Habari kuhusu Taasisi ya kukusanya Mapato (TRA)

Come27

JF-Expert Member
Dec 1, 2012
7,694
7,370
Naomba serikali ijalibu kutusaidia kuwaondoa vishoka na matapeli wote waliopo waliopo katika office za TRA, wamejaa sana kiasi kwamba ukifika pale kidogo ukiulizia office yoyote pale mapokezi anatokea mtu anajifanya kama anataka kukusaidia, sasa apo atakupa michanganuo ya kukupiga pesa ivi ni kweli kabisa TRA mmeshindwa kuweka michanganuo ya kodi fulani inatakiwa ilipweje, naomba mtu saidie maana watu wengi katika huduma zenu tunashindwa kuzipata kutokana na office zenu kuzungukwa na vishoka na matapeli pale njee na mule ndani katika kolido zote. Kuna watu wengi wanshinda kuanzia asubuhi mpaka jioni.
Kingine cha mwisho ukifnikiwa kufika sehemu husika uwezi kupata huduma utaambiwa mtandao aupo. Lakini wakifika vishoka na matapeli wanaacha zile fomu zao wanafanyiwa kazi, wafanyakazi wote waliopo TRA office wanajua kwamba pale kuna vishoka na matapeli.
Na ndio maana watu wengi wanshindwa kupata huduma.
Leo nimeenda pale TRA office nimekaa siku nzima akuna cha huduma wanadai mtandao aupo, ivi kweli kwa mwendo huu watu wengi wataweza kulipa kodi kweli
 
Kingine cha mwisho ukifnikiwa kufika sehemu husika uwezi kupata huduma utaambiwa mtandao aupo. Lakini wakifika vishoka na matapeli wanaacha zile fomu zao wanafanyiwa kazi, wafanyakazi wote waliopo TRA office wanajua


Yaani ni shida tu! Kishoka mmoja anaweza kuja na mafaili utadhani amehamishia ofisi nzima hapo TRA. Mtu mmoja fomu 20. Unasubiri mpaka basi na hii kauli ya mtandao hakuna muda mwingine ni mbinu chafu ya kuwakatisha wateja tamaa ili waondoke. Na bado maana kama malipo mengi yataelekezwa TRA na huku hawajajipanga ni shida. Nashauri kuwa ni vizuri maofisa wa TRA wakasambazwa halmashauri ili wa take over system ya malipo ya Halmashuri kwa muda kwa zile Kodi zilizokuwa zikilipwa huko na sasa ziende TRA.

Hili la vishoka na maajenti wa clearing &Fowarding-TRA tengenezeni dirisha special kwa ajili ya hawa maajenti huko mtawakagua vizuri. nasie wateja tunaokuja in person inabidi kitambuliusho mbele kama tai ilikuondoa huu uhuni.

cc. Moderator
 
TRA shaurimoyo wamezodi kwa kua na utaratibu mbovo.Wateja wanasota zaidi ya wiki kupata tax clearence na hoduma nyingine.Wekeni utaratibu mzuri watu wapate huduma kwa muda na warudi kufanya shughuli nyingine za uzalishaji.
 
Leo nimeenda pale TRA office Tazara. Awana mtandao tokea Jana. Duh ila TRA office wanafanya mchakato wa kulipa kodi uwe mgumu sana. Ivi kweli mtandao aupo siku mbili kweli. Au ndio njaama za kufanya serikali inakosa mapato
 
Ingekuwa post ya siasa watu wengi wangechangia lakini ishu za Msingi uoni watu wengi
 
Back
Top Bottom