu. Akamwambia mzee Olioh kwamba hakutakiwa kuhofia kitu chochote kwani yeye kama mzazi angezungumza na Sharifa na bila shaka msichana huyo angekubaliana naye.
 
Bruno The Fish Man

Mtunzi.Nyemo Chilongo

Epsode 2


Mzee Olioh akaondoka kurudi jijini Nairobi huku akiwa na mategemeo mengi kwamba Sharifa angekubali na hivyo kuolewa na kijana wake.
Huku nyuma, mzee Jumanne alikuwa na kazi kubwa ya kuzungumza na binti yake. Alijua kabisa kwamba alikuwa kwenye maumivu makali lakini hakutaka kuona akimkataa Rahman, ilikuwa ni lazima akubali kwa kuwa alitoka katika familia iliyokuwa na pesa.
Sharifa alipoambiwa, akashtuka, hakuamini kama baba yake alifikia hatua ya kumtafutia mwanaume wa kumuoa. Hilo lilimuumiza mno moyoni mwake na bila kificho alimwambia baba yake kwamba hawezi kuolewa na mwanaume huyo.
“Ila ana pesa! Anasoma Marekani!” alisema mzee Jumanne.
“Siwezi kuolewa. Siwezi kuolewa na mwanaume yeyote baba,” alisema Sharifa huku akimwangalia baba yake.
“Huoni kama umri unakwenda tu binti yangu?”
“Kama unaona umri unakwenda, ungemkubali Bruno anioe, umeona amekufa ndiyo unakuja na kuniambia kwamba umri unakwenda. Kwa taarifa yako siolewi,” alisema Sharifa huku akimwangalia baba yake.
Huo haukuwa muda wa kuogopa tena, alimwambia baba yake wazi kwamba hakutaka kuolewa na mwanaume huyo. Mzee Jumanne hakusema kitu, akakubaliana na mtoto wake na kuondoka.
Alikwenda mpaka chumbani kwake, alivimba kwa hasira, hakuamini kama Sharifa angekataa kufanya kile alichotaka akifanye. Yeye ndiye alikuwa mzazi, sasa kwa nini amkatalie kuolewa na mwanaume aliyekuwa akimtaka?
“Nitatumia mabavu kama mzazi! Si anakataa kwa hiari, sasa ataolewa kwa lazima,” alisema mzee Jumanne,.
Alichokifanya ni kumpigia simu mzee Olioh na kumwambia kwamba kila kitu kilikuwa tayari, alizungumza na binti yake na kukubaliana naye na hivyo walitakiwa kupanga tarehe ya kufunga ndoa kijijini hapo.
Haraka sana mzee huyo alipoambiwa hivyo, akampigia simu kijana wake nchini Marekani na kumwambia kile kilichojiri kwamba msichana waliyekuwa wamemchagulia alikubali kuolewa naye na hivyo alitakiwa kurudi Kenya haraka sana mara baada ya kumaliza mitihani.
“Amekubali?” aliuliza.
“Ndiyo! Haikuwa kazi kubwa.”
“Ila ni binti mzuri?”
“Niamini! Siwezi kumchagulia kijana wangu binti mbaya! Ni mzuri kama mama yako alivyokuwa kijana,” alisema mzee Jumanne na kuanza kucheka.
“Sawa. Nilindieni mke wangu! Nikija tu ni ndoa na kuendelea kufanya mambo yangu,” alisikika Rahman.
“Sawa. Hakuna shida.”
***
Safari baharini ilikuwa ikiendelea, mabaharia walikuwa wamelala kwa kuwa usiku mzima walikuwa wamekunywa pombe kali. Ndani ya meli hiyo iliyokuwa na watu kumi na sita ni watu wawili tu ndiyo ambao hawakuwa wamelala, nahodha, mzee Sam Maskovich na mzee Todd aliyekuwa katika chumba alichohifadhiwa.
Meli iliendelea kukata mawimbi, hapo walipokuwa, hakukuwa na nchi kavu yoyote iliyokuwa ikionekana. Meli ilikuwa katikati ya bahari ikiendelea na safari yake.
Macho ya Maskovich yalikuwa mbele kabisa, alikuwa akiangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea. Alichoka mno lakini hakuwa tayari kulala, yeye ndiye alikuwa kila kitu katika safari hiyo.
Wakati akiendesha meli hiyo, pembeni kulikuwa na chupa ya pombe ambayo ndiyo ilikuwa ikimuweka sawa kila alipokuwa akisikia usingizi. Muda ulizidi kwenda mbele mpaka pale alipokiona kitu kikiendelea juu ya maji.
Hakujua ni kitu gani, haraka sana akachukua darubini na kuanza kuangalia kwa karibu, alichokiona ni mwanaume akiwa anaelea juu ya maji. Alishtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kimeendelea mpaka mwanaume huyo kuwa hapo.
Alichokifanya ni kuwaamsha wenzake na kuwaambia kile kiliichokuwa kikiendelea. Wote wakaamka na kuangalia mbele, kweli walimuona mwanaume akiwa anaelea juu ya maji.
“Chukueni boya,” alisema mzee Maskovich.
Boya moja la duara lililofungwa kamba ngumu likachukuliwa na kutupwa baharini, mwanaume mmoja naye akajitosa baharini na kuanza kumfuata mtu huyo kule alipokuuwa.
Alipomfikia, akamshika na kuwaambia wenzake wavute boya kitu ambacho kilifanyika kwa haraka sana. Mtu aliyekuwa kwenye maji akaokolewa na kuwekwa ndani ya meli, alikuwa Bruno ambaye hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mahali hapo.
Tumbo lake lilikuwa kubwa, alikunywa maji mengi, ngozi yake ilikuwa laini sana huku ikiwa inateleza kutokana na muda mwingi kuwa ndani ya maji.
Huduma ya kwanza kabisa waliyompa ni kumlaza kifudifudi na kuanza kuukandamiza mgongo wake kwa lengo la kuyatoa maji aliyokuwa amekunywa. Hiyo ilisaidia kwani baada ya kukandamizwa mara kadhaa, maji yakaanza kutoka, walipohakikisha kwamba wamemaliza, wakamchukua na kumpeleka kitandani kupumzika.
Kila mmoja alikuwa na maswali mengi, walijiuliza kuhusu mwanaume huyo, alikuwa nani na alikuwa akifanya nini mpaka kuwa baharini hapo. Wengi wakahisi kwamba inawezekana alikuwa kwenye meli na wenzake na meli kuzama.
Wakaangalia mahali pale ili kuona kama wangeweza kuwaona watu wengine lakini hawakufanikiwa. Walipomaliza kumpa huduma ya kwanza, wakamchukua na kumpeleka katika chumba alichokuwemo mzee Todd na kumuacha humo.
Mzee huyo alishtuka, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alimwangalia kijana aliyekuwa ameletwa, hakuwa na fahamu, alionekana kuwa kwenye hali mbaya kwani hata kwa jinsi ngozi yake ilivyokuwa, ilionyesha alikuwa kwenye mateso makali ya kupigwa baridi.
Akamsogelea pale chini alipokuwa na kuyasikiliza mapigo ya moyo wake, yalikuwa yakidunda kwa mbali sana hali iliyomfanya kugundua kwamba mwanaume huyo alikuwa hai.
“Kwa nini wamemleta humu? Naye ni mateka au?’ alijiuliza mzee huyo huku akimwangalia Bruno aliyekuwa hapo chini.
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, hakurudiwa na fahamu japokuwa alionekana kuwa hai. Vijana wa meli hiyo walikuwa wakiingia mara kwa mara ndani na kumwangalia kama alikuwa ameamka au la. Kila walipoingia, bado Bruno alionekana kuwa vilevile kama alivyokuwa kipindi cha nyuma.
Walimuokoa kutoka baharini lakini baada ya kuona kwamba amechukua muda mrefu pasipo kurudiwa na fahamu, wakajadiliana ni kitu gani wafanye, wakakubaliana kwamba wamtupe baharini kwani tayari alionekana kuwa mzigo.
“Tumtupe? Hakuna! Siwezi kukubaliana na kitu hicho,” alisema mzee Maskovich huku akiwaangalia watu hao.
“Lakini amekufa!”
“Bado mapigo yake ya moyo yanadunda.”
“Lakini haamki! Inawezekana ndiyo hatua zake za mwisho kuishi ndani ya dunia hii,” alisema mwingine.
“Hata kama. Tusubiri, kama kweli yeye ni wa kufa, atakufa na sisi kumtupa. Tumemuokoa, hebu tufanyeni lolote kuionyesha dunia kwamba tuna upendo wa ajabu,” alisema nahodha huyo maneno ambayo yaliingia kichwani mwa kila mtu.
Siku nyingine ilipoingia ndipo Bruno akarudiwa na fahamu, akaanza kuwa kuyafumbua macho yake na kuangalia huku na kule. Alishangaa, alikumbuka kwamba mara ya mwisho alikuwa ndani ya bahari huku mawimbi yakimpeleka huku na kule na hatimaye kuzama, ila kilichotokea baada ya hapo, hakukijua.
”Nipo wapi?” lilikuwa swali la kwanza kabisa alilouliza mara baada ya kufumua macho na kumuona mwanaume mmoja akiwa amekaa pembeni yake.
“Who the hell are you?” (wewe ni nani?) aliuliza mzee Todd. Aliposikia hivyo tu akajua kwamba mtu huyo alikuwa Mzungu, hivyo naye alitakiwa kuongea Kiingereza japokuwa kwa elimu yake ya kidato cha nne hakuwa akiifahamu vizuri.
“Bruno!” alijibu huku akijitahidi kujinyanyua kutoka pale alipokuwa.
“Bruno?”
“Help me! I’m hungry...give me food, pleaseee...” (nisaidie! Nina njaa, naomba chakula tafadhali) alisema Bruno.
“Want some food huh?” (unataka chakula huh?)
“Yeah! Help me! Hunger is killing me,” (ndiyo! Nisaidie! Njaa inaniua) alisema Bruno huku akimwangalia mzee huyo kwa jicho lililokuwa la huruma kupita kawaida.
Alichokifanya mzee huyo ni kusimama na kisha kuanza kupiga mlango kwa nguvu huku akiita kwa sauti. Hiyo ilisaidia, baada ya sekunde chache, mlango ukafunguliwa na kijana mmoja ambaye baada ya kuingia tu akamwambia kwamba kijana yule alizinduka na alikuwa na njaa kali.
“Nakuja!”
Kijana yule akaondoka, kule alipokwenda, akawaambia wenzake, vijana wanne wakaelekea kule huku wakiwa na chakula, walipofika, wakampa na Bruno kuanza kula kwa pupa kwani alihisi kama asingekula ndiyo ungekuwa mwisho wake.
“Want some more?” (unataka kingine?)
“Yeah!”
Akaletewa, alikula na kula, baadaye akapelekewa soda na kunywa. Kidogo tumbo lake likapata nafuu na nguvu kuanza kurudi upya. Aliwaangalia vijana waliokuwa wamesimama mbele yake, hakujua ni wakina nani na hakujua ni kitu gani kilitokea.
Vijana hao wakamnyanyua na kuondoka naye mpaka kwa wenzao, wakamuweka kati na kuanza kumuuliza sababu ya kuwa baharini. Hakutaka kuficha, alisimulia kila kitu, historia yake iliwakera watu wote kwa sababu kuchukiwa kwa mtu kisa umasikini kilikuwa kitu kibaya sana.
“Pole sana! Kwa hiyo huna pa kwenda?”
“Sina! Kama mtaweza, naomba mnirudishe!” alisema Bruno.
***
Kila mmoja alibaki akimshangaa Bruno, hawakuamini kama kungekuwa na mtu aliyekuwa radhi kumuua mtu mwingine kwa kumtosa baharini tu kwa kuwa upande wa pili kulikuwa na mzazi ambaye hakutaka binti yake aolewe na mwanaume huyo.
Kila mmoja akahisi kwamba alikuwa akidanganywa, kitu walichohisi ni kwamba Bruno alikuwa mmoja wa waharamia waliokuwa wakiteka meli baharini kwa kushirikiana na makundi ya Kisomali.
Walikwishawahi kukutana na watu wa namna hiyo, walikuwa wana roho mbaya, walitoa roho za watu pasipo kujali kama walikuwa watu wema, wachungaji au mashehe. Walimwangalia Bruno, kwa jinsi mikono yake ilivyojazia kutokana na kupiga sana kasia, wakahisi kabisa kwamba huyo alikuwa mmoja wa watu hao.
