Habari Njema kama ilivyoandikwa na Kompanero Mwanamapinduzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Habari Njema kama ilivyoandikwa na Kompanero Mwanamapinduzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Jul 30, 2010.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mwaka wa tano wa kutawala kwake Rais Jakaya Kikwete, Amani Karume alipokuwa Rais wa Zanzibar, na Ali Karume, ndugu yake, Balozi wa Nchi, na Mizengo Pinda Waziri Mkuu wa Tanzania, wakati wa Uspika wa Samuel Sitta na Anna Makinda, neno la kura likamfikia Kompanero, mwana wa Kamaradi, jijini. Akafika nchi yote iliyo karibu na maziwa makuu, akihamasisha uchaguzi uletao ondoleo la ufisadi, kama ilivyoandikwa katika juzuu la Mwanaharakati Mwanakijiji:

  Sauti ya mtu aliaye vijijini,
  Itengenezeni njia ya Dakta,
  Yanyoosheni mapito yake.
  Kila shimo litafukiwa,
  Na kila kifusi kitashushwa,
  Palipopotoka patakuwa pamesawazishwa,
  Na wote wenye macho watayaona mabadiliko ya kweli.

  Basi, aliuambia mkusanyiko wa wale waliomwendea ili awahamasishe, Enyi Wazao wa Kijani, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia safishasafisha itakayokuja? Basi, pigeni kura ipingayo ufisadi; wala msianze kusema mioyoni mwenu, tunaye baba, ndiye Nyerere; kwa maana nawaambia katika mashina haya Siasa yaweza kumwinulia Nyerere wanachama. Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya Chama, basi kila shina lisilozaa matunda bora hukatwa na kutupwa jalalani-jela. Makutano wakamwuliza, tufanye nini basi? Akawajibu akiwaambia, mwenye kadi mbili za kupiga kura arudishe moja kwa mhusika; na mwenye takrima afanye hivyo. Watoa rushwa nao wakaja kuhamasishwa, wakamwuliza, Mwanamapinduzi, tufanye nini sisi? Akawaambia, msitumie fedha zaidi kuliko mlivyoamuriwa kisheria. Polisi nao wakamwuliza, wakisema, Sisi tufanye nini? Akawaambia, msishurutishe kupiga kura, wala msishiriki kuiba kura, tena mtosheke na posho zenu.

  Basi, wananchi walipokuwa wakisubiri yatakayotokea, wote wakitafakari-tafakari mioyoni habari za Kompanero, kama labda yeye ndiye Dakta, Kompanero alijibu akawaambia wote, kweli mimi nawahamasisha kwa kanuni za uchaguzi; lakini yuaja mdau mwenye ushawishi kuliko mimi, ambaye sistahili kuulegeza mkanda wa gwanda lake, yeye atawahamisha kwa ilani ya uchaguzi na sera moto moto, ambaye fagio lake li mkononi mwake, naye ataisafisha nchi yake, na kuikusanya ngano serikalini mwake, bali makapi atayafunga kwa kifungo kisichoisha.

  Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahutubia watu. Lakini...
   
 2. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2010
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  [​IMG]
   
 3. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,172
  Trophy Points: 280
  Nimecheka mpaka basi..Haya ni maandiko matakatifu au ni maandiko ya wasifu kwa katiba yetu takatifu??? NICE one though!!!
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Yep mkubwa kama nabii vile, let your voice be heared by every fisadi!
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135

  Mzee haya maneno ni mazuri lakini kwa kuwa nakupenda nimeona nikushirikishe habari ambayo ameisema Yohana tena yakiwa ni maneno ya mwisho. Soma Ufunuo wa yohana 22, 18-19. Nakushauri utengeneze na bwana. Ushauri tu. Maneno yenyewe yanasema

  18 Mimi Yohane nawapa onyo wote wanaosikia maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki: mtuyeyote akiongeza chochote katika mambo haya, Mungu atamwongezea mabaa yaliyoandikwa katikakitabu hiki.

  19 Na mtu yeyote akipunguza chochote katika maneno ya unabii yaliyomo katika kitabu hiki, Munguanya sehemu yake katika ule mti wa uzima, na sehemu yake katika mji mtakatifu, ambavyokatika kitabu hiki.
  atamnyang` vimeelezwa
   
 6. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Unabii huu wa campanero utatimia pale tu waalimu wote wa Tanzania na wengine watakaosimamia masanduku ya kuhesabia kura mwezi October watakaposimama kidedea kuzuia wizi wa kura unaopangwa na chama cha mafisadi ili kupoka matakwa ya waliowengi nchini.
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa ng'ambo ya mto wa Detroit pembezoni ya Jengo la Makao Makuu ya kampuni ya GM nikiangalia ng'ambo ya jiji la Windsor lililoko Canada wakati wa majira ya baridi mwaka 2005. Nilikuwa nimefunga kwa muda wa siku saba mfululizo na mwili wangu ulikuwa umepoteza nguvu....


   
 8. K

  Keil JF-Expert Member

  #8
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hapa ndipo ambapo walimu na polisi ambapo huwa wananiacha hoi. Mishahara yao ni midogo, wakidai wanaambiwa hakuna hela, lakini hela za ufisadi ziko nje nje na wafanya biashara wakubwa wanakwepa kodi ya mabilioni ya shilingi na wengine hupewa misahama ya kodi na ilihali wanaenda kufanya biashara.

  JK akibanwa na TUCTA anasema hahitaji kura za wafanyakazi, lakini ajabu ni kwamba siku ya kupiga kura hawa hawa walimu wanaodai wananyanyaswa na serikali, na hawa hawa polisi wanaoishi kwenye full-suti za mabati na mishahara midogo ndiyo wanaisaidia CCM kuiba kura na kufanya udanganyifu kwenye fomu mbali mbali.

  Ninakubaliana nawe mkuu, siku hawa watu muhimu sana kwa CCM wakibadilika na kutenda haki, mazingira ya kazi yataboreshwa kwa kiasi kikubwa, hawatanyanyaswa tena na watatendewa haki. Ile keki ya taifa itagawiwa kwa uwiano mzuri na hakutakuwa na watu wa kukwepa kodi na hivyo revenue ya serikali itakuwa kubwa.
   
 9. Companero

  Companero Platinum Member

  #9
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Shalom, asante sana, nami nampenda Yesu kama wewe na nakifuatilia sana kitabu cha Ufunuo na kuitambua sana tahadhari hiyo ndio maana sijakufuru Neno hapo zaidi ya kuiga staili ya uandishi wa mpendwa Dakta Luka - kwa uchambuzi zaidi wa kitabu cha Ufunuo tembelea UFUNUO: Revelation of Hope
   
 10. Companero

  Companero Platinum Member

  #10
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Basi, aliuambia mkusanyiko wa wale waliomwendea ili awahamasishe, Enyi Wazao wa Kijani, ni nani aliyewaonya ninyi kuikimbia safishasafisha itakayokuja? Basi, pigeni kura ipingayo ufisadi; wala msianze kusema mioyoni mwenu, tunaye baba, ndiye Nyerere; kwa maana nawaambia katika mashina haya Siasa yaweza kumwinulia Nyerere wanachama. Na sasa hivi shoka limekwisha kuwekwa penye mashina ya Chama, basi kila shina lisilozaa matunda bora hukatwa na kutupwa jalalani-jela. Makutano wakamwuliza, tufanye nini basi? Akawajibu akiwaambia, mwenye kadi mbili za kupiga kura arudishe moja kwa mhusika; na mwenye takrima afanye hivyo. Watoa rushwa nao wakaja kuhamasishwa, wakamwuliza, Mwanamapinduzi, tufanye nini sisi? Akawaambia, msitumie fedha zaidi kuliko mlivyoamuriwa kisheria. Polisi nao wakamwuliza, wakisema, Sisi tufanye nini? Akawaambia, msishurutishe kupiga kura, wala msishiriki kuiba kura, tena mtosheke na posho zenu.

  Basi, wananchi walipokuwa wakisubiri yatakayotokea, wote wakitafakari-tafakari mioyoni habari za Kompanero, kama labda yeye ndiye Dakta, Kompanero alijibu akawaambia wote, kweli mimi nawahamasisha kwa kanuni za uchaguzi; lakini yuaja mdau mwenye ushawishi kuliko mimi, ambaye sistahili kuulegeza mkanda wa gwanda lake, yeye atawahamisha kwa ilani ya uchaguzi na sera moto moto, ambaye fagio lake li mkononi mwake, naye ataisafisha nchi yake, na kuikusanya ngano serikalini mwake, bali makapi atayafunga kwa kifungo kisichoisha.

  Basi, kwa maonyo mengine mengi aliwahutubia watu. Lakini...
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Duuhh........aisee hizo fasihi hapo juu...............hongereni wakuu................mi niko kijijini huku kazi ni ngumu kweli kweli kuwashawishi yale makutano kuwa kivuli cha ule mti mkubwa kitawafaidisha wote na sio wachache............na kazi iendelee
   
 12. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Companero,
  Hongera sana kwa unabii huu,

  Ninaimani utatimia mda si mrefu.

  Ombi: Uandike kwa kirefu unabii huu kwani wengine tungependa kuuprint then kusambaza sehemu mbalimbali km vile mashuleni, vijiweni, nk
   
 13. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Jamani,na ushauri wa kuhusiana na kampeni uanze,ile kama ya Obama!ile kampeni si mchezo,naomba tuwe na thread kama hiyo,na kama ipo mnijulishe....Hapa naona ni mambo ya sauti ya Nyikani?Nakubaliana na Companero,Shalom hakuna liloharibika mkuu.
   
 14. O

  Ogah JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Mushi..........wengine tulishaanza na tuna mategemeo............kusema ukweli kazi ya kuelewesha wananchi si lelemama....lakini ukiwa uko fit na kumbu kumbu za matukio mbali mbali yaliyo na yanayoturudisha nyuma kimaendeleo kama Taifa......na ukawaambia wananch ihow serious Dr. Slaa is............wanakubali na wanaelewa.....................sasa kuelew ani kitu kimoja na kupiga kura ni kitu kingine......hivyo elimisha kuhusu umuhimu wa kura yake na mabadailiko tunayotarajia.............ili ajue kabisa kuwa kura yake ndio silaha ya ufisadi..........
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Amani iwe nanyi
   
 16. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2010
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Wananchi ambao hawapigi kura ni wengi sana,na kwasababu ya umasikini basi ungetegemea wawe motivated kupiga kura na kufanya mabadiliko,nadhani ni vitisho vya ccm kuwa vurugu itatokea endapo upinzani utashinda....Sasa huwa najiuliza vurugu hiyo upinzani wailete ya nini na watakuwa wameshinda?hapo ni wazi wao ndo wataleta vurugu,na huo ni utawala wa kimabavu.

  Mkuu Ogah unajuwa ccm wanajuwa kutumia dhaifu za wananchi,niliudhika sana niliposikia tv ya Mengi ilihusika kwenye propaganda za kuonyesha vita vya wenyewe kwa wenyewe kipindi cha uchaguzi ili kuwatisha wananchi....Wananchi kwa uelewa wao wanadhani kuwa upinzani ukishinda basi polisi na jeshi vitaleta fujo,labda kwa wao kudhani kuwa vyombo hivyo ni vya ccm....Ndio maana nakubaliana na MKJJ kuwa Dr Slaa ni lazima a act ka president to come...Kujitambulisha na kuongea na vyombo hivyo usalama wakiwemo,ili kuondoa ile dhana kuwa upinzani ni uadui....Na Mengi naye aache hao mambo yake ya ku broadcast issues kwa manufaa ya mafisadi.
   
 17. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi mkuu, inabidi atembelee hata makambi yajeshi kuwaona wakuu wa kambi, kuongea na askali wa kawaida! atembelee hata magerezani, pote sehemu kama hizi atembelee ili aonyeshe tofauti kubwa ya yeye na mafisadi.

  Dr. nenda hata Amana pale ujionee wagonjwa wanavyolala chini , nenda polisi ongea nao hata Mwema aongee naye! Naimani kila mmoja atatimiza kazi yake safari kiukweli.
   
 18. Monstgala

  Monstgala JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2010
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 1,082
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hii imekaa safi sana mkuu
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Yaaani nina hakika akitokea msaani wa kuiba mistari hiii na kuibinafisha kumfagilia JK memo itaandikwa fasta apewe kazi pale BOT
   
 20. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #20
  Aug 1, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Ndipo watakaposema kuwa hakika alikuwa mwanamapinduzi wa kweli, dokta na mwana halisi wa tanzania. Wakati huo watakuwa wamechelewa kutokana na kupokea takrima na kukuta mlango wa masanduku ya kura umefungwa.

  Ndipo atakapowaambia, niliwaomba kura tuwang'oe mafisadi hamkunipa. Niliwapa ushahidi wa kila ovu walilotenda hamkuniamini. Nilifika milangoni mwa majimbo yenu nikabisha hodi hamkunifungulia. Niliwaambia saa ya ukombozi ni sasa mkasema sistahili hata kugusa gidamu za uongozi wa nchi. Niliwapenda upendo wa agape lakini mkanining'iniza kwa misumari ya kejeli na hoja chakavu juu ya msalaba wa uchaguzi.

  Sitapenda mlie na kusaga meno pindi mtakapogundua hamkuwa sahihi na ndio maana nawaletea haya maono mpate badili upepo wa fikra zenu ili kwa pamoja tuweze kufika nchi ya ahadi. Nchi ya asali na maziwa. Tanzania mpya yenye mwanzo mpya. Mwenye masikio na asikie
   
Loading...