FENtastic
JF-Expert Member
- Aug 4, 2015
- 6,780
- 10,553
Leo makala yetu inajikita katika wizi huu ambao haujawahi kutokea nchini Marekani, mnamo mwaka 1950 na kuitwa wizi wa karne kutokana na namna wizi huo ulivyofanyika kiakili na kiasi kikubwa cha fedha kilichoibwa. Ni wizi ulioamsha hisia za Wamarekani kila kona nchini humo, kuangalia jinsi wezi hao walivyotekeleza wizi huo na FBI walivyokuwa wanasuasua katika chunguzi zao kulizidi kuvuta hisia zaidi.
J. Edgar Hoover, mkurugenzi mbabe na katili wa FBI ambaye hajawahi kutokea katika nchi ya Marekani ndiye aliyekuwa madarakani kwa kipindi hicho nahii ni moja ya kesi iliyomsumbua sana kichwa chake kwa kutaka kumshushia sifa zake kwa jamii ya Wamarekani. Huyu jamaa ndiye mkurugenzi wa kwanza wa FBI na alihudumu kwa takribani miaka 48 (Mei 5, 1924 mpaka Mei 2, 1972). Miaka ya nyuma kabla ya wizi huu kulikuwa na wasumbufu wa kuiba kwenye mabenki mbalimbali kama akina Baby Face Nelson- huyu alitamba miaka ya 1930 na alipewa jina hilo kutokana na sura yake ya kitoto na umbo lake dogo, Machine Gun Kelly, Pretty Boy Floyd- huyu nae alisumbua miaka ya 1930 mpaka alipoangushwa na FBI wakiongozwa na agent Melvin Purvis mnamo mwaka 1934 na wengineo wengi ambao walikuwa wakijulikana kama “Public Enemies No.01”.
Sasa Hoover aliweza kupambana na hawa jamaa vizuri bila kujua mbeleni huko atakutana na akina Joseph “Big Joe” McGinnis ambao nao watamuumiza kichwa chake vibaya mno. Ukiona FBI wanaweka jina lako katika orodha ya Public Enemies No.01 ujue umeshindikana kabisa, na huhitaji hata kukaa jela zaidi ya kupotezwa kwenye uso wa dunia.
Tuangalie Kuzaliwa kwa Wazo hili
Kabla hatujaangalia kuzaliwa kwa wazo, tufahamu kwanza Brink ni nini. Brink ni kampuni ya ulinzi na usalama wa mali za watu binafsi, kampuni mbalimbali, benki na serikali. Ilianzishwa mnamo mwaka 1859 na Perry Brink, makao yake makuu yakiwa 1801 Bayberry Court Richmond, VA 232226 Virginia. Hii ni moja ya kampuni bora kabisa inayoaminika sana nchini Marekani kutokana na kuwa na mifumo bora nay a kisasa ya ulinzi wa mali, na yote hayo pia wanapokea na kusafirisha fedha nyingi za benki huku ikiwa imeshika kasi zaidi ya nchi 100 duniani, wafanyakazi 134k, vifaa mbalimbali vya utendaji kazi 1,100 na magari 13,300.
Kutokana na ukubwa wa kampuni hii na fedha nyingi inazozihifadhi imepelekea kuwavutia wezi bila kujalisha usalama na ulinzi wa kampuni hii. Kuna matukio mawili makubwa ya wizi yaliyowahi kufanyika kwenye kampuni hiyo huku tukio la kwanza ndilo tunalolizungumