Basi na kila atakayesoma ujumbe huu na amfikishie mwenzake ili nchi yote ikapate kusikia juu ya unabii huu, na wala asitokee hata mtu mmoja wa kupaza sauti ya kwamba hakusikia. Siku yaja, mafisadi na wazandiki watakapotaka kutumia utaratibu wao ule ule wa kujipatia ushindi kwa ulaghai, basi na iwe kwetu nafasi ya kuwakana mchana kweupe kwa kuwa hawayatendi wala hawayaishi wanayonena, nao wamejifanyia nchi hii kivuno chao, wala wasiwakumbuke wapiga kura wao.