Wacha wamtimulie mbali huyu bwana mdogo Kabila. Amekuwa legelege mno kwani hata kujiimarishia ulinzi wake mwenyewe pale Kinshasa (wachilia mbali huko mashariki Goma) pia anashindwa. Yaani yupo pale DRC kama mtawala TX hivi (yaani kama dezaini ya mwakilishi wa malkia au mfalme hivi kama Governor Twinning vile🙂.
Wacongoman wanadai kazi kubwa ya kabila na familia yake ni kui fisadi nchi na kuhamishia kila kitu nje ya nchi kama vile siku moja atakuwa hayupo kabisa. Wanasema moyoni hana maslahi ya DRC. Wenyewe Wacongo wanadai pesa na investment yake kubwa anaifanyia Tanzania.