Wakaanza kuongea pembeni kwamba ilikuwa ni lazima Bruno auawe kwani waligundua kwamba kile alichokuwa akikizungumza hakikuwa na ukweli wowote ule, aliwadanganya kwa kuwa tu alihitaji msaada kutoka kwao.
Wakamchukua na kumrudisha ndani ya kile chumba, alibaki humo akiwa kimya, hakuzungumza na mzee Todd aliyekuwa pembeni ambaye naye alikuwa akishangaa sababu ya kijana huyo kupelekwa katika chumba kile kilichoonekana kuwa na mateso makubwa.
“Why are you here?” (kwa nini upo hapa?) aliuliza mzee huyo huku akimwangalia Bruno.
“My friends tossed me,” (marafiki zangu walinitosa)
“Why did they do that?” (kwa nini walifanya hivyo?)
Bruno hakuficha, alimwambia mzee Todd kila kitu kilichotokea kwa kuamini kwamba kwa kusema ukweli vile basi angeweza kuonewa huruma. Kwa mzee huyo, hata naye jambo hilo halikumuingia hata kidogo, alibaki akimwangalia Bruno kwa macho yaliyoonyeshwa kutokuridhishwa na majibu yake kabisa.
“So, he sent people to toss you in the sea?” (kwa hiyo aliwatuma watu wakutose baharini?) aliendelea kudadisi mzee huyo.
“Yeah! I am a poor. I have nothing, her parents dinied me to marry her!” (ndiyo! Mimi ni masikini. Sina kitu, wazazi wake walikataa nimuoe) alisema Bruno.
Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa watu hao kuonana. Walizungumza mambo mengi huku mzee Todd akimwambia Bruno matatizo yote aliyokuwa akipitia na kwamba alikuwa njiani kuuawa na watu hao.
Moyo wake ulimuuma, hakuogopa kufa bali kitu alichokuwa akikiogopa ni kuiona familia yake, mkewe Juddie na mtoto wake, Martha wakipata maumivu makubwa moyoni mwake.
Muda ulizidi kwenda mbele, walikuwa ndani ya chumba kile, kila mmoja alifikiria kifo, walijua kabisa kwamba ilikuwa ni lazima wanaume wale wawamalize na kuondoka zake. Akili ya Bruno ilikuwa ikicheza kwa kasi, hakutaka kuona akifa, hakutaka kuona akipotea na mpenzi wake, Sharifa kujua kwamba alikufa, kama mwanaume, alitakiwa kupambana kuhakikisha kwamba anatoka salama ndani ya meli ile.
Akasimama na kuanza kuzunguka huku na kule, macho yake yaliangalia kila kona, alitaka kujua ni mahali gani ambapo wangepatumia ili kutoroka ndani ya meli ile. Mzee Todd alimwambia kwamba alitakiwa kuuawa. Alijua fika kwamba mauaji yangefanyika baada ya meli kuvuka Afrika Kusini ambapo ilikuwa ni lazima meli ikaguliwe sana.
Alimwambia hilo mzee huyo na kugundua kwamba kifo chake kingetokea baada ya kuvuka hapo Afrika Kusini katika bandari ya Cape Town ambayo hujulikana kama Table Bay ikiwa na maana ya Ghuba yenye mfanano wa meza.
“Tuna siku mbili mpaka kuingia Afrika Kusini. Na kutokana na muda huo itakuwa ni lazima tuwe tumekwishapata majibu kabla ya kuingia katika nchi hiyo!” alisema Bruno.
“Sawa. Ngoja nijifikirie!”
***
“Innocent! Where are you?” (Innocent! Upo wapi?)
“At home!” (nyumbani)
“Did you contact with him today?” (uliwasiliana naye leo?)
“Who?” (nani?)
“Mr. Todd.”
“No! Do you want me to contact him?” (Hapana! Unataka niwasiliane naye?)
“Yeah!”
Innocent ambaye alipigiwa simu na mke wa mzee Todd akachukua simu yake na kumpigia mzee huyo, simu haikuwa ikipatikana, hakuacha kumpigia zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale kwamba mzee huyo hakupatikana.
Haraka sana akampigia mtu aliyekuwa amempigia ambaye alikuwa ni mke wa mzee huyo, Juddie na kumwambia kwamba hakuwa akipatikana hivyo kumwambia kwamba waonane.
Mwanamke huyo alikuwa na hofu kubwa moyoni mwake, hiyo ilikuwa inakatika siku nzima mumewe hakuwa akipatikana katika simu. Hilo lilimfanya kuwa na hofu kubwa, alimpigia simu zaidi na zaidi lakini majibu yalikuwa yaleyale.
Hakuishia kumpigia kijana Innocent ambaye alikuwa mmoja wa vijana waliokuwa wakifanya kazi nyingi za mume wake, akawapigia wengine lakini nao hawakuwa wamewasiliana na mzee huyo na mbaya zaidi hata wale vijana aliokuwa amekwenda nao nchini Msumbiji hawakuwa wakipatikana.
Hapo ndipo taarifa zikatolewa polisi ambao waliwasiliana na polisi wa Msumbiji kwa kupitia kitengo cha Interpol ambapo taarifa za awali zilisema kwamba kweli mwanaume huyo aliingia nchini humo kwani hata ndege yake ilikutwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Maputo.
“Sasa atakuwa wapi?” lilikuwa swali alilouliza mkewe.
“Hata sisi hatufahamu chochote kile. Ngoja tufuatilie halafu tutakupa taarifa,” alisikika Innocent ambaye aliamua kusafiri mpaka Msumbiji kujua ukweli wa kile kilichokuwa kimetokea.
Ilikuwa ni lazima kujua mahali bwana Todd alipokuwa. Ndege yake ilikuwa katika uwanja wa ndege, je, yeye mwenyewe alikuwa wapi? Walichokifanya ni kumtafuta rubani wake, kumpata haikuwa shida kwani alipouliziwa tu, alipatikana katika hoteli moja ya kifahari.
Alipoulizwa kuhusu mzee huyo, hakufahamu kitu, aliwaambia kwamba alifika na mzee huyo mpaka nchini Msumbiji ambapo akamwambia akakae kwenye hoteli ile huku akilipia kila kitu.
“Kwa hiyo hata wewe hujui yupo wapi?”
“Sijui! Ndiyo kwanza mmeniambia nyie.”
Polisi nchini Msumbiji wakaanza kuhaha kumtafuta mzee huyo, kila kona walipokuwa wakiuliza, hakukuwa na mtu aliyekuwa akifahamu ukweli. Zawadi nono ikawekwa kwa mtu yeyote ambaye angefanikisha kupatikana kwa mwanaume huyo lakini napo haikusaidia.
Kikafika kipindi ambacho serikali ya Msumbiji ikahisi kwamba kundi la Boko Haram ndilo lililokuwa limemteka mzee huyo lakini katika hali ya haraka sana kiongozi wa kundi hilo akaibuka na kuzipinga taarifa hizo kwamba hawakumteka mzee huyo kwa kuwa hawakuona kama kuna ulazima wa kufanya jambo hilo.
Taarifa za kupotea kwake zikaanza kuvuma kwenye mitandao ya habari, watu wengi walikuwa na maswali mengi kwamba ni nani alihusika kumteka mzee huyo? Kama alikuwa nchini Msumbiji, mbona alitafutwa kila kona lakini hakuwa amepatikana?
Marekani haikubaki kimya, kupotea kwa mzee huyo iliwashangaza sana, walichokifanya ni kuwatuma maofisa wa CIA kuelekea nchini Msumbiji ambapo huko walitakiwa kufuatilia kila kitu na kugundua mzee huyo alikuwa wapi na ni kwa jinsi gani walitakiwa kumtafuta na kumpata.
Maofisa wanne wakasafiri na kuelekea nchini humo. Kitu cha kwanza kabisa kilikuwa ni kutafuta mawasiliano yake, walitaka kugundua ni watu gani alikuwa amewasiliana nao mara ya mwisho alipoingia nchini humo.
Namba yake wakaipata na kuona namba ya bilionea mmoja kutoka nchini Msumbiji, Moutinho ambaye mara ya mwisho aliwasiliana naye. Huyo ndiye mtu wa mwisho ambaye aliwasiliana na huyo mzee siku mbili zilizopita. Walichokifanya ni kumfuata kwa lengo la kuzungumza naye.
“Alikuja kwangu! Nilizungumza naye, hakuonekana kuwa sawa siku hiyo, alikuwa na hofu kubwa,” alisema Moutinho.
“Sawa. Baada ya kuondoka hukujua alipoelekea?”
“Sikujua kitu chochote kile.”
“Sawa. Haina shida.”
Hawakutaka kuzungumza naye zaidi, walichokifanya ni kuondoka huku wakiwa na uhakika kwamba bilionea huyo alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea. Walipofika hotelini, wakawasiliana na wenzao waliokuwa nchini Marekani na kuwaambia kuhusu bilionea huyo waliyezungumza naye kwamba alikuwa akifahamu kila kitu japokuwa alijifanya kutokujua lolote lile.
“Hakikisheni anawaambia ukweli. Ikiwezekana, mrudieni na kuzungumza naye kibabe,” alisikika kiongozi wao.
“Ondoa hofu. Tutakupa majibu kesho!”
“Sawa.”
***
Innocent hakutaka kukubali, mbele yake kulikuwa na kazi kubwa ambayo alitakiwa kupambana nayo mpaka kuhakikisha anashinda. Alitaka kuwasiliana na vijana wake kwa kuamini kwamba wangegundua mahali alipokuwa Bwana Todd kwa haraka tofauti na maofisa wa CIA walivyotaka iwe.
Watu wa kwanza kabisa kuwasiliana nao walikuwa ni vijana walioishi katika Jiji la Maputo nchini Msumbiji, wakawaambia kwamba kulikuwa na tukio la kupotea kwa bosi wao, vijana hao walikuwa wakifahamu kila kitu, walipata taarifa mapema sana kwamba bosi wao huyo alikuwa amepotea.
Kulikuwa na makundi mengi nchini Msumbiji, waliamini kwamba kulikuwa na wanachama fulani katika kundi fulani ambao walikuwa wakifahamu mahali Bwana huyo alipokuwa, walitaka kuwafahamu watu hao, wakaanza kuwasiliana na vibaraka vyao mbalimbali kwa lengo la kuwaambia kuhusu taarifa juu ya mahali alipokuwa bosi wao.
Baada ya kuulizia kwa siku mbili, tena huku wakitoa ahadi za kutoa kiasi fulani cha pesa kwa mtoa taarifa wakaambiwa kwamba kulikuwa na mtu alihusika katika utekaji wao, mtu huyo alikuwa bilionea Maxwell ambaye alimtumia bilionea mwenye kundi la kihalifu, Moutinho.
“Kwa hiyo ikawaje?” aliuliza Innocent.
“Tuliambiwa kwamba wanakwenda naye Afrika Kusini, wakipita katika ukaguzi, watamuulia huko na mwili wake kuutupa baharini,” alisikika kijana kutoka upande wa pili.
“Basi sawa. Ngoja tufanye upelelezi zaidi,” alisema Innocent na kukata simu.
Hakutaka kuchelewa, haraka sana akampigia simu mtu wake mwingine aliyekuwa Afrika Kusini ambaye kwa miaka zaidi ya kumi walikuwa wakishirikiana kuzipitisha meli zilizokuwa na mzigo wa madawa ya kulevya bandarini.
Kijana huyo aliitwa Xuso. Alimwambia kila kitu kilichokuwa kikiendelea na kumwambia kwamba inawezekana kabisa ni meli ya Bwana Maxwell ndiyo iliyokuwa imetumika hivyo ilikuwa ni lazima kuhakikisha wanaipekua meli hiyo na kuingia ndani ambapo huko watamchukua mtu wao na kundoka naye.
“Hilo si tatizo!”
“Sawa. Hakikisha linafanikiwa!”
“Haina shida. Nitawatumia polisi!”
“Polisi?”
“Si polisi halisi. Hao watakuwa vijana ambao watajifanya polisi, hilo usijali,” alisikika Xuso kwenye simu.
Wakakubaliana na kukata simu. Hakukuwa na mua wa kupoteza, haraka sana mawasiliano yakafanyika na Xuso kuwaandaa vijana wake ambao walitakiwa kutafuta mavazi ya kipolisi tayari kwa kufanya kazi hiyo iliyokuwa mbele yao.
Baada ya saa kadhaa, akapigiwa simu na kuambiwa kwamba vijana walikuwa tayari na hivyo walitakiwa kujiandaa kwa lengo la kuisubiri meli hiyo.
