barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,874
Hii ilikuwa huko Iringa,Refa msaidizi alipoamua kuwatandika vichwa wachezaji "jeuri" waliotaka kumpiga muamuzi wa kati kwa madai kuwa anapeleka mambo kwa upendeleo.
Wachezaji hawa wawili walikula vichwa mpaka kupata majeraha,huku mmoja akilia hadharani kama mtoto mdogo.
Refa msaidizi amepewa adhabu kwa kosa hili...hawa ni wachezaji wa Mshikamano FC waliotaka kuleta vurugu baada ya kufungwa na "Wanapaluhengo Lipuli FC".Marefa wa siku hizi sio wa mchezomchezo!!!