Hadi lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hadi lini?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by MR NDEE, Nov 21, 2011.

 1. M

  MR NDEE Member

  #1
  Nov 21, 2011
  Joined: Aug 2, 2011
  Messages: 54
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Ninasema kwa yakini,Ya kweli ya mitaani
  Mejitokeza machoni,Sononeko li moyoni
  Hawa walio shakani,Lini tatoka tabuni
  Mjizigo tumboni,Mateso yao moyoni

  Starehe watupatia,Na wana watuzalia
  Na ngumi twawapatia,Pekee wajililia
  Ulemavu jipatia, Na ndoa wazililia
  Mateso yao moyoni,Mijizigo matumboni

  Maneno ya kuhadaa,Katu hawatokataa
  Tena kwa yao ridhaa,Hapo kati utapata
  Utamuona bidhaa,Mimba utaikataa
  Mjizigo matumboni,Mateso yao moyoni

  Na wale macho mekundu,Ni wale vibibi vizee
  Wanao shikiwa mundu,Eti wachawi wazee
  Tena na vijana watundu,Mezaliwa na wazee

  Mijizigo matumboni,Mateso yao moyoni
   
Loading...