Habari za uhakika: Dozi ya Manure yakamilika

Habari za uhakika: Dozi ya Manure yakamilika

Nyakwec's Bro

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2012
Posts
820
Reaction score
174
MELWOOD,LIVERPOOL Habari za uhakika nilizozipata hivi punde zinasema kwamba dozi kwa ajili ya timu inayosumbuliwa na maradhi kadhaa ya manure imekamilika,na dozi hiyo itasaidia timu hii kuwa na amani na kubaki kusubiria tu kuona msimu ujao utakuwaje maana ndoto zao za kuwemo katika 4 bora ya ligi ya uingereza zitakuwa zimefutiliwa mbali.

Habari zaidi zinasema kocha amepokea maombi mengi ya watu wanaojiita kuwa mashabiki wa manure wamemtumia maombi kwamba atoe dozi ya kumuondoa kabisa kocha wao kibaruani kama alivyofanya kwa Spurz na timu zingine ambazo mnazifahamu lakini kocha huyo makini wa Liverpool BR amesema kwanza kwa kuangalia namna ambavyo wamekuwa na uhusiano mwema na Moyes tangu akiwa pale Everton ni jirani yake mwema kabisa na yeye hatokuwa tayari kum-over dozi.

Habari hizo kutoka hapa Melwood zinasema kwamba BR ameandaa dozi ya kuwekeana heshima mjini tu ya bao 4 ambayo itakuwa ni fair sana kwa Moyes na mashabiki wa Manure.

Zaidi amesema wachezaji wake wako fit na wanategeme kuongezeka hari na nguvu maada ya mastaa wake wawili waliokuwa majeruhi,Mamadouh Sakho na Lucas Leiva kuwa fit tena hivyo Kopites waendeleze tu shangwe.

Liverpool ndiyo timu pekee ambayo haijapoteza mchezo tangu mwaka huu wa 2014 uanze na ni timu ambayo huwa inakuwa na nguvu mpya katika mechi 10 za mwisho za ligi hivyo hakuna namna mashetani wekundu wanaweza kuzima lengo la timu hii msimu ujao kushiriki ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

source: Melwood news..
 

Attachments

  • br.jpg
    br.jpg
    20.8 KB · Views: 74
  • capt.jpg
    capt.jpg
    25.7 KB · Views: 79
  • ds15.jpg
    ds15.jpg
    14.3 KB · Views: 68
  • gp.jpg
    gp.jpg
    47.1 KB · Views: 70
Back
Top Bottom