Askofu mkuu wa kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima, amemtembelea ili kumjulia hali na Kumwombea Ndugu, Yusuf Manji aliyelazwa hospitalini kwa matibabu. Hii inafuatia baada ya mfanyabiashara huyo kutajwa na Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam (Paul Makonda) kwenye orodha ya watuhumiwa wa sakata la madawa ya kulevya.