Gwajima alaani umwagaji wa damu unaoendelea nchini

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Mchungaji Gwajima kwenye Ibaada yake ya Jumapili hii, akifundisha somo aliloliita LAANA YA DAMU, amekemea kwa ukali Umwagaji wa Damu wa aina yoyote akisema kila Damu inapomwagika huwa inapiga kelele za Laana, kama haikumwagika kwa Haki. Akiendelea mbele amesema Kitendo cha Polisi kumwaga Damu za wananchi wasio na Hatia kwenye matukio mbalimbali ya kijamii na kisiasa Inaleta Laana si kwa Jeshi la Polisi peke yake Bali pia Laana kwa Nchi.

Ameendelea zaidi na Kufundisha kwamba Laana Hii ingawa imetendwa na kikundi cha watu wachache lakini nchi nzima huathirika na madhara hayo.

Amendelea kusema kwamba Laana ya Damu huwaletea watu Roho ya mafundo ambayo humfunga mtu kwenye maamuzi.

Akasema kiwango cha mafanikio cha mtu kinategemea na Uwezo wake wa kufanya maamuzi Magumu kwenye maisha yake ambayo yatamletea Maisha Bora. Akasema Utamwona mtu anasita sita kila siku kuchukua hatua ya maamuzi kwenye maisha yake, utamkutamtu ana chumba kimoja alichopanga, anaoa ndani ya chumba hicho kimoja, anazaa ndani ya chumba hicho hicho kimoja, mtoto wake anaoa au kuolewa akiwa ndani ya chumba hicho hicho kimoja cha kupanga na anafia hapo. Mtu huyo alishalogwa kwa kufungwa mafundo kwa sababu ya Laana za Damu.

Utamwona mtu ana wajihi na elimu ya kutosha kwenye ajira Fulani, na zaidi ya hayo amebakia kwenye ajira ambayo kipato chakeni kidogo sana, anaona udahili kwenye gazeti wa kazi bora kwa elimu yake na ujira mzuri, anashindwa kuchukua hatua ya kuisaili kazi hiyo. Ukimuuliza mdomoni kwake ana majibu mengi tu, utaskia "hizo kazi lazima uwe na refa..",mara kazi hiyo haina "secutity"', na mengi mengineyo. Mtu huyu alishalogwa kwa Kifungo cha mafundo kwa sababu ya Laana za Damu, labda mtu atajiuliza kwanini nilogwe, mchawi hana sababu, watu flan waliona umeva shati zuri wakaona wivu na hiyo ni sababu tosha ya kukupelekea hata njiwa kwa mganga, njiwa anachinjwa kwa jina lako naDamu inamwagika na kisha unafungwa.

Akaendelea kusema kuna mtu aliomba usaili wa kazi, kumbe hakuwa anajua kwamba wenzakewamamfunga kifungo cha mdomo, alipofika mbele ya usaili hakuweza kusemachochote , kila swali akiulizwa ingawa analifahamu lakini anapanic na kujibutofauti, na kila kazi alizoomba alikuwa akipoteza.

Damu hiiya binaadamu wasio na hatia, inayomwagwa na Jeshi la Polisi, akielezea Tukio laKuuwawa kwa Mwandishi wa Habari Iringa, ni baya na yeye analilaani Vikali kwasababu linaleta laana Kubwa sana kwa nchi yetu.

Katika Ibaada Hiyo ambayo tukio la ajabu sana Limetokea la Kufufuliwa kwa Binti wa mama mmoja anayeitwa Modesta mkazi wa Vetenari ambaye bint yake aliyefahamika kwa jina la Joice, aliyefariki na kufikishwa hapo kanisani kwa maombezi na kufufuliwa madhabahuni.. Tukio hilo la ajabu nalitafutia kwa ushahidi wa picha za mnato na video na nadhani nitaliweka jamvini kwa wale wataopenda. Kama hupendi unaacha.
 
Back
Top Bottom