Siku iliyofuata, asubuhi na mapema walifika bandarini, wakazugazuga huku wakizunguka huku na kule. Kila mtu aliwaona vijana hao waliojifanya polisi, walionekana kuwa wapya na si kama wale ambao kila siku hufika mahali hapo na kufanya ukaguzi wa meli.
Baaa ya saa kadhaa, wakaambiwa kwamba kulikuwa na meli ilikuwa ikija, ilikuwa ni meli ya bwana Maxwell ambayo mara nyingi ilikuwa ikifanyiwa ukaguzi wa juujuu kwa kuwa alikuwa akibeba madawa ya kulevya.
Siku hiyo kila mtu aliwaona polisi hao wa bandia kuwa na mzuka wa kufanya kazi. Kwanza walifika mapema lakini pia walionekana kuwa na uchu na meli hiyo kiasi kwamba baahi ya viongozi waliokuwa pale bandarini wakahisi kwamba watu hao waliambiwa mchongo mzima kwamba kulikuwa na ishu iliyokuwa ikichezwa mahali hapo.
Meli ilipofika tu na kutua nanga, harakaharaka polisi wale wakaelekea kule pa kuingilia na kutaka kuingia. Vijana wa Maxwell walishangaa, haikuwa kawaida kwani kila siku walipokuwa wakifika ilikuwa ni lazima wapewe taarifa kwamba kulikuwa na polisi kadhaa ambao walikuwa wamekwishaingiziwa kias cha pesa mapema kabisa.
Siku hiyo hawakupewa taarifa yoyote ile kwani hapo kabla walimalizana na mkuu wa polisi kwamba polisi hao hawakutakiwa kuja pale kwa kuwa walitaka kufanya mambo yao kwa urahisi zaii.
“Who are you?” aliuliza Jackson, mmoja wa vijana wa Maxwell.
“You must be kidding me!” (unanitania!)
“What te hell is going on” (nini kinaendelea?) aliuliza Jackson, uwepo wa polisi wale ulimshangaza kupita kawaida.
Hawakutaka kusikia kitu chochote kile, wakaingia ndani ya meli hiyo kibabe kwa kuwa walitaka kufanya kazi yao. Wazungu hao walibaki nje wakishangaa, siku hiyo waliona kabisa mabadiliko, polisi waliokuja hawakuonekana kuwa na urafiki hata kidogo.
Wakaanza kuingia kwenye chumba kimoja mpaka kingine, walikuwa na bunduki zao mikononi mwao, wakapekua mpaka katika chumba cha mwisho kabisa ambacho ndicho Bwana Todd na Bruno walipokuwa wamefungwa.
Walipoufungua mlango, macho yao yakatua kwa watu hao, polisi hao wakatabasamu, walichokifanya ni kuwachukua wote wawili na kuanza kutoka nao kwenda nje ya meli ile, wakati wakiwa wamekwishafika mlangoni tu, macho yao yakatua kwa polisi wenyewe waliokuwa wamefika mahali hapo huku wakiwa na bunduki mikononi mwao.
“You are under arrest...” (mko chini ya ulinzi) alisema polisi mmoja, na polisi wote wakawanyooshea bunduki.
***
Uwepo wa polisi wa bandia kuwepo mahali pale ulimshtua mkurugenzi wa bandari. Yeye kazi yake kubwa ilikuwa ni kucheza madili makubwa. Mkurugenzi huyo aliyejulikana kwa jina la Kumaro alipigiwa simu na Maxwell na kuambiwa kwamba ahakikishe meli yake siku hiyo inapita pasipo kukaguliwa.
Hilo halikuwa tatizo, akakubaliana nao kwa kuwa tayari hapo kabla alipigiwa simu na Bwana huyo na kuambiwa kwamba siku hiyo hakutakiwa kuhofia kitu chochote kile kwa kuwa polisi wasingefika kabisa mahali hapo kwani tayari alimalizana na kamanda mkuu wa jeshi la polisi hapo Cape Town, Thambo.
Kitendo cha vijana wa Xuso kufika bandarini, kilimshangaza Kumaro na hivyo kuamua kumpigia simu Thambo na kumlalamikia kwamba alichokifanya halikuwa jambo zuri kwa kuwa alimwambia kabisa kwamba kusingekuwa na polisi, sasa mbona kuna polisi walikuwa wamefika mahali hapo?
“Polisi?” alisikika Thambo akiuliza.
“Ndiyo!”
“Sijatuma polisi hapo. Hebu ngoja niwatume polisi waje, nahisi kuna kitu,” alisikika Thambo na kukata simu.
Polisi wa bandia walipoingia ndani ndiyo muda ambao polisi wa kweli walifika mahali hapo. Waliambiwa kila kilichotokea na hivyo kuwasubiri watu hao hapo nje.
Walipotoka tu, hawakutaka kuchelewa, wakawaweka chini ya ulinzi lakini wakati huo wengine walikuwa kwa ndani hata mlango hawakuwa wameusogelea wakiwemo Bwana Todd na Bruno.
Walipowaona wenzao wa mbele wamesimama, tayari wakahisi kulikuwa na kitu tena wakapata hofu kabisa baada ya kusikia wakiambiwa kwamba walikuwa chini ya ulinzi.
Bruno hakutaka kubaki mahali hapo, tayari akili yake ilimwambia kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akamvuta Bwana Todd na kumwambia waondoke kwa kupitia ndani ya meli mpaka nje ya meli hiyo kwa kupitia ubavu wa meli ulioangalia baharini.
“Tumepata msaada...subiri!” alisema Bwana Todd.
“Tusubiri nini? Unajua nani polisi na nani adui yako? Huo aliyesikika akiwaambia hawa apo chini ya ulinzi ni nani? Kama ni polisi, sawa, je hawa ni wakina nani?” aliuliza Bruno huku akimwangalia Bwana huyo.
Kidogo maneno hayo yakamuingia akilini na kuona kwamba kweli inawezekana kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea, akakubaliana na Bruno na hivyo kuondoka kwa kurudi nyuma.
Hawakufika mbali, wakaanza kusikia milio ya risasi, wale watu walioamini kwamba walikuwa polisi walikuwa wakipambana kwa risasi na watu wengine kitu kilichoonyesha kwamba mahali hapo hakukuwa salama tena.
“Tukimbie! Kimbia,” alisema Bruno na kuendelea kukimbia na Bwana huyo.
Walikimbia, hakukuwa na sehemu ya kutokea, walichokifanya ni kuingia katika chumba kimoja miongoni mwa vyumba vingi vilivyokuwa ndani ya meli hiyo.
Ndani ya chumba hicho walikutana na vitanda vya dabo deka, kwa kule pembeni kabisa kulikuwa na kidirisha cha kioo na hivyo kukifuata kwa lengo la kukivunja.
Kilikuwa kioo kigumu mno na isingewezekana kukivunja kwa urahisi kama walivyofikiria. Bruno akaanza kutafuta kitu cha kuvunjia, kila kona aliyokuwa akiangalia kulikuwa na chupa tu ambazo hata kama angezitumia zote hizo asingeweza kuvunja kioo hicho.
“Ni lazima tukivunje kioo hiki ili tutoroke,” alisema Bruno, nje ya kioo kile kulikuwa na bahari na uzuri ni kwamba wingi wa maji hayakuwa sawa na dirisha lile, yalikuwa kwa chini kidogo.
Bruno hakutaka kukata tamaa, aliendelea kutafuta kitu cha kuvunjia kioo ndani ya meli ile na kwa bahati nzuri akakutana na kipande cha chuma, haraka sana akaelekea katika kidirisha kile na kuanza kukigonga.
“Puu..puu...puu...” aliendelea kukigonga kioo kile huku Bwana Todd akiwa pembeni akimwangalia alivyokuwa akipambania maisha yao.
Haikuwa kazi ndogo, ilikuwa ni kazi kubwa mno, alichoka lakini hakuacha kuendelea kugonga kioo kile. Wakati akiendelea kugonga, milio ya risasi ilikuwa ikizidi kuendelea kusikika kutoka kule walipotoka hivyo kumfanya Bruno kugonga kwa haraka zaidi kwa kuamini mara baada ya watu hao kupambana na wale watu waliotoka kuwachukua ndani ya chumba kile, basi watu ambao wangefuata wangekuwa wao.
Alitumia dakika tano, tena kwa kukigonga kwa nguvu zote, kioo kile kikaanza kuvunjika taratibu, kikaanza kutoa alama za mvunjiko, Bruno hakutaka kuacha, akaendelea kugonga zaidi na zaidi hatimaye kioo kuvunjika.
“Tupite kupitia hapa,” alisema Bruno, akachukua shuka lililokuwa kitandani na kuweka kwenye kidirisha kile kwa chini ili kuzuia vipande vya kioo vilivyobaki kutokuwakata.
“Anza wewe kupita...” alisema Bwana Todd.
“Hapana! Anza wewe. Ingia ndani ya maji, piga mbizi kwa nguvu tuelekee upande ule kule wenye meli ile kule kubwa, tukifika kule tutatoka. Ingia, hatuna muda wa kupoteza.Ngoja nikupe boya,” alisema Bruno, hapohapo akampa boya moja lililokuwa kitandani.
“Na wewe?”
“Nitaogelea. Usijali!”
Bwana Bruno akalichukua boya lile na kulivaa. Akapita katika kidirisha kile na kutumbukia ndani ya maji. Bruno hakubaki, naye akapita katika kidirisha kile na kutumbukia majini. Akamshika Bwana Bruno aliyeonekana kutokuwa na nguvu za kuogelea kwa kuwa umri ulienda sana na kuanza kumvuta kuelekea katika upande mwingine wa meli.
Ilikuwa ni lazima kutoroka katika meli ile kama tu walitaka kuendelea kuwa hai.
***
Rahman alikuwa nchini Marekani, alikuwa akisoma katika Chuo cha Mississippi huku moyo wake ukiwa nchini Kenya tu. Alikuwa na furaha tele, kitendo cha baba yake kumwambia kwamba msichana alipatikana tena akiwa ni mzuri mno alisikia furaha ya ajabu moyoni mwake.
Hakuacha kumpigia simu mzee Oloah na kumuuliza zaidi kuhusu binti huyo, leo alipokuwa akiambiwa hivi, kwamba alikuwa mzuri kama malaika, kesho alipiga simu tena na kuuliza alifananaje.
Alichanganyikiwa kupita kawaida, mwili wake ulikuwa nchini Marekani lakini baada ya kuambiwa kuhusu msichana huyo, tayari moyo wake ukahama na kwenda nchini Kenya.
Siku ziliendelea kukatika lakini kwake zilionekana kwenda taratibu sana, alitamani kuondoka kuelekea nchini Kenya ili aende kumuona Sharifa aliyeambiwa kwamba ni mzuri mno lakini hilo halikuwezekana.
Baada ya mwezi mmoja, akamaliza masomo yake na kuanza safari ya kuelekea nchini Kenya. Njiani, mawazo yake yalikuwa kwa msichana huyo, hakuwahi kumuona lakini kichwani mwake kulitengenezwa picha ya msichana mmoja mrembo, aliyekuwa na umbo la kuvutia, sura nzuri na tabasamu lililomfanya kuvutia zaidi.
Baada ya saa ishirini ndege ikafika mjini Dubai, akateremka na kupumzika kwa muda akisubiri kuendelea na safari ya kuelekea nchini Kenya. Hapo, akaelekea kwenye maduka ya nguo na kuanza kununua nguo kwa ajili ya wazazi wake na hata msichana ambaye hakuwahi kumuona.
“Baba aliniambia ni mwembamba, mrefu kidogo, nadhani hizi nguo nitakuwa nimelenga,” alisema huku akichagua nguo kwa ajili ya Sharifa.
Alipomaliza, baada ya saa mbili akapanda ndege na kuendelea na safari ya kuelekea nchini Kenya. Mapigo yake ya moyo yalikuwa juu, alikuwa na presha kubwa, moyo wake ulikuwa na shauku kubwa ya kumuona msichana huyo, alitaka kuona alifananaje, je, alikuwa kama msichana ambaye alimtengeneza kichwani mwake au alikuwa zaidi.
Baada ya saa kadhaa, ndege ikaanza kutua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi. Akateremka na kuanza kupiga hatua kuelekea katika jengo la uwanja huo na abiria wengine huku mizigo yao ikichukuliwa na kupelekwa sehemu kwa ajili ya kuchunguzwa.
Kila kitu kilipokamilika, akapewa mizigo yake na kuondoka mahali hapo. Alipofika nje, akawaona wazazi wake ambao walimfuata, wakamkumbatia na kumpongeza kwa kumaliza masomo yake.
Alifurahi kuwaona, akawasalimia na kitu cha kwanza kabisa kuuliza kilikuwa ni juu ya Sharifa, alitaka kumuona haraka sana, hakuwa radhi kuona akipoteza muda wake pasipo kumuona msichana huyo ambaye kwa kipindi kirefu alichokuwa chuoni mawazo yake yalikuwa kwake tu.
“Kesho tutakwenda kwao!” alisema mzee Olioh huku akimwangalia kijana wake.
“Sawa. Nimemkumbuka mno. Ninampenda, nina uhakika ni mzuri na anastahili kuwa mke wangu!” alisema Rahman huku akiwaangalia wazazi wake.
Furaha ikawa tele nyumbani kwa mzee huyo, kitendo cha kijana wake kurudi salama kutoka masomoni nchini Marekani kilimpa furaha kupita kawaida.
Wakawa watu wa kuzungumza mambo mengi, Rahman aliwaambia mengi kuhusu maisha yake nchini Marekani, jinsi alivyosoma kwa kipindi kirefu na hata kujiepusha na wasichana wa huko ambao nao walikuwa wakimtaka kwa lengo la kulala naye lakini hakuonekana kuwa mwepesi hata kidogo.
“Sina usingizi! Yaani ninatamani hata usiku huu tuondoke kwenda kumuona Sharifa! Hebu niambie tena baba! Anafananaje?” aliuliza Rahman, yaani kila alipokaa mawazo yake yalikuwa kwa Sharifa tu.
“Ni mzuri!”
“Kama?”
“Malaika!”
“Kweli?”
“Niamini! Ni mzuri mno. Mtaratibu, anajielewa, yaani uzuri wake hakuna mfano,” alisema baba yake.
Maneno hayo yakazidi kumtia presha kubwa, hakuamini kama kweli msichana huyo aliyekuwa akiambiwa alikuwa mzuri kiasi hicho, hakuacha kumuuliza baba yake zaidi kuhusu Sharifa kwani kesho yake aliona ni ndefu mno na saa zilikatika taratibu kama kinyonga.
“Ni mweupe?”
“Kama mwarabu!”
“Mungu wangu! Ninavyopenda Waarabu mimi! Nadhani huyo atakuwa ni mzuri sana. Ninataka nimuone jamani! Nilishachanganyikiwa. Leo silali. Baba! Nataka kesho saa kumi na mbili asubuhi twende kwao,” alisema Rahman.
Kama alivyosema ndivyo ilivyotokea, usiku hakulala, alibaki chumbani kwake huku akimfikiria msichana huyo mrembo. Ilipofika asubuhi, yeye ndiye alikuwa na jukumu la kumwamsha baba yake na kumwambia kwamba walitakiwa kujiandaa na kwenda kumuona Sharifa.
Mzee Olioh alishangaa mno, aligundua kwamba kijana wake alitokea kumpenda mno msichana huyo japokuwa hakuwa amemuona. Hakukuwa na tatizo, akajiandaa na ilipofika saa mbili wakaondoka na kuelekea katika Kijiji cha Guolduvai.
Kutoka jijini Nairobi mpaka Guolduvai kulikuwa na umbali wa kilometa mia nne, walitumia saa mbili njiani mpaka kufika huko. Mapigo ya moyo ya Rahman yalikuwa juu mno, macho yake yalikuwa na hamu kubwa ya kumuona Sharifa kuliko kitu chochote kile.
Walipofika, gari likasimamishwa na kuelekea katika nyumba ya mzee Jumanne. Kwa jinsi wasichana wengine walivyokuwa wakionekana kijijini hapo, Rahman alipata hofu kwamba inawezekana baba yake alimremba tu lakini Sharifa hakuwa mrembo kama alivyokuwa ameambiwa.
Wasichana wengine walikuwa wa kawaida kabisa, sasa ilikuwaje huyo Sharifa aliyekuwa akizungumziwa kuwa na uzuri kama ule aliokuwa ameambiwa?
Wakakaribishwa ndani ya nyumba hiyo kwa furaha na kutulia. Muda wote macho ya Rahman hayakutulia, alikuwa akiangalia huku na kule, kila mtu aliyekuwa akiingia ndani ya nyumba hiyo alikuwa akimwangalia mno.
“Tumekuja kumuona Sharifa kwanza!” alisema mzee Olioh.
Hilo halikuwa tatizo, Sharifa ambaye alikuwa uani akaitwa mahali hapo. Jinsi alivyoitikia, hiyo Beee alivyoitoa moyo wa Rahman ukamlipuka na kuanza kudunda kwa nguvu kana kwamba ulitaka kuchomoka.
Wala hazikupita sekunde nyingi, Sharifa akatokea sebuleni hapo. Macho ya Rahman yalipotua kwa msichana huyo hakuamini kama alikuwa akimwangalia binadamu au malaika.
Alikuwa msichana mrembo mno, msichana wa ajabu ambaye alikuwa na uhakika kwamba wakati Mungu alipokuwa akimuumba alihakikisha amemaliza kazi zake zote na kuanza kumuumba msichana huyo tena kwa udongo maalumu.
Alikuwa na uzuri wa ajabu. Moyo wa Rahman ukazidi kudunda na kuchanganyikiwa, alishindwa kuamini kama yeye ndiye ambaye angemuoa msichana huyo, kulala naye kitanda kimoja na hatimaye kuzaa watoto.
Akashindwa kujizuia, tabasamu pana likaonekana usoni mwake, akatamani kusimama na kwenda kumkumbatia kwani kwa jinsi alivyoonekana, alikuwa bab’ kubwa.
“Sharifa...” Rahman alijikuta akiita, baba yake akamminya kwa mguu na kumtaka atulie. Si kwamba aliliita jina hilo kwa makusudi, lilimtoka tu mdomoni kwani ule uzuri aliouona kwa msichana huyo hakika ulimchanganya.
Sharifa akakaa kochini na baba yake kuanza kutoa utambulisho. Akamwambia Sharifa kuhusu ugeni ule, mzee Olioh hakuwa mgeni machoni mwake, alimfahamu, alikuwa mzee yule aliyekuja mahali pale mwezi uliopita na kuzungumza na baba yake kuhusu kijana wake aliyetaka kumuoa na bila shaka kijana aliyekuwa naye ndiye ambaye alitaka kumuoa.
Alibaki akiangaliana na Rahman. Kwake, hakukuwa na mwanaume mzuri kama Bruno, pamoja na umasikini aliokuwanao kijana yule bado alikuwa akimpenda vilevile, kwake, hata kama angekuja mwanaume mzuri kuliko wote katika dunia hii, moyo wake ungeendelea kuwa kwa Bruno tu.
Walizungumza mno, baadaye akapewa nafasi Rahman, kama kawaida akaanza kushukuru na mwisho wa siku kumshukuru baba yake kwa kuamua kumchagulia msichana ambaye alikuwa mzuri zaidi ya alivyokuwa akifikiria.
“Sharifa ni msichana mzuri, msichana ambaye naamini atakuwa bora katika maisha yangu, mke bora ambaye nitakuwa naye kwenye shida na raha,” alisema Rahman huku akimwangalia Sharifa kwa jicho lililoashikilia mapenzi makali aliyokuwanayo juu yake.
Kila mtu aliongea lake, mzee Jumanne alionekana kuwa na furaha tele, kitendo cha binti yake kuwa mkimya mahali hapo kilionyesha kabisa kwamba alikubaliana na kile kilichokuwa kikiendelea.
Walichokifanya kama wazazi ni kuwaachia nafasi wawili hao sebuleni wakae na kuzungumza kwa muda, wazoeane ili mapenzi yaanze huku mipango ya kufungwa ndoa ianze kufanyika.
“Nimetokea kukupenda sana Sharifa. Nilipoambiwa kuhusu wewe, hakika sikuwa na swali kwani naamini kwamba baba yangu huchagua vilivyo bora kabisa,” alisema Rahman huku akimwangalia Sharifa ambaye alikuwa kimya kabisa.
“Ninakupenda Sharifa. Upo tayari kuwa mke wangu wa ndoa?”
“Hapana!”
 
Bruno The Fishman

Mtunzi.Nyemo

Episode 3

“Kwa nini tena jamani? Tatizo nini Sharifa!”
“Hapana! Umeniuliza, nimekwambia hapana! Kuna swali tena katika hilo?” aliuliza Sharifa huku akimwangalia Rahman.
Moyo wa Rahman ukanyong’onyea, hakuamini alichokuwa amekisikia. Mategemeo yake yalikuwa tofauti na jinsi alivyodhani hapo kabla, alihisi kwamba baba yake alimaliza kila kitu na ni yeye tu ndiye aliyekuwa akisubiriwa kwa msichana huyo.
Hilo lilimuuma lakini hakutaka kukata tamaa, alijua kwamba huyo alikuwa msichana na kama angeendelea na msisitizo wake basi kuna siku angekubaliana naye.
Mpaka wazazi wanarudi mahali hapo, hakukuwa na kitu kilichobadilika lakini Rahman aliona ni muda wake kupambana.
Maisha yaliendelea, hakuacha kwenda Guolduvai, mara kwa mara alikuwa akienda huko na kuonana na Sharifa, alimuonyeshea kwamba alimpenda kupita kawaida, kila alipokuwa akienda alibeba zawadi kwa ajili ya msichana huyo.
Bado hakuweza kuubadilisha moyo wa Sharifa, msisitizo wake ulikuwa uleule kwamba hakutaka kuwa na mwanaume huyo. Mwezi mmoja ulipokatika, ndipo kidogo moyo wa Sharifa ukaanza kulegea na hatimaye akaanza kumkubali Rahman kwani alionekana kuwa mwanaume mpole na mwenye uvumilivu mkubwa mno.
Tabasamu likaanza kuonekana usoni mwake na hatimaye kumwambia kwamba alikubali kuolewa na yeye lakini kwa sharti moja tu, kama lingeshindikana basi amuache na kufa akiwa hajaolewa.
“Nipo tayari kwa sharti lolote lile,” alisema Rahman.
“Ni kwamba nilikuwa na mpenzi!”
“Niliambiwa. Si huyo Bruno?”
“Ndiyo! Inasemekana alikufa baharini. Ila mimi siamini hilo hata kidogo. Najua atakuwa hai sehemu fulani,” alisema Shakira.
“Labda! Hakuna ajuaye.”
“Sasa basi. Kama kuna siku atarudi tena na kugundulika hakufa! Huo ndiyo utakuwa mwisho wangu mimi na wewe hata kama utakuwa umenioa na kukuzalia watoto,” alisema Shakira.
“Haina shida.”
“Unahisi utaweza kuniacha nikaendelea na maisha yangu na mpenzi wangu?”
“Nitakuruhusu! Nakuahidi kukuruhusu endapo atarudi.”
“Sawa. Kama ni hivyo hakuna tatizo!”
Wakakubaliana na maisha kuendelea. Walikuwa wakifanya kila kitu isipokuwa mapenzi tu. Waliahidiana kwamba wangefanya mapenzi siku ambayo wangeoana na kuwa mume na mke. Kwa Rahman hilo halikuwa tatizo hata kidogo, alichokuwa akikiangalia ni kuwa na msichana huyo tu.
Siku zikaendelea kukatika, wazazi wakafurahia na hatimaye tarehe ya kufunga ndoa ikapangwa na wawili hao kujiandaa. Kwa mzee Jumanne ilikuwa ni furaha tele, hakuamini kama hatimaye alifanikiwa kumlaghai mtoto wake na hatimaye alikuwa akiolewa na kijana kutoka katika familia ya kitajiri.
“Hakika umenifanya nijisikie baba! Nakupenda sana binti yangu! Naomba usahau yote yaliyopita,” alisema mzee Jumanne.
“Asante baba! Nimekusamehe!” alisema Sharifa.
Siku zikakatika na hatimaye siku ya harusi kufikia. Kila mmoja alionekana kuwa na furaha tele. Sharifa alichukuliwa na kupelekwa Nairobi, akafanyiwa shopping ya maana huku ikiwa tayari imepita miezi sita tangu alipopewa taarifa ya kifo cha mpenzi wake.
Akarudi Guolduvai akiwa Sharifa mwingine, alibadilika, alikuwa mrembo. Chakula kikapikwa, watu wakajiandaa kusherehekea sherehe hiyo. Simu ikapigwa na kuambiwa kwamba msafara wa bwana harusi ulikuwa njiani kuja kuchukua mke.
Wanawake walikuwa wakicheza ngoma, siku hiyo hakukuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea kijijini hapo zaidi ya kusherehekea harusi hiyo kubwa.
Bwana harusi alipofika tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kupelekwa katika uwanja maalumu wa kucheza ngoma za kitamaduni na kuanza kucheza. Madrasa ikaanza kazi yake, ikapiga madufu na dua ya maana kupigwa.
Wakati bwana harusi akijiandaa kufunga ndoa huku mzee Jumanne akiwa amekwishakaa kwenye mkeka tayari kwa kufungishwa ndoa hiyo, kwa mbali alionekana Abdul akiwa anakimbia kwa kasi, shati lilikuwa mkononi mwake, watu walimshangaa, hakuwa akikimbia kimya kimya, alikuwa akipiga kelele kwa nguvu huku akiliita jina la Sharifa.
Shekhe aliyetaka kufungisha ndoa ikabidi anyamaze na kumwangalia kijana huyo ambaye alipitiliza mpaka katika chumba alichokuwamo Sharifa kitu kilichomfanya kila mtu kupigwa na butwaa.
“Sharifa...Sharifaaa...Sharifaaa...” aliita Abdul huku akiwa ameingia, Sharifa aliyekuwa kitandani na shela lake akashtuka baada ya kuona mlango umefunguliwa.
“Kuna nini?”
“Bruno yupo hai! Bruno yupo hai Sharifa....” alisema Abdul huku akimwangalia Sharifa aliyeonekana kushtuka.
“Yupo wapi?”
“Sijui! Ila yupo hai! Tuondoke! Bruno yupo hai,” alisema Abdul huku akimshika Sharifa mkono na kumvuta.
Kitendo cha kusikia Bruno yupo hai, Sharifa alichanganyikiwa. Hakukuwa na ndoa tena, huyo ndiye alikuwa mwanaume wa maisha yake, alikubaliana na Rahman kwamba kama mwanaume wake angerudi tena kusingekuwa na ndoa.
Wakatoka ndani, wakapita katika umati wa watu waliokuwa nje ambapo ndoa ilitaka kufungwa. Mzee Jumanne alibaki akishangaa, akasimama na kumuita binti yake aliyekuwa akikimbia na Abdul.
“Sharifa...Sharifa kuja hapa...” alisema mzee huyo.
“Siwezi! Siwezi baba! Bruno yupo hai...” alisema Sharifa huku akikimbia, maneno hayo yalimfanya kila mtu kushtuka, iliwezekanaje mwanaume huyo awe hai na wakati alikufa baharini tena miezi sita iliyopita.
Hata kuwakimbiza wakashindwa kwani watu hao walikuwa wakikimbia kwa kasi huku shela likiwa mwilini mwa Sharifa. Ni ndani ya dakika moja tu, wakapotea machoni mwao. Ubwabwa ukawa mchungu. Pale Rahman alipokuwa, alitamani ardhi ipasuke atumbukie ndani.
***
Hawakuchukua muda mrefu baharini wakafanikiwa kufika nchi kavu ambapo moja kwa moja wakaanza kuondoka huku eneo zima likiwa halina mtu kutokana na milio ya risasi iliyokuwa ikisikika mahali hapo.
Wakaondoka mpaka katika geti namba sita la kuingilia bandarini hapo, hawakutaka kupoteza muda, haraka sana wakaondoka mahali hapo na kwenda barabarani.
Bruno hakujua kitu chochote kile, hakujua ni mahali gani walitakiwa kuelekea, alibaki huku akiangalia huku na kule, kazi yake kubwa ilikuwa ni kumtoa mzee yule ndani ya meli ile na baada ya hapo basi mzee huyo ndiye angeshikilia usukani kwa kuwa alipafahamu Afrika Kusini tofauti na yeye ambaye ilikuwa ni mara ya kwanza kufika mahali hapo.
“Where to?” (twende wapi?) aliuliza Bruno huku akimwangalia mzee yule.
“Wait?” (subiri)
Akasubiri. Mzee Todd akatulia, alionekana kama mtu aliyekuwa akijifikiria kitu fulani hivi. Baada ya dakika moja, akauinua uso wake na kumwambia Bruno kwamba walitakiwa kwenda sehemu, katika Mtaa wa Kloof ambao ulikuwa na maduka mengi, mtaa pekee ambao ulikuwa ukiongozwa kutembelewa na wakazi wengi wa hapo Cape Town.
Mzee huyo aliendelea kumwambia kwamba huko kulikuwa na mtu aliyekuwa akimfahamu ambaye angewasiliana naye na kuondoka kurudi nchini Marekani. Wakaanza safari ya kuelekea huko huku kila mmoja akiwa hana kitu kabisa mfukoni mwake.
Kwa jinsi walivyokuwa wakionekana, hakukuwa na mtu aliyeamini kama watu hao walitakiwa kutembea katika jiji hilo la kitalii, jiji lililojaza watu wenye pesa ambapo kila mtu aliyekuwa akionekana barabarani alikuwa na muonekano wa pesa.
Safari ya kwenda Kloof haikuchukua muda mrefu, wakafika. Ulikuwa mtaa uliokuwa na watu wengi waliokuwa wakizunguka huku na kule, wengine walikuwa wakijipiga picha za ukumbusho huku wengine wakifanya manunuzi yao.
Wakaelekea mpaka katika sehemu iliyokuwa na nyumba nyingi za kifahari, mageti makubwa, sauti nyingi za mbwa zilikuwa zikisikika, wakalifuata jengo moja na kuanza kugonga geti, wala hazikupita sekunde nyingi, sauti ya mlinzi ikaanza kusikika kutoka katika kipaza sauti kidogo kilichokuwa kimepachikwa ukutani.
“Wewe nani?” alisikika mlinzi huyo.
“Todd.”
“Nikusaidie nini?”
“Ninataka kuonana na Brown.”
“Una miadi naye?”
“Hapana! Naomba kuonana naye.”
Alichokifanya mlinzi ni kupiga simu ndani ambapo akalisema kama alivyoambiwa. Alimwambia mzee huyo kwamba kulikuwa na mtu aliyekuwa akimuulizia aliyeitwa Todd. Mtu ambaye alikuwa akimfahamu mwenye jina hilo alikuwa mmoja tu, mfanyabiashara maarufu aliyekuwa na utajiri mkubwa.
“Todd! Haiwezekani kuja bila taarifa, hebu subiri,” alisema Brown.
Hapohapo akaelekea katika chumba kilichokuwa na kompyuta mbili na kuanza kuangalia nje kupitia kamera ndogo za CCTV zilizokuwa getini. Aliwaona watu wawili waliokuwa wamesimama, mmoja alimfahamu vilivyo, alikuwa ni mzee Todd lakini kwa jinsi alivyoonekana, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea.
Hakutaka kubaki ndani, akaondoka na kuelekea getini, akamwambia mlinzi afungue geti, akafanya hivyo na watu hao kuingia. Alimwangalia Todd, hakiamini kama alikuwa yeye, alibadilika, alionekana mchafu, hakuwa yule Todd aliyekuwa akimfahamu.
“Kuna nini kimetokea?”
“Ni habari ndefu sana. Naomba tuingie ndani kwanza,” alisema Todd.
Hilo halikuwa tatizo, wakaingia ndani na kuanza kumuhadithia kila kitu kilichokuwa kimetokea. Alimwambia kuhusu mpango uliokuwa umesukwa, mpango ambao alikuwa na uhakika kwamba nyuma yake kulikuwa na mtu lakini bahati mbaya hakumgundua mtu aliyekuwa nyuma yake.
“Na huyu?”
“Ni kijana ambaye naye aliletwa ndani ya meli ile,” alijibu Todd kuhusu Bruno.
Brown akanyamaza, akamwangalia Todd, hakuamini alichokuwa amekisikia, alihisi kudanganywa. Akamwambia kwanza asubiri aende chumbani ambapo angempa pesa na kwenda kumfanyia harakati zote za kusafiri na kurudi nchini Marekani.
“Nitashukuru sana,” alisema Todd.
Brown akaondoka. Sebuleni walibaki wawili. Bruno alimwangalia Todd, alikuwa mwanaume mzee, aliyehitaji sana msaada wake, alijua kabisa kwamba kama angemuacha pasipo mtu huyo kufika nchini Marekani basi ingekuwa vigumu sana kufika kwa kuwa tu wale watu ambao waliwatoroka wangemtafuta na kumuua.
Walikuwa wamezungumza na Brown, kwa jinsi alivyoonekana, Bruno alihisi kulikuwa na kitu. Akamwambia Todd kwamba walitakiwa kuondoka mahali hapo kwa kuwa moyo wake haukuwa na amani na mwanaume huyo aliyekuwa amewakaribisha.
“Ni rafiki yangu!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo!”
“Unamwamini?”
“Asilimia mia moja. Tusubiri!” alisema Todd ambaye alionekana kutokuwa na hofu hata kidogo.
“Hapana! Simuamini. Nahisi kuna jambo. Tuondoke!” alisema Bruno lakini mzee huyo aliendelea kukataa kwa kumwambia kwamba waendelee kubaki kwa kuwa msaada pekee uliokuwa umebaki ulikuwa ni kwa rafiki yake huyo.
Huku wakiwa wamejiachia kwenye kochi na Kituo cha Televisheni cha SABC kikiendelea na matangazo huku kikiwa kimejiunga na Kituo cha Habari cha CNN cha nchini Marekani, wakaona taarifa ya habari ambayo ilimshtua kila mmoja.
Kulikuwa na mtu aliyekuwa akitafutwa kwa kuhusishwa na madawa ya kulevya. Nyumbani kwake kulikutwa na kilo tano za madawa ya kulevya, nakala ambazo zilionyesha kabisa kwamba alikuwa akiifanya biashara hiyo kupeleka Mexico, Cuba na sehemu nyingine.
Polisi waligundua hilo baada ya kwenda kupekua nyumbani kwake na kukuta vitu hivyo vyote. Wote wawili walishangaa kwani mtu huyo aliyekuwa akitafutwa alikuwa Todd.
“Nini?” aliuliza Todd huku akisimama na kuisogelea televisheni.
Hakuamini alichokuwa akikiangalia, alishangaa, ni kweli alikuwa akifanyya biashara ya madawa ya kulevya tena kwa siri kubwa, na hakuwahi kuyapeleka madawa hayo nyumbani na hata familia yake haikuwa ikijua kilichokuwa kikiendelea, sasa iweje mzigo wa madawa hayo yakutwe nyumbani kwake? Nani aliyaweka na wakati hakuwahi kufanya kitu kama hicho?
“Tuondoke,” alisema Bruno, bado hakuwa na amani.
“Hapana! Brown atanisaidia,” alisema mzee huyo huku akianza kutokwa na machozi, alitia huruma.
Bruno hakuwa na imani na Brown, alihisi kabisa kwamba mtu huyo kulikuwa na jambo alilotaka kulifanya. Akayapeleka macho yake katika televisheni ambapo ilitangazwa kwamba kwa yeyote ambaye angefanikisha kukamatwa ka mzee huyo basi angepewa kiasi cha dola milioni mbili.
“Tuondoke!” alisema Bruno kwa hasira, hakutaka tena kuona mzee huyo akikataa, akamshika na kuanza kumvuta kwenda nje.
Todd alikataa lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana na Bruno na kuondoka naye mahali hapo kwani hakuwa na jinsi, kama kweli mwanaume huyo alikuwa na hofu na Brown, basi hakuwa na jinsi.
***
Bilionea Maxwell alishika simu yake na kuanza kuongea na Innocent, kijana ambaye alikuwa karibu sana na mzee Todd. Alimpigia simu kwa lengo moja tu la kutaka kucheza mchezo fulani ambao aliamini ungeweza kumpoteza kabisa Todd.
Alimwambia kuhusu mpango wake aliokuwa nao, alihitaji mtu wa kumsaidia na hakuona kama kungekuwa na mtu mwingine zaidi ya Innocent. Alimwambia wazi kwamba alitenga kiasi cha dola milioni moja kwa ajili yake kama malipo kwa kazi kubwa aliyoitaka aifanye.
Dola milioni moja kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kiliichanganya mno akili ya kijana huyo. Haraka sana akamuuliza kuhusu kazi hiyo, hakutaka kumficha, alimwambia kwamba alitakiwa kumsaliti mzee Todd.
“Kivipi?”
