Nitaenda kwa mada husika. Nimekuwa nikipokea jumbe nyingi kwa account yangu ya gmail ukitaka kunipongeza kuwa nimeshinda Green Card ya Marekani nyingine mara Umepata nafasi ya ajira Canada mara Australia.
Nikijaribu kufuatilia na kujiandikisha, kuna fees. Je, hizi email sio fake na Je uhalali wake jinsi ya kuomba ni kwa njia ipi. Msaada wakuu kwa anayejua.
Mkuu nimekupata.Ni ajabu kushinda bila kushiriki au kuomba. Nafikiri ni jumbe zinazokuja kama hizi za mitandao ya simu kwamba hongera umeshinda labda muda wa maongezi au umechagiliwa kushiriki shindano fulani.