Gwaride la Sherehe za Uhuru zitakuwepo?

Gwaride la Sherehe za Uhuru zitakuwepo?

K A B U R U

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Posts
922
Reaction score
1,257
Mwaka jana 2015, sherehe za Uhuru na Muungano zilisitishwa na pesa zikaelekezwa kwenye maeneo ambayo wananchi wengi wanafaidika nayo. Maamuzi hayo yaliungwa mkono na wengi, ingawa hayakueleza kama yatakuwa endelevu kwa miaka inayofuata. Sasa naomba wadau wenye taarifa za kuwepo au kutokuwepo kwa maazimisho hayo kwa mwaka huu 2016 watujuze.
 
sherehe za mwaka huu zitaadhimishwa kwa watanzania kuonyesha bidhaa zinazotoka kwenye viwanda vyetu vya ndani
 
Litakuwepo, pia baada ya miaka mingi kupita kamisheni ya maofisa itafanyika Dar tarehe 26 mwezi huu badala ya monduli. Good morning.
 
Nashukuru kwa taarifa hizo, ingawa nami naomba niongezee hapo kwenye majibu ya baadhi ya wadau kuwa, kiswahili sahihi ni maonesho badala ya maonyesho.
Neno maonesho limetoholewa kutoka neno ONA wakati neno maonyesho limetoholewa kutoka neno ONYA.
 
Back
Top Bottom