“Ninataka kuiteka familia yake, si kwa nia mbaya, hapana, ni kwa nia nzuri sana na baadaye nitaiachia,” alisema Maxwell kana kwamba alikuwa mtu mzuri.
“Mmh!”
“Ndiyo! Unaweza kunisaidia katika hilo. Nitakulipa dola milioni moja keshi,” alisikika mzee huyo.
Hilo lilionekana kuwa jambo gumu lakini kiasi cha pesa alichokuwa ametajiwa kilikuwa kikubwa mno, kilimchanganya, hakutaka kuona kiasi hicho cha pesa kikipita mbele yake, kama alitakiwa kumsaliti basi hakukuwa na tatizo lolote lile.
Alikuwa bosi wake, alimfanyia kazi, hakuwa ndugu yake, kama alikuwa bosi wake, aliamini kuna siku mzee huyo angekuwa na uwezo wa kumfukuza na kumuajiri mtu mwingine kwa kuwa tu alihitaji pesa na hata muda mwingine kubana matumizi.
Alijitoa kafara na kumwambia Maxwell kwamba alikubaliana naye hivyo hizo pesa ziandaliwe, hilo halikuwa tatizo. Alichokifanya Maxwell ni kuwasiliana na vijana wake na kuwaambia kwamba alihitaji mzigo wa madawa ya kulevya kilo tano, akapelekewa na kuanza kuwapa maelekezo juu ya nini kilitakiwa kufanyika.
Akapigiwa simu Innocent na kuambiwa kwamba kuna vijana wangekwenda nyumbani hapo na kuingia ndani, walinzi wasingeweza kuwagundua kwa kuwa yeye mwenyewe alitakiwa kusema kwamba alikuwa akiwafahamu kama marafiki wa Todd.
Hilo likafanyika, vijana wakaelekea huko. Innocent mwenyewe hakuona jinsi madawa yalivyokuwa yamebebwa kwani yalibebwa kwa siri sana tena kwa vifurushi vidogo.
Wakati wameingia mpaka sebuleni na vijana wanne, Innocent akaenda kumuita mke wa Todd. Kitendo cha kuondoka sebuleni hapo kilionekana kuwa kosa kubwa, hapohapo vijana wale wakachukua vifurushi vile vya madawa na kuanza kuvificha katika makochi na sehemu nyingine.
Mpaka Innocent na mkewe wa Todd wanafika sebuleni, tayari walikamilisha kila kitu. Wakamwambia mwanamke huyo kwamba walitakiwa kwenda sehemu kuonana na mume wake kwa kuwa alikuwa amejificha kwa kuogopa kutafutwa na wabaya wake.
“Mnasemaje?”
“Mzee yupo! Amejificha, alikwenda nchini Msumbiji. Kuna watu walimteka na kutaka kumuua, alifanikiwa kuwatoroka na kuja huku. Wabaya wake wapo hapahapa jijini New York, ameogopa kuja nyumbani kwani anaamini kwamba wanaweza kuja hapa na kumuua,” alisema kijana mmoja kwa sauti ya unyenyekevu, tena kwa suti aliyokuwa amevaa, ilikuwa vigumu kugundua kama alikuwa mtu mbaya.
“Yupo wapi?”
“Kwenye jumba lake la mafichoni. Mama! Mzee yupo kwenye hatari sana,” alisema kijana huyo, akabadilisha muonekano wa sura yake, akawa na huruma ghafla kama Papa John Paul wa Pili alivyokuwa.
“Jamaniiiiii!”
“Mama hatuna muda,” alisema kijana huyo.
Hakutaka kuchelewa, kwake, mume wake alikuwa kila kitu moyoni mwake, alimpenda kuliko kitu chochote kile. Kwa kuwa aliambiwa kwamba mumewe alikuwa akimsubiri, akamuita na binti yake kwa lengo la kwenda huko kuonana naye.
Wakaondoka kwa kuwa alimwamini kijana yule lakini la zaidi ni kwa sababu alimwamini Innocent. Walinzi hawakujua chochote kile, wakawaruhusu kuondoka, wakaingia ndani ya gari na kuondoka.
Baada ya Maxwell kuambiwa kwamba kila kitu kilikamilika, akapiga simu polisi na kujidai akitoa taarifa ya madawa ya kulevya. Polisi walivyosikia tu, haraka sana wakaelekea huko, walipofika na kufanya upekuzi, wakayakuta madawa hayo ya kulevya na hivyo mtu wa kwanza kushukiwa alikuwa mzee Todd.
Taarifa ikatolewa kwamba mzee huyo alikuwa akitafutwa, na mbaya zaidi ilitoka taarifa iliyosema kwamba alikwenda Afrika kupeleka mzigo mwingine. Kiasi cha dola milioni moja kikawekwa mezani kwa kila mtu ambaye angefanikisha kukamatwa kwake.
***
Mke wa mzee Todd, Juddie na mtoto wake, Martha walipelekwa mpaka katika chumba kilichokuwa na mwanga hafifu na kuambiwa watulie kwenye viti vilivyokuwa ndani ya chumba hicho.
Hawakuelewa mahali walipokuwa, walikuwa wakiangalia huku na kule, chumba hicho kiliwaogopesha kwani mbali na kuwa na viti hivyo pekee, kuta za chumba hicho zilikuwa na michirizi ya damu ambayo ilionyesha kabisa kwamba hakikuwa chumba cha mchezo hata kidogo.
Waliogopa, hawakujisikia amani. Japokuwa waliambiwa kwamba Todd alikuwa huko na ndiye ambaye alikuwa akiwahitaji, hawakuhisi kama kweli hilo jambo lilikuwa hivyo, walihisi kabisa kulikuwa na kitu kilichokuwa kikiendelea.
Walimwamini Innocent, hawakuwa na hofu naye hata kidogo. Watu waliokuwa wamewachukua hawakuwafahamu lakini kwa kuwa Innocent alihusika katika kila kitu, hawakuhofia kitu chochote kile.
Wanaume wale walikuwa wakiingia kwa zamu, kila walipowauliza, walijibiwa kwamba walitakiwa kutulia kwani kila mtu aliyekuwa ndani ya chumba kile hakutakiwa kupiga kelele kwa kuwa ukimya ndiyo ulikuwa ulinzi wao pekee.
“Tell us, where is Todd?” (tuambie, Todd yupo wapi?) aliuliza Juddie.
“I told you to shout the hell up,” (nimekwambia nyamaza) alisema mwanaume huyo kwa hasira na sauti kubwa iliyomfanya Juddie na mtoto wake, Martha kuogopa.
Wote waliogopa, waliwaona watu hao kuwa mahatili ambao wangewatoa roho yao muda wowote ule kama tu wangeendelea kuongea kitu ambacho hakikutakiwa kufanyika ndani ya chumba hicho.
Waliendelea kukaa mpaka ilipofika usiku wa manane. Hawakulala, bado walikuwa wakiamini kwamba Todd angetokea lakini mpaka inafika alfajiri hakukuwa na dalili za mwanaume huyo na kugundua kwamba kulikuwa na jambo jingine lililokuwa likiendelea.
Asubuhi, wakaletewa chai na kuanza kunywa. Hawakunywa kwa raha, walikunywa huku wakiwa na hofu nzito mioyoni mwao. Ilipofika majira ya saa nne, mwanaume mmoja akaingia na kuanza kuzungumza nao.
Huyo ndiye aliyewaambia kilichokuwa kikiendelea, walikuwa mahali pale kwa kwa sababu Todd alikuwa amewafanya jambo baya ambalo hakutaka kuwaweka wazi. Walishangaa, waliuliza kuhusu jambo hilo baya, hawakuambiwa kitu zaidi ya kuambiwa watulie tu.
Maxwell alipigiwa simu na kuambiwa kwamba kila kitu kilikuwa tayari. Akaridhika na hivyo kuanza kumtafuta Todd kwenye simu lakini akamkosa.
Hakutaka kujali sana, alichokifanya ni kuwapigia vijana wake na kuwauliza kilichokuwa kikiendelea. Kitu ambacho kilimchosha ni baada ya kusikia kwamba mwanaume huyo alikuwa ametoroka.
“Ametoroka?” aliuliza Maxwell, hakuamini alichokuwa amekisikia.
“Ndiyo mkuu!”
“Inawezekana vipi? Hivi kweli anaweza kutoroka ndani ya meli? Anaweza kuogelea?” aliuliza Maxwell huku akionekana kuchanganyikiwa.
Kijana huyo akaanza kumwambia kila kitu kilichokuwa kimetokea bandarini mpaka Todd kutoroka akiwa na kijana waliyemuokota baharini kwa lengo la kumsaidia.
Maxwell alichanganyikiwa, hakuamini alichokisikia, akahisi kabisa alikuwa akidanganywa au kulikuwa na mchezo uliokuwa umechezwa. Si kwamba hakufahamu kuhusu mapigano ya risasi yaliyotokea bandarini huko Cape Town, alifahamu kila kitu lakini kilichomshangaza ni namna ambavyo watu hao walitoroka.
Kwa hasira, akawaambia wawatafute na kukata simu. Kichwa chake kilichanganyikiwa. Kutoroka kwa Todd kilimaanisha kitu kibaya kwake, hakutaka kuona mwanaume huyo akiendelea kuwa hai, kuendelea kuwa hai kungemaanisha mwisho wake kwani kwa namna moja ama nyingine ilikuwa ni lazima kumtafuta na kulipa kisasi.
Wakati huo, taarifa za habari katika vituo mbalimbali vya televisheni vilikuwa vikitangaza kuhusu kutafutwa kwa mwanaume huyo. Kila kona, picha yake ilionekana.
Dunia ilipigwa na butwaa, kile kilichokuwa kikionekana kilimshangaza kila mmoja. Wengi hawakuamini kama utajiri wa mzee huyo ulitokana na biashara ya madawa ya kulevya aliyokuwa akiifanya.
Wema wake, ukasahaulika, chuki za Wamarekani dhidi yake zikaanza kutawala katika mioyo yao. Kila kona watu walikuwa wakiongea kuhusu jambo hilo tu, waliandika mabango, kwenye mitandao walitoa maoni yao huku wakiitaka dunia iseme mahali alipokuwa mwanaume huyo aliyekuwa akiwapoteza vijana wengi kwa kuwauzia madawa ya kulevya.
Maofisa wa FBI (Federal Bureau Of Investigation) wakaanza kumtafuta nchini Marekani huku wale wa CIA (Central Interlligence Agency)wakiondoka kwenda barani Afrika ambapo waliambiwa mtu huyo alikuwepo kwa lengo la kumtafuta.
“We have one week! We have to arrest this dude,” (tuna wiki moja! Inapaswa tumkamate huyu mshikaji) alisema ofisa mmoja.
“Did you find out where he is by now?” (ulikwishajua mahali alipokuwa sasa hivi?)
“Nope! But we have to,” (hapana ila inabidi tumkamate)
Wakati picha zake zilipokuwa zikitoka katika vyombo mbalimbali vya habari ndipo kipindi hichohicho ambacho Brown aliona kwenye televisheni. Alichoamini ni kwamba Todd alikuwa nchini Marekani lakini baada ya kuambiwa na mlinzi kwamba alikuwa akihitajika na mwanaume huyo getini, hakuamini.
Kiasi cha pesa kilichokuwa kimewekwa kilikuwa kikubwa mno, hakutaka kuona akikikosa, kwake, pesa zilikuwa muhimu kuliko hata urafiki. Alikwishawahi kuua watu wengi kwa sababu ya pesa, aliwasaliti watu wengine kwa sababu ya pesa, sasa kumsaliti Todd na kumchoma kwa polisi hakukuwa na tatizo lolote lile.
Kule chumbani alipoelekea, akachukua simu yake na kuwapigia polisi. Aliwaambia kwamba alimuona Todd yule aliyekuwa akitafutwa na muda huo aliokuwa akizungumza nao alikuwa ndani ya nyumba yake, hivyo walitakiwa kufika haraka sana kumkamata.
“Una uhakika ni yeye?” lilikuwa swali la kwanza kutoka kwa polisi aliyekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu.
“Acha ushamba! Sasa kama sina uhakika ningewapigia?” aliuliza Brown, swali alilokuwa ameulizwa lilimkasirisha kupita kawaida.
Simu ilipokatika, akaondoka na kurudi sebuleni, alitaka kupiga stori na watu hao mpaka pale ambapo polisi wangefika na kumkamata. Alipokwenda sebuleni, kilichomshangaza ni kwamba mwanaume huyo hakuwepo. Alichanganyikiwa, akatoka na kwenda kwa mlinzi, akamuuliza na kumwambia kwamba watu hao wawili waliondoka.
