Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,629
- 34,173
Wakuu Habari,
Kutokana na kuwa kumekuwa na utamaduni wa watanzania walio wengi kutopenda sana kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi yetu[Utalii wa ndani],wengi wetu wamekuwa hawaifahamu vizuri nchi yetu.
Mimi nitajaribu kuwaelezea kuhusu mkoa wa MARA kwa KIUTAMADUNI,SHUGHULI ZA KIUCHUMI,KIJAMII,MICHEZO,WATU,KISIASA na mambo mbalimbali yanayogusa MKOA huu.
Kwa wale wanoufahamu pia MKOA huu au wenyeji wa Mkoa huu wanaweza kusaidiana na mimi ili kushibisha uzi huu @Moderator au @Invisible watatusaidia kuweka mpangilio mzuri katika uzi huu.
N.B.Naomba ieleweke uzi huu hauna nia yoyote mbaya bali ni kujaribu kuonesha UZURI wa nchi yetu.
Ninazungumzia Mkoa wa MARA kwa kuwa ni mwenyeji wa mkoa huo.Pia kumekuwa na taswira zisizo SAHIHI miongono mwa watanzania kuhusiana na mkoa huu.
Twende pamoja,Itatumika lugha ya kiswahili na kiingereza itakapobidi.
==================================================
================================================
UTANGULIZI
Mkoa wa Mara ni kati ya mikoa 30 ya Tanzania. Musoma ndipo Makao makuu ya mkoa.
Mara imepakana na mikoa jirani ya Mwanza na Shinyanga upande wa kusini, Arusha upande wa kusini-mashariki, Kagera kwa njia ya Ziwa Nyanza (au Viktoria) na Kenya upande wa mashariki.
Idadi ya wakazi ilikuwa 1,743,830 wakati wa sensa ya 2012 , zaidi ya 1,368,602 wa sensa ya 2002. Makabila ni mengi kuliko mikoa yote ya Tanzania, kama vile Waluo, Wajita, Waruri, Wazanaki, Wakuria, Wakabwa, Wakiroba, Wasimbiti, Wangoreme, Wakwaya, Waikoma, Wanata, Waisenye, Waikizu, Wasizaki, Wasukuma and Wataturu.
Kuna wilaya za Bunda, Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama, Musoma mjini na Musoma vijijini.
Sehemu kubwa ya Hifadhi ya Wanyama ya Serengeti iko ndani ya Mkoa wa Mara.
Photo Credit:Wikipedia
THE BEAUTY OF MARA REGION
HOTELI KUBWA YA UTALII DUNIANI(SINGITA).
HOTEL YA KWANZA KWA UBORA DUNIANI IPO TANZANIA.
Hoteli ya Singita Grumeti Reserves, iliyopo Serengeti, Mara, Tanzania, inathibitisha kufuru ya utajiri uliopo Tanzania.
Singita ndiyo hoteli nambari moja duniani, ikichukua tuzo hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo. Tuzo hizo hutolewa kila mwaka na taasisi maarufu ya Marekani, US Travel + Leisure ambayo ‘hudili’ na viwango vya biashara ya utalii duniani.
Hoteli hiyo, inathibitisha kwamba thamani ya Tanzania ipo juu mno, ndiyo maana mwekezaji kutoka Afrika Kusini, Luke Bailes, aliamua kufanya uwekezaji wa hali ya juu ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Matokeo hayo, yaliandikwa Agosti mwaka huu kwenye jarida maarufu kwa kuchapisha matukio ya biashara za utalii, linaloitwa T+L Magazine. Jarida hilo linamilikiwa na Taasisi ya US Travel + Leisure.
Tangu kufunguliwa kwake, Singita Grumeti imekuwa kivutio cha viongozi, matajiri na watu maarufu ambao mara kwa mara hutinga kujivinjari, vilevile kujionea vivutio vya utalii vilivyopo nchini.
Kwa mujibu wa US Travel + Leisure, sababu ya kuipa Singita hadhi ya kuwa hoteli namba moja duniani, inatokana na muundo wake, huduma zinazotolewa, kuwa ndani ya mbuga kubwa kabisa ya wanyama duniani (Serengeti), vilevile wageni mashuhuri inaopokea.
Inaelezwa kwamba Singita Grumeti ndiyo hoteli inayoongoza kwa sasa duniani kwa kupokea wageni wenye hadhi ya daraja la kwanza, wakiwemo marais, matajiri, wanamichezo, wasanii, viongozi mbalimbali maarufu ulimwenguni na kadhalika.
HAWA WANATAJWA KUJIVINJARI SINGITA
Marais wa 42 na 43 nchini Marekani, Bill Clinton na George W. Bush, kwa nyakati tofauti wamefikia kwenye hoteli hiyo baada ya kuvutiwa na sifa zake zinazotikisa duniani.
Bilionea wa Kirusi anayemiliki Klabu ya Chelsea ya Uingereza, Roman Abramovich, alipotembelea nchini Septemba 2009, inaelezwa kwamba alilala kwenye hoteli hiyo.
Bilionea wa Kihindi, Mukesh Ambani ambaye kwa sasa ni tajiri namba 19 duniani, alifika nchini mwaka jana na kufikia kwenye hoteli hiyo.
Wakati alipowasili nchini, Mekesh alikuwa tajiri namba nne duniani. Ripoti ya mwaka 2011, ilimtaja kuwa tajiri namba tisa na sasa anashika nafasi ya 19.
Mke wa zamani wa mwanasoka anayechezea Chelsea ya England, Ashley Cole, Cheryl, alipofika nchini miaka miwili iliyopita, inaelezwa pia kwamba alifikia kwenye hoteli hiyo.
Mwanamitindo aliye pia mcheza sinema maarufu wa Hollywood, Marekani, Angelina Jolie na mumewe Brad Pitt, waliripotiwa kufika nchini na moja kwa moja makazi yao yakawa Singita Grumeti.
Wengine ambao wanatajwa kuwahi kupumzika kwenye hoteli hiyo ni mwanamuziki wa Marekani, Sean Carter ‘Jay Z’, mwanasoka Thierry Henry, Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa orodha ya wageni wanaofikia Singita ni kubwa mno, tatizo hufanywa siri kwa sababu watu wengi mashuhuri ulimwenguni huwa hawapendi ijulikane kama wamefikia kwenye hoteli hiyo kwa sababu za kiusalama.
SIFA ZA HOTELI HIYO
Ni hoteli yenye eneo kubwa, kutoka ‘loji’ moja hadi nyingine, inabidi utumie usafiri maalum.
Imegawanywa kwenye ‘loji’ mbili, moja inaitwa Ebony na nyingine ni Boulder.
Hoteli hiyo, pia inaundwa na ‘loji’ nyingine inayoitwa Castleton Camp ambayo inaweza kuhamishwa kutoka sehemu moja hadi nyingine.
Bei ya chini kabisa kwa mtu kulala kwenye hoteli hiyo ni shilingi 2,000,000 na bei hiyo hutegemea na msimu.
Bei zimetofautiana kati ya ‘loji’ moja hadi nyingine na mtu kulala kwenye Castleton Camp, inaweza kugharimu mpaka shilingi milioni 23 kwa siku moja.
Courtesy:Mo dewjiblog

Last edited by a moderator: