diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
MRADI wa ujenzi wa barabara ya mabasi yaendayo haraka, maarufu kama mwendokasi, awamu ya pili kutoka Gerezani hadi Mbagala Kuu jijini Dar es Salaam, unatarajiwa kuanza wakati wowote kuanzia sasa
Imeelezwa kuwa mbali na Gerezani-Mbagala Kuu, ujenzi huo utafanyika pia kwenye Barabara ya Kawawa kuanzia Magomeni, Barabara ya Chang'ombe kuanzia Mgulani hadi makutano ya Barabara ya Kilwa na eneo la Mgulani JKT. Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (Dart), Ronald Lwakatare, aliiambia Nipashe jana kuwa makandarasi wameshatia saini mkataba na Wakala wa Barabara (Tanroads) na mradi wa kwanza utahusisha kilomita 20.3 za barabara zitakazojengwa kwa Sh. bilioni 189.43. Alisema mradi mwingine ni wa karakana moja, vituo vikuu vya kusimamia mabasi na vituo vya barabara za kupishania magari utakaogharimu Sh. bilioni 48.82.
“Ujenzi unaanza wakati wowote kuanzia sasa baada ya magari ya abiria kupisha katika vituo tulivyowaelekeza. Miradi hii miwili inasimamiwa na makandarasi wawili, wa majengo utakamilika kwa miaka miwili na wa barabara utakamilika kwa miaka mitatu,” Lwakatare
Alibainisha kuwa tayari wameshalipa fidia kwa wananchi 105 wanaopaswa kupisha utekelezaji wa mradi huo. “Watu wanaotakiwa kupisha mradi wameshalipwa fedha zao karibu zote, hivyo sasa wanatakiwa kupisha ili kazi ianze kufanyika haraka," alisema Lwakatare.Aliwataka wananchi na watumiaji wote wa barabara zote zinazohusika na mradi huo kupisha utekelezaji mara moja. Vilevile, aliwataka wamiliki wa magari ya abiria, maarufu daladala, yanayoingia kituo cha Gerezani, kuondoa magari yao kabla ya kesho ili kupisha mradi huo.
Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) pia imetoa utaratibu utakaotumika kwa safari za daladala zilizokuwa zinatumia kituo hicho. Kwa mujibu wa taarifa ya Sumatra iliyotolewa na Dart, daladala zote zinazotumia Barabara ya Kilwa kuelekea Gerezani, zitatakiwa kwenda Kituo cha Machinga Complex kupitia Barabara ya Msimbazi, Uhuru na Shaurimoyo na kurudi yalikotoka kwa kutumia Barabara za Lindi na Shaurimoyo.
Pia magari yanayotumia barabara ya Chang’ombe kuelekea Gerezani yatakwenda Mtaa wa Lindi kupitia Barabara ya Shaurimoyo na Lindi na kurudi yalikotoka kupitia barabara ya Lindi na Shaurimoyo. Ilielezwa katika taarifa hiyo kuwa magari yote yanayotumia Barabara ya Nyerere na Uhuru kuelekea Gerezani, yatakwenda Mnazi Mmoja na kurudi yalikotokea kupitia barabara hizo.