“Kwa nini uliwaruhusu?”
“Hukuniambia niwazuie mkuu! Nilidhani umemalizana nao,” alijitetea mlinzi.
Hilo lilimchanganya mno, aliona kabisa mamilioni ya dola yakiondoka mikononi mwake katika hatua ya mwisho kabisa. Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya, alitoka mpaka nje ya nyumba ile na kuangalia huku na kule, si Todd wala Bruno aliyekuwa akionekana.
Njiani, Todd na Bruno walipishana na gari mbili za polisi zikienda kule walipokuwa wametoka. Hapo, ndipo Todd akaamini kwamba Brown hakuwa mtu mzuri, alikuwa amewachongea kwa polisi kwa kuwa kukamatwa kwake kungemfanya kupata kitita cha dola milioni moja.
***
Rahman alihisi kuchanganyikiwa, pale alipokuwa hakukukalika hata kidogo, alimwangalia mzee Jumanne ambaye naye kwa kumwangalia tu alionekana kuchanganyikiwa kama alivyokuwa.
Alimpoteza mwanamke aliyekuwa akimpenda, tena katika hatua ya mwisho kabisa kabla ya kufunga ndoa. Alinyong’onyesa, pale alipokuwa alihisi kabisa akipigwa na baridi kali na kuanza kutetemeka,
Uso wake ukajawa na aibu, kila mtu aliyemwangalia, akamuonea huruma kwani hakuvumilia, ni ndani ya sekunde chache machozi yakaanza kutiririka mashavuni mwake.
Alimpenda mno Sharifa, kwake, msichana huyo alikuwa kila kitu. Alimuahidi mambo mengi mno, na kweli angeyatimiza kwa kuwa alikuwa akimpenda lakini cha kushangaza, msichana huyo akakimbia huku akipiga kelele kwamba hataki kuolewa kwa kuwa Bruno alikuwa hai.
“Who is this man?” (huyu ni nani?) alimuuliza baba yake huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Bruno! The poorest fella in the village,” (Bruno! Mwanaume masikini kabisa hapa kijijini) alijibu baba yake kwani aliambiwa na mzee Jumanne kwamba Bruno alikuwa masikini mno.
Mzee Jumanne alihisi miguu ikimtetemeka, alihisi kama angeanguka muda wowote ule kwani kile kilichokuwa kimetokea, hakukiamini hata mara moja.
Hakutaka hata kumwangalia Rahman, alijua ni kwa jinsi gani mwanaume huyo alikuwa amechanganyikiwa, mtu muhimu kabisa ambaye alitakiwa kuzungumza naye alikuwa James, yeye ndiye aliyemuagiza kwenda kumuua Bruno, kama hakufa, nini kilitokea.
James alikuwa kwenye harusi hiyo, yeye mwenyewe alikuwa amepigwa butwaa, hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea mpaka Abdul kufika mahali hapo na kusema kwamba Bruno alikuwa hai.
“James! Nini kimetokea?” aliuliza mzee Jumanne.
“Sijui ni kitu gani kimetokea.”
“Wewe si ulisema ulimuua?”
“Hapana! Nilisema tulimtupa baharini!”
“Ikawaje?”
“Bila shaka alikufa kwani mawimbi yalikuwa yakipiga makubwa mno, bahari ilichafuka,” alisema James huku akimwangalia mzee huyo.
“Niambie kitu kiimoja. Bruno alikufa au hakufa?” aliuliza mzee Jumanne.
“Nahisi alikufa!”
“Sikiliza. Sitaki uhisi. Niambie alikufa au hakufa?”
“Kwa kweli ni ngumu kujibu ila kwa jinsi mawimbi yalivyokuwa, alikufa,” alijibu James, yeye mwenye hakuonekana kujiamini hata kidogo.
Hilo likawa gumzo kijijini hapo, kila mtu alikuwa akiliongelea suala hilo kwamba iliwezekanaje Bruno yule waliyeambiwa kwamba alikufa baharini miezi sita iliyopita awe hai?
Kila mmoja akashikwa na hamu ya kumuona, walitaka kuamini baada ya kumuona lakini si kusikia kama walivyokuwa wamesikia. Alipokimbia Sharifa na Abdul, hakukuwa na mtu aliyepafahamu, wote walikuwa wakisikilizia kumuona mtu huyo, je, ni kweli alikuwa hai au mchezo tu uliokuwa umepangwa?
***
Bruno na mzee Todd walikuwa wakitembea kwa kasi kuelekea Upande wa Kaskazini, vichwa vyao vilikuwa vikifikiria maisha yao yangekuwaje nchini Afrika Kusini huku yeye, Todd akitafutwa dunia nzima kwa makosa ambayo hakuwahi kuyafanya.
Kichwa chake kilimfikiria mke wake na mtoto wake, aliwakumbuka, alitamani kuungana nao tena lakini kwa kipindi hicho haikuwezekana kabisa. Ukiachana na yeye, Bruno kichwa chake kilikuwa kikimfikiria mpenzi wake, Shakira tu.
Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea huko, alitamani kurudi haraka nchini Kenya ili kwenda kuonana naye kwa mara nyingine lakini hilo halikuwezekana kabisa. Hakujua ni kwa jinsi gani angeweza kurudi nchini humo na wakati mfukoni mwake hakuwa na pesa yoyote ile.
Hapo Cape Town walitembea kwa kujificha sana mpaka walipofika katika kituo cha treni za umeme cha Bellstar Junction. Hapo walitaka kupanda treni na kuondoka jijini Cape Town na kuelekea Johannesburg ambapo huko waliamini kwamba wangepata msaada wa kuondoka nchini humo.
Hawakuwa na pesa mfukoni lakini mzee Todd alikuwa na pesa nyingi katika akaunti yake. Aliogopa kwenda benki na kuchukua pesa kwani sura yake ilikuwa dili kila sehemu na watu walimtafuta kwa nguvu kubwa.
“Ninataka kuelekea benki kuchukua pesa, ila nahisi nitakamatwa. Unadhani unaweza kwenda kwa ajili yangu?” aliuliza Todd huku akimwangalia Bruno.
“Kwenda benki?”
“Ndiyo!”
“Sawa. Benki gani?” aliuliza.
“Barclays!”
“Haina shida.”
Alichomwambia ni kwamba alitakiwa kwanza kwenda huko kwa lengo la kuchukua karatasi ya kuandikia hundi (cheque) na yeye kuipeleka benki. Hilo halikuwa tatizo, akaelekea benki ambapo huko akakutana na dada mmoja wa Kizulu na kuanza kuongea naye.
Alizungumza naye huku akionekana kuwa mchangamfu mkubwa, alijua kumteka mtu kupitia mazungumzo yake kiasi kwamba msichana huyo aliyeitwa kwa jina la Susan akabaki akikenuua tu kwani kila neno alilolizungumza Bruno kwake liliukuna moyo wake.
“Umetoka wapi?” aliuliza Susan, hakuwahi kukutana na mwanaume aliyekuwa akiongea kama Bruno.
“Kenya!”
“Ooh! Kumbe Afrika Mashariki. Nawapenda watu wa huko, wanaongea sana, ni wachangamfu mno. Si ndiyo ilipo Tanzania?” aliuliza msichana huyo.
“Ndiyo!”
“Ninawapenda sana Afrika Mashariki!”
Hilo likampa uhakika wa kukamilisha kile alichokitaka. Akamwambia kwamba lengo la kufika mahali hapo lilikuwa ni kuchukua kitabu cha hundi. Hilo halikuwa tatizo, Susan akampa kitabu hicho na Bruno kuondoka mahali hapo.
Huko alipokwenda, alimfuatan mzee Todd na kumpa kile kitabu. Mzee huyo akakichukua na kuandika kiasi cha dola milioni moja apewe mkononi. Bruno alipokichukua kitabu hicho na kuangalia, hakuamini, alimwangalia vizuri mzee Todd, alihisi kama kiasi kile cha pesa alichoandikiwa kilikuwa ni uongo.
“Dola milioni moja?”
“Ndiyo! Hakikisha unakwenda na kufungua akaunti yako. Utazichukua hizi pesa na kuziingiza kwenye akautnti yako, tutakuwa tunazitumia kupitia akaunti yako,” alisema mzee huyo.
Bruno alichanganyikiwa mno, hakuamini alichokuwa akikisoma kwenye cheki ile. Kiasi kile, kwa pesa za shilingi ya Kenya kilikuwa ni sawa na bilioni moja, milioni mia mbili na senti kadhaa huku kwa shilingi ya Kitanzania ikiwa ni zaidi ya shilingi bilioni mbili.
Akaondoka mahali hapo na kumuacha mzee huyo akiwa sehemu amekaa kwa kujificha sana. Alipofika, kama kawaida yake akamfuata Susan na kuanza kuongea naye. Kitu cha kwanza alichohitaji kilikuwa ni kufungua akaunti.
“Una randi elfu ishirini?” aliuliza Susan.
“Ya nini?”
“Kufungulia akaunti!”
“Sina! Ila nitakuwa nazo baada ya kufungua akaunti!”
“Kivipi?”
Alichokifanya Bruno ni kumuonyeshea Susan ile hundi aliyokuwa ameandikiwa. Msichana huyo hakuamini, kilikuwa kiasi kikubwa cha pesa ambacho kilitakiwa kuingia mara baada ya kufunguliwa kwa akaunti hiyo.
Haraka sana Susan akampeleka sehemu ya kupiga picha, akafanya hivyo na kufuata taratibu zote na kiasi hicho cha pesa kumlipia yeye mwenyewe kwani aliamini kwamba angelipwa kwa fadhilla alizokuwa ameonyesha.
Mchakato ulipokamilika, hundi ile ikachukuliwa na pesa kutolewa katika akaunti ya mzee huyo na kuingizwa katika akauti ya Bruno, akatoa kiasi cha dola elfu ishirini na dola elfu moja na kumpa Susan kisha kuondoka zake.
Hilo likamfurahisha mzee Todd na kuona kwamba walikuwa wakienda kufanikiwa kile walichokuwa wakikitaka. Wakawa na pesa, walichokifanya ni kukata tiketi na safari ya kuelekea Johannesburg kuanza.
Njiani, mzee Todd alikuwa na kofia, hakutaka kugundulika na mtu yeyote yule kwani aliamini kwamba dunia nzima ilikuwa ikifahamu kama alikuwa akitafutwa. Treni hiyo ilichukua saa moja mpaka kufika katika Jiji la Johannesburg ambapo wakateremka na kufikiria kwenda kupumzika hotelini.
Kitu walichokifanya ni kununua simu. Kila mmoja akanunua yake pamoja na laini ambazo zilisajiliwa kwa jina la Bruno. Kila kitu kilipokamilika, kwa kuwa namba ya mke wake aliifahamu, akaanza kumpigia.
Simu haikuita muda mrefu ikapokelewa na mkewe. Sauti yake haikuwa ya kawaida, alikuwa akizungumza huku akilia. Alihitaji msaada kwani pale alipokuwa hakukuonekana kuwa salama kabisa.
Wakati akizungumza naye, mara simu akapokonywa na sauti ya mwanaume kusikika kutoka upande wa pili. Iliongea kibabe, sauti ambayo haikuonekana kuwa na mchezo hata kidogo.
“Tunakuhitaji ndani ya saa arobaini na nane. Mbali na hilo, utaziona maiti za familia yako ufukweni. Una saa arobaini na nane kujisalimisha kwetu,” alisema mwanaume huyo kwa sauti yenye utetemeshi.
“Wewe nani?”
“Si lazima unifahamu. Fanya kama nilivyokwambia,” alisema mwanaume huyo na kukata simu.
Mzee Todd akabaki akitetemeka, hakujua mwanaume huyo aliyekuwa akizungumza upande wa pili alikuwa nani. Akachoka, akatulia kwenye kiti huku akitetemeka kupita kawaida.
Hakujua ni kitu gani alitakiwa kufanya. Maneno aliyozungumza mwanaume huyo yalionyesha kabisa kwamba familia yake haikuwa salama huko ilipokuwa.
“Halo...halo...” aliita lakini hakukuwa na sauti iliyosikika upande wa pili.
Bruno alibaki akimwangalia mzee huyo, alikuwa akilia, machozi yalitiririka mashavuni mwake. Alionekana kuumizwa na kile kilichokuwa kimetokea. Aliipenda familia yake na mara kadhaa alikuwa akiizungumzia kwamba aliikumbuka na alitamani sana kuonana nayo.
Akamuuliza kilichokuwa kimetokea, akamwambia kwamba familia yake ilitekwa na mtu asiyemfahamu na alimuhitaji ndani ya saa arobaini na nane kitu ambacho kilikuwa ni vigumu kufanyika.
“Kwa hiyo?” aliuliza Bruno kwa sauti ya upole.
“Sijajua ni kitu gani kinatakiwa kufanyika. Familia yangu itauawa! Familia yangu itauawa!” alisema mzee Todd huku akilia kama mtoto.
***
Hakukuwa na mtu aliyekuwa muhumu kwa kipindi hicho kama mzee Todd. Maofisa wa CIA walikuwa wakimtafuta kila kona, walimtaka mzee huyo kwa udi na uvumba.
Walihangaika kila kona kumtafuta lakini hawakujua mahali alipokuwa. Wakati mwingine waliambiwa kwamba alikuwa nchini Msumbiji, walisafiri na kwenda huko lakini hawakufanikiwa kumpata.
Mzee huyo aliwasumbua kichwa kupita kawaida. Dunia ilikuwa kimya, kila mmoja alitaka kuiona nguvu ya Marekani kwamba kama ingeweza kumpata mwanaume huyo au la.
Walihangaika, kwenye simu hakuwa akipatakana na hata walipojaribu kuitraki simu yake hawakuambulia kitu chochote kile. Walisumbuka kwa muda wa wiki nzima ndipo siku moja wakafanikiwa kuiona simu ya mke wake ikiita, ilikuwa ikipigiwa na simu kutoka nchini Afrika Kusini.
Waliifuatilia simu ya mkewe bila yeye mwenye kugundua. Walijua kwamba ilikuwa ni lazima kwa mzee huyo kuwasiliana na familia yake na ndiyo maana walikuwa makini sana kuhakikisha wanakamata mawasiliano kutoka kwa watu hao.
Simu iliyopigwa katika simu ya mwanamke huyo ilitoka Afrika Kusini walichokifanya ni kuiunganisha na kuanza kusikiliza mazungumzo ya watu hao. Maneno waliyoyasikia yaliwashangaza, Juddie alisikika akilia huku akiomba msaada kuonyesha kwamba alikuwa kwenye hatari na baada ya hapo wakasikia sauti ya mwanaume ikimwambia kwamba alimpa saa arobaini na nane tu awe amejisalimisha.
Maofisa wa CIA hawakujua kilichokuwa kikiendelea, hawakujua ni kitu gani kilikuwa nyuma ya pazia. Ili kujua kile kilichokuwa kikiendelea ilikuwa ni lazima kumkamata Todd na kumuuliza kuhusu hayo yote yaliyotokea na huku wakiwa wameandaa kesi kwa lengo la kumpeleka mahakamani.
“Simu imetoka Afrika Kusini karibu na kituo cha treni cha Johannesburg Park. Waambie vijana waende huko, wamuwahi mzee huyo na kumtia mikononi mwao,” alisema mwanaume mmoja, haraka sana simu ikapigwa Afrika Kusini, maofisa wa CIA waliokuwa huko, wakawataarifu kwamba mahali walipokuwa hakukuwa mbali na kituo hicho, hivyo walikuwa wakienda haraka sana kuhakikisha mzee huyo anatiwa mikononi.
***
Johannesburg haikuonekana kuwa sehemu salama kwa maisha yao, ilikuwa ni lazima waondoke nchini humo huko Bruno akimwambia mzee Todd kwamba walitakiwa kuelekea nchini Kenya kwani alikuwa akizijua sehemu nyingi za kujificha ikiwemo kijijini kwake.
Hilo halikuwa tatizo, lakini kabla ya kuondoka kuelekea nchini humo ilikuwa ni lazima wapate mtu ambaye angewaunganishia na meli yoyote ile ili waondoke kuelekea Kenya. Kwa Bruno, kwake lilionekana kuwa suala kubwa na gumu kwani humo Afrika Kusini, hakuwa na ndugu, rafiki au mtu yeyote yule.
Walitamani kukutana na mtu yeyote ambaye angewaambia mahali pa kwenda kwani kwa jinsi mzee Todd alivyokuwa akitafutwa, walijua kabisa kwamba wasingeweza kupanda ndege, ilikuwa ni lazima kuondoka nchini humo kwa kutumia gari au meli.
“What should we do?” (Tufanye nini?) aliuliza mzee Todd.
“Let’s go to Soweto. I’m sure there are people who can help us out,” (Au twende Soweto, naamini huko kuna vijana wengi ambao wataweza kutusaidia,” alisema Bruno.
Hakuwahi kufika Soweto lakini alisikia tu kwamba huko kulikuwa ni uswahilini mno, kulikuwa na wahuni wengi ambao walikuwa wakipanga madili yao ya kuvamia benki na hata kufanya uchafu wa kila aina. Ilikuwa ni lazima kwenda huko kama tu walikuwa wakihitaji msaada wa kuondoka nchini humo.
Soweto ilikuwa ndani ya Johannesburg hivyo haikuwa vigumu kwao kufika huko. Kwa kuwa walikuwa na kofia, miwani hawakuhofia kumuuliza mtu yeyote mahali ilipokuwa Soweto. Walipouliza kwa mtu mmoja tu, akawaambia mahali kulipokuwa na kuanza kwenda huko.
Walikuwa na hofu, waliijua Soweto, kulikuwa na fujo za kila aina, watu walikuwa wakiuawa kila siku, haikuwa sehemu salama ya kuishi kwani watu wote waliokuwa wakiishi humo walikuwa waswahilini ambao waliamini zaidi katika fujo.
Baada ya dakika kadhaa, wakaingia Soweto. Sehemu hiyo haikutofautiana na sehemu nyingine za uswahilini. Kulikuwa na nyumba mbovu, barabara za vumbo na kitu pekee ambacho kilipendezesha mtaa huo ni uwanja wa timu ya Orlando Pirates.
Kila mtu alikuwa akiwaangalia jinsi walivyokuwa wakitembea mtaani. Walikuwa wakiangalia huku na kule, kwa kuwaangalia tu ilikuwa ni rahisi kugundua kwamba watu hao walikuwa wageni. Walitembea kwa kujishtukia huku muda mwingi wakiangalia huku na kule.
Walitembea mpaka walipokuta sehemu iliyokuwa imefungwa kamba kwa mbele. Hiyo ilikuwa ni kuingia ndani kabisa ya mtaa huo wa Soweto. Watu waliokuwa wakipita hapo walikuwa wale wa kitambo au wahuni ambao kutoa roho za watu ilikuwa ni sawa na kuua mbu.
Magari yote yaliyokuwa yakiibwa mjini, yalipitia hapo na kamba ile kufungwa. Hao ndiyo walikuwa chanzo cha mashirika ya umeme kuanzia mfumo wa luku kwa kuwa hawakuwa wakilipa na kila siku watu wa umeme waliokuwa wakienda huko walikuwa wakipigwa na wengine kuuawa.
Walisimama pale barabarani huku wakijifikiria kama iliwezekana kuvuka mahali pale au la. Kwa kupaangalia, palionekana kuwa pa kawaida, hakukuwa na mtu yeyote, barabara ya vumbi haikuwa hata na gari moja.
“Kuna kamba! Hii inamaanisha haturuhusiwi kuingia?” aliuliza Bruno, hakujua maana ya kamba ile.
“Nahisi kwa magari! Sisi tuingie,” alisema mzee Todd.
Hicho ndicho walichokifanya, wakaingia kwa kuivuka kamba ile, wakateembea kwa mwendo wa kawaida kusonga mbele huku kila mmoja akionekana kuogopa mno. Walipopiga kama hatua mia moja, mbele wakamuona mwanaume akijitokeza na kusimama barabarani.
Mkono wa kulia alishika panga huku wa kushoto akiwa na bunduki aina ya AK-47. Mwanaume huyo alivalia usongo kichwani kama Rambo huku akiwa na kaoshi na kipenzi kilichokuwa kimechanikachanika.
Wakasimama na kuanza kuangaliana na mwanaume yule. Kabla hawajachukua hatua yoyote ya kufanya, wakageuka nyuma, wanaume wengine waliokuwa na muonekano kama wa mwanaume yule aliyekuwa mbele yake wakatokea, walikuwa zaidi ya wanne.
Mpaka kufikia hapo, wakajua maana ya Mtaa wa Soweto. Walisikia tu kwamba ndani ya mtaa huo mauaji yalikuwa waziwazi, halikuwa jambo la kushangaza kuwaona watu wakipigwa au miili yao kutupwa barabarani kama mizoga.
“Hey! White! What are doing here?” (Hey! Mzungu! Unafanya nini hapa?) lilikuwa swali la kwanza alilouliza mmoja wa wanaume waliokuwa nyuma yao.
Hakukuwa na Mzungu aliyejaribu kwenda Soweto. Watu hao hawakupendwa huko kwa kuwa weusi waliamini kwamba walikuwa katili na ndiyo waliokuwa wakiwatesa watu weusi wengi nchini humo.
Kulikuwa na mapigano ya chini kwa chini baina ya Wazungu na watu weusi. Walitafutana kimya kimya, Wazungu walikuwa wakiokotwa wakiwa wamekufa na hata wakati mwingine nao watu weusi waliokotwa wakiwa wamekufa.
Hakukuwa na mtu aliyemaliza uhasama huu, ulikuwa ukiendelea huku kila mmoja akijiona kuwa sahihi na kusingekuwa na mtu yeyote wa kumbabaisha.
Soweto haikuwa na maendeleo makubwa na watu hao waliamini kwamba Wazungu ndiyo waliokuwa wakiinyima maendeleo kwani pamoja na kuwa katika jiji la biashara la Johannesburg lakini uswahilini bado kuliendelea kuwa Soweto.
Wazungu wengi waliwahusisha wanawake weusi katika biashara ya ngono. Walikuwa wakiwachukua na kuwapeleka katika madanguro ya Kizungu na hata cassino na kuanza kuwafanya walivyotaka.
Wanawake hao walitafuta pesa, walijua kwamba walikuwa wakijidhalilisha lakini hawakuwa na jinsi, kwa kuwa walikuwa wakaiingiza pesa, kwao
Kitendo cha mzee Todd kuonekana humo ilikuwa ni hatari kwa maisha yake, aliulizwa swali lakini hakuwa na jibu lolote lile. Wakawasogelea na kuanza kuwaangalia vizuri, waliporidhika, wakawachukua, wakawafunga kamba na kuanza kuondoka nao.
Wote wakajua huo ndiyo ulikuwa mwisho wao, walikuwa na hofu na kuona kwamba huo ungekuwa mwisho wao. Walipitishwa mitaani, kila mtu aliyekuwa akiwaangalia, alishangaa na zaidi kuliko yote walikuwa wkaimshangaa mzee Todd, ilikuwaje ajiamini aende Soweto na wakati Wazungu wote walikuwa wakiogopa kwenda huko?
Ni mwendo wa dakika tano tu wakafika katika jumba moja bovu na kuingizwa humo na kuamriwa watulie kwani kulikuwa na kiongozi wao aliyetakiwa kuwaona na kuwauliza maswali machache kabla ya kutoa uamuzi kwamba baada ya kuuawa huyo Mzungu, naye Bruno alitakiwa kuuawa au la.
“Do they want to kill us?” (wanataka kutuua?) aliuliza mzee Todd huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Yeah! They really want to kill us. Let’s get prepared,” (Ndiyo! Wanataka kutuua hasa. Tujiandae tu) alisema Bruno kwani kwa jinsi watu wale walivyokuwa wakionekana, walionyesha kila dalili za kutaka kuwamaliza watu hao.
Kitu walichokifanya ni kuwapokonya simu zao na kwenda kuzifungia ndani. Wakawapekua na kuwakuta na pesa, dola aambazo napo wakazichukua na kadi ya benki ambayo kwao ilikuwa muhimu kuliko kitu chochote kile.
“How much do you have?” (mna kiasi gani?) aliuliza mwanaume mmoja huku akiwa ameshika kadi ya ATM.
“We have nothing...” (hatuna kitu) alijibuu Bruno.
“You must be kidding me,” (utakuwa unanitania)
“Serious brother, we have nothing,” (siriazi kaka, hatuna kitu) alijibu Bruno, hakutaka kumuacha mzee Todd aongee kwani kwa hofu aliyokuwanayo ingekuwa rahisi kusema kiasi chote kilichokuwa kwenye akaunti na wakati yeye mwenyewe alikuwa akikitaka.
“Give me the password,” (nipeni namba ya siri) alisema mwanaume huyo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom