Green Cards za Marekani

Sim Card

JF-Expert Member
Dec 30, 2019
882
1,592
Wandugu heri ya mwaka mpya.

Nitaenda kwa mada husika. Nimekuwa nikipokea jumbe nyingi kwa account yangu ya gmail ukitaka kunipongeza kuwa nimeshinda Green Card ya Marekani nyingine mara Umepata nafasi ya ajira Canada mara Australia.

Nikijaribu kufuatilia na kujiandikisha, kuna fees. Je, hizi email sio fake na Je uhalali wake jinsi ya kuomba ni kwa njia ipi. Msaada wakuu kwa anayejua.
 
Green Card haina fees kwa hatua za awali.

Pili, sehemu ya kutuma maombi ni moja tu kwingine unaweza pata hao vishoka.

Mwisho, as long as Trump order is still at large, wabongo hawana chance kwa sasa kuomba maombi mapya ya hiyo kitu.
 
Weka screenshots za E-mail account hizo. Halafu unashindaje bila kuomba au kushiriki hayo mashindano???!!!
Mkuu nimekupata.Ni ajabu kushinda bila kushiriki au kuomba. Nafikiri ni jumbe zinazokuja kama hizi za mitandao ya simu kwamba hongera umeshinda labda muda wa maongezi au umechagiliwa kushiriki shindano fulani.
 
Tz kwa sasa haimo kwenye green card ya Marekani, nafikiri unajua.
 
KUNA KICHWA KITALIWA PESA MUDA SIO MREFU NA WATU WA AFRIKA MAGHARIBI
 
Kama ulishiriki kutuma maombi mwezi October 2020 basi subiri majibu katika acc yako mwezi may 2021..... Hao ni wapopo wapo kazini kuwa makini....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom