Mimi ni mpenzi mkubwa wa kwenda gym, nimejaribu kuulizia Gymkhana, nimeambiwa kuwa pale wana vifaa vyote vya mazoezi na kuna michezo mingi sana, nikataka kujuwa taratibu za kuwa member nikaambiwa bei zao ziko juu ukilinganisha na sehemu nyingine, lakini hilo sio tatizo kwangu. Nilichokwama ni kuwa nimeambiwa kupata u member pale ni ngumu kwa sababu vigogo wengi serekalini wanafanya mazoezi pale.Ningepeda kuwauliza wana jf hizi habari zina ukweli wowote? Kuna mtu anayeweza kujuwa namna ya kujiunga gymkhana? naomba atusaidie