Hadi sasa, Mbunge wako ametekeleza ahadi yake ipi? Utamchagua tena 2020?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,280
25,858
  • Mbunge wako wa jimbo, ametekeleza ahadi yake ipi hadi sasa? Ni zile ahadi alizozitoa mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu wakati wa kampeni.
  • Kwa kutekeleza au kutotekeleza ahadi zake, utamchagua tena mwaka 2020 akigombea tena Ubunge?
Binafsi, bado nasubiri ahadi za Mbunge wangu wa Ubungo Saed Kubenea hasa zinazohusu sakata la UDA, kufutwa kwa Mahakama ya Jiji na kutaja Bungeni wachota pesa kutoka benki kwenye sakata la Escrow.

Kama ahadi hizi hatazitekeleza, na kama Kubenea atagombea tena mwaka 2020, sitamchagua. Akizitekeleza na kuahidi nzuri zaidi nitamwamini na kumchagua.

Vipi kuhusu wewe muungwana?
 
Mbunge wangu Mwigulu Nchemba.... hujaanza kutimiza ahadi zako Iramba! Nakusubiri kwa hamu 2020
 
  • Mbunge wako wa jimbo, ametekeleza ahadi yake ipi hadi sasa? Ni zile ahadi alizozitoa mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu wakati wa kampeni.
  • Kwa kutekeleza au kutotekeleza ahadi zake, utamchagua tena mwaka 2020 akigombea tena Ubunge?
Binafsi, bado nasubiri ahadi za Mbunge wangu wa Ubungo Saed Kubenea hasa zinazohusu sakata la UDA, kufutwa kwa Mahakama ya Jiji na kutaja Bungeni wachota pesa kutoka benki kwenye sakata la Escrow.

Kama ahadi hizi hatazitekeleza, na kama Kubenea atagombea tena mwaka 2020, sitamchagua. Akizitekeleza na kuahidi nzuri zaidi nitamwamini na kumchagua.

Vipi kuhusu wewe muungwana?

Hiyo ya UDA mbona RAIS wako kaisha idhinisha ufisadi wa UDA kwa kuwapa kabisa hisa siku ya ufunguzi wa Mwendokasi??

Kama ulidhania kuna vita ya ufisadi basi bado uko usingizini
 
Lwakatare jimbo limeshamcharaza na sie twamngoja, hatutaipa CCM ila Chadema wana nafasi wakibadirisha mtu
 
Mimi mmbunge wangu vedatus matayo anajitahidi kuleta maendeleo musoma hasa kwenye upande wa barabara kila sehemu ninayoipita naiona msoma mpya tofauti na vicent nyerere

Sema tu mmbunge wetu hachangii bungeni
 
Ufirauni wa tume kutulazimisha tujiandikishe vyuoni , uchaguzi likizo
 
mbunge wetu wa ubungo sijui yupo?bora hata diwani manota angekuwa ndo mbunge barabara anapitishaga greda hasa mitaa ya toroka uje!ila huyu mbunge sijui
 
Yaani, kwanza, baada ya uchaguzi hajawahi kurudi jimboni kwake.

Hadi jina lake tumelisahau.

Sasa tuje kwenye ahadi , mmmmmh: ahadi alizozitoa yeye mwenyewe (Mbunge) amezisahau hadi vitu alivyoahidi kavisahau.

Kwa kifupi, wabunge hawana faida tena, ni bora tu bunge livunjwe namaanisha nchi tusiwena bunge.
 
Mimi huwa nachagua tu kishabiki,maana ahadi zenyewe najua kabisa huwa hazatekelezeki ila mbunge wetu wa imalaseko kiboko,ni kazi kubugia kitwanga tu.2020 kama bado ntakuwepo na sijatekwa simpi kura ng'o.
 
  • Mbunge wako wa jimbo, ametekeleza ahadi yake ipi hadi sasa? Ni zile ahadi alizozitoa mwaka 2015 kwenye uchaguzi mkuu wakati wa kampeni.
  • Kwa kutekeleza au kutotekeleza ahadi zake, utamchagua tena mwaka 2020 akigombea tena Ubunge?
Binafsi, bado nasubiri ahadi za Mbunge wangu wa Ubungo Saed Kubenea hasa zinazohusu sakata la UDA, kufutwa kwa Mahakama ya Jiji na kutaja Bungeni wachota pesa kutoka benki kwenye sakata la Escrow.

Kama ahadi hizi hatazitekeleza, na kama Kubenea atagombea tena mwaka 2020, sitamchagua. Akizitekeleza na kuahidi nzuri zaidi nitamwamini na kumchagua.

Vipi kuhusu wewe muungwana?

Mimi Mbunge wa Jimbo langu la kufikia ni Tundu Lisu, kwa kweli sitaki hata kumuona na hii ni familia na marafiki zetu wote!
 
Huyu wa kwangu wa Ubungo kama amekata tamaa na ameamua aanze kula pensheni yake taratibu. Kama hayupo vile....Mbunge wangu sasahivi namuona Makonda tu maana anafanya kazi za kibunge kuliko Mbunge. Yani yuko karibu nasisi wananchi wa Ubungo kama vile anatuwakilisha Bungeni...

Mkimuona Mbunge wa Ubungo popote pale mwambieni tunayo matatizo mengi sana na ahadi zake bado hazijatatuliwa...
 
Bajeti.jpg
 
Mimi Mbunge wa Jimbo langu la kufikia ni Tundu Lisu, kwa kweli sitaki hata kumuona na hii ni familia na marafiki zetu wote!
Nasikia hataki kuwahamasisha wananchi kujiletea maendeleo...anasema wananchi waisubiri Serikali itawaletea kilakitu kwakuwa wanalipa kodi. Ila mmeanza kumchoka mwe!!! Hasa tangu awe raisi wa nchi gani ile inaitwa tieloesi sasa ntu rais ila bado anataka kuwa mbunge mbona ana kazi nyingi hivyo mwe!!!
 
Back
Top Bottom