‘Hackers’ wazuia mashambulizi ya ISIS nchini Italia

‘Hackers’ wazuia mashambulizi ya ISIS nchini Italia

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,092
Reaction score
34,903

Magaidi wa ISIS

Rome, Italia
Kundi la wadukuzi wa mtandaoni (Online Hackers) linalojiita Anonymous, limefanikiwa kuzima shambulizi la kigaidi la kundi la ISIS baada ya kuvamia akaunti zao za mitandao ya kijamii kisha kuwataarifu polisi na wahusika wa eneo shambulio hilo lilipokuwa limepangwa kufanyika.

Kwa mujibu wa Anonymous, shambulio hilo lilipangwa kufanyika Jumatatu, Desemba 28, mwaka huu lakini wakafanikiwa kunasa taarifa za magaidi hao wakati wakipanga mipango yao kisha kuivuruga.

“Tumefanikiwa kuzima shambulio moja la kigaidi nchini Italia leo, tunaamini tutazuia mengine,” Anonymous waliliambia Gazeti la The Independent.

Anonymous walitangaza kuingia kwenye vita ya kimtandao na Kundi la ISIS baada ya mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea jijini Paris, Ufaransa na kusababisha vifo vya watu 130, mwezi Novemba.

Kundi hilo liliachia video yake mtandaoni likieleza kuwa litatumia teknolojia ya mawasiliano ya intaneti, kuwasaka wahusika wa shambulio hilo, kuvamia mawasiliano yao, kuzifunga akaunti za magaidi mtandaoni na kuwakamatisha kwa polisi kwa lengo la kuwavuruga ili waache kuua watu wasio na hatia.

Siku chache baadaye, Anonymous waliposti mitandaoni taarifa kwamba wamenasa mawasiliano ya siri ya ISIS wakipanga kufanya mashambulizi Marekani, Indonesia, Italia na Lebanon na wakafanikisha kuzima mashambulizi hayo.

“Lengo letu ni kuifanya dunia, au kundi fulani la watu kujua kwamba eneo fulani limewekwa kwenye ‘target’ ya kushambuliwa ili hata kama mtu anaamua kwenda, awe anajua mapema,” ulisomeka ujumbe kwenye akaunti ya Anonymous na kuongeza kuwa changamoto kubwa wanayoipata, ni watu kupuuza taarifa wanazozitoa.
“Hatuhitaji kuaminiwa, cha msingi ni kuhakikisha hakuna mtu mwingine anayeuawa na magaidi,” liliposti kundi hilo kwenye akaunti yao ya mtandao wa Twitter.chanzo.GBP
 
Hao jamaa wanaojiita anonymous ,ni akina nani hasa ,kati ya wachina,usa,UK,Russia,franch,naomba kujua zaidi kuhusu hawa jamaa
 
Haya sas hackers kwa mahackers kazi ipo
 
Magaidi akili zao ni ndogo! Mungu wao alishawanyima maarifa!
 
Hao wanaitwa Ethical Hackers
Hawa sio Ethical Hackers, ni hacktivists ambao wamehusika kwenye DDoS nyingi sana dhidi ya tovuti za serikali kadhaa. Wamehusika hata kuhack twitter accounts za watu mashuhuri. Japo hapa kwa kudukua mitandao ya kigaidi nawaunga mkono, kama wasemavyo Waingereza "The enemy of my enemy is my friend"
 
Hawa jamaa inawezekana ikawa CIA .. Ingekua ni kikundi cha wahuni tu wangekua washakamatwa zamani. You need to think out of the box. Hao ISIS wenywe hivi mnajua wanakua funded na nani? Nani anawapa silaha? Ukishapata majibu ya maswali hayo ndo utakua umeelewa kidogo point yangu.. Hii dunia imejaa siasa chafu na propaganda. Wahenga wanasema "ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya.."
 
Hiyo ndio intelijensia inayotakiwa na yenye faida. Sio intelijensia ya kovu kwa ukawa.
 
ISIS ni nani? Mbona tunachezeana akili tu? Mwizi ajiibia mwenyewe wapi inawezekana?
 
Hawa jamaa inawezekana ikawa CIA .. Ingekua ni kikundi cha wahuni tu wangekua washakamatwa zamani. You need to think out of the box. Hao ISIS wenywe hivi mnajua wanakua funded na nani? Nani anawapa silaha? Ukishapata majibu ya maswali hayo ndo utakua umeelewa kidogo point yangu.. Hii dunia imejaa siasa chafu na propaganda. Wahenga wanasema "ukitaka kumuua mbwa, mpe jina baya.."
Kikundi cha annonymous wamekamatwa wengi mbona, kwenye matukio tofauti. Huwa ni jamii ya hackers wengi bila uongozi mmoja, nia na madhumuni huwa ni kutumia udukuzi kwenye harakati za kuasidia jamii, japo kuna baadhi yao hupitiliza na kufanya maovu.
 
Hao jamaa wanaojiita anonymous ,ni akina nani hasa ,kati ya wachina,usa,UK,Russia,franch,naomba kujua zaidi kuhusu hawa jamaa
Hao ni Anonymous kwa tafsiri haswa ya hilo neno, hawajulikani.
 
Kwa hiyo isis wanapata misaada hule tunakokujua hadi ya teknolojia mfano za kuhacky ?
 
Mbali na kusaidia jamii na hii DDoS attack, hawa majamaa bado ni watu wa itikadi kali. Kadri IS ilivyo na fedha za kishenzi, Anonymous wataweza kuukwepa makachero wa IS?
 
Wazee wa CEH ....

Enzi hizo nawaza kuisoma kwa tutorials za YouTube ......kumbe sivyo!
Achana na professionals za watu
 
Mbali na kusaidia jamii na hii DDoS attack, hawa majamaa bado ni watu wa itikadi kali. Kadri IS ilivyo na fedha za kishenzi, Anonymous wataweza kuukwepa makachero wa IS?

Anonymous hupiga hata mitandao ya kiserikali, hivyo sio watu wa kutishwa na vikundi vya kigaidi. Hacker wa kweli huwa hafuati hela.
 
Back
Top Bottom