Green Guard na mavazi ya kijeshi

Green Guard na mavazi ya kijeshi

Noor Hassan

Member
Joined
Mar 26, 2013
Posts
17
Reaction score
5
Niliwahi kupost kwenye
mitandao ya facebook
kuhusu hatari ya raia
kuvaa nguo
zinazofanana na sare za
jeshi.
Post ambayo ninaamini
ilileta mabadiliko
makubwa kwani baada
ya muda tuliona wa2u
wakikamatwa na
kuonywa wasizivae .
Pengeni unaweza
kujiuliza ni kwa nini
niliandika mada
hiyo .moja ya sababu ni
kutokana na baadhi ya
wa2u kujihusisha na
vitendo vya ujambazi
huku wakiwa wamevaa
sare za jeshi,ktk post
yangu ya leo ninataka
kuzungumzia suala la
vijana wa ccm ambao
inadaiwa ni askari wa
chama hicho na
waliobatizwa jina la '
green guard ' ,hawa
wanavaa mikanda
inayovaliwa na askari
wa jwtz pamoja na
mabuti .
Nimekuwa nikijiuliza
kwa muda mrefu kuhusu
uvaaji wa vijana hawa
ambao wanajiita askari
wa chama hicho. Kwa
kuruhusiwa kuvaa
mavazi ya kijeshi huku
serikali
ikiwaangalia .hawa
green guard wamekuwa
wakivaa mikanda ya
kijeshi na mabuti hata
mbele ya viongozi / polisi
ambao wanajua kuwa ni
makosa kwa raia kuvaa
sare yoyote ya kijeshi na
hilo ni kosa la jinai
lakini hawachukuliwi
hatua yoyote.
Ktk uchaguzi wa kata 4
za udiwani jijini arusha
green guard walikuwa
wakitumia mikanda hiyo
kuwapiga wananchi na
hata waliposhtakiwa
hawakuchukuliwa
hatua .pengine
watanzania wanataka
kufahamu kama hilo
nalo ni jeshi
linalotambulika
kisheria na kama
limepata baraka za
kufanya kazi hiyo ni
ibara gani ya katiba ya
tanzania ?
Kama sio jeshi kwa nini
liruhusiwe kuvaa
mikanda ya jeshi ?
Wakati green guard
wanaruhusiwa kuvaa
mikanda ya jeshi wapo
askari wa halali
wanavaa viatu
vilivyoshonwa ,mikanda
iliyochanika lakini hawa
green guard leo hii
wana mikanda ,buti
mpya sijui kati ya hawa
anastahili kuvaa sare
hizo.
Mimi leo nataka
wanajeshi wanijibu
kuwa tangu lini
wameanza kuvaliana
nguo na green guard au
ni kwa vile wao wako
ktk chama tawala .
Ninajiuliza kama
wangekuwa ni vijana wa
chadema wamevaa
mikanda na buti za
kijeshi wangeachwa ?
Jwtz wanapaswa
kuwaeleza wananchi
kuhusu uhalali wa
vijana hawa wa ccm
kuvaa sare hizi na ni
nani aliwapa mikanda
ma viatu hivyo ?
Mkuu wa majeshi
atuambie kuwa green
guard ni la nani ?
Linawajibika kwa nani ?
Kama jeshi letu haliwezi
kuwanyang'anya vijana
hawa mikanda na viatu
basi tufahamu kuwa
wao ndio
wanaowasaidia kuwapa
mikanda na viatu hivyo
tanzania ni nchi yenye
amani na inatawaliwa
kwa majeshi
yanayotambuliwa na
katiba ya jamhuri ya
muungano wa tanzania
nisingependa kuona
kundi la chama fulani
linajifanya kuwa ndilo
jeshi na linawatishia
wananchi kwa kushiriki
vitendo vya
kuwanyanyasa
 
dogoo unafahamu mavazi ya jeshi kama combat unazovaa wewe tutaita mavazi ya jeshi ndugu yangu wewe mwenyewe umecheza gwaride ulikuwa ukivaa nguo za kijani ambazo ni sare ya chama sasa hivi unavaa rangi ya kaki ila najua ngombe akipotea zizi lazima jioni atarudi pamoja anko
 
Back
Top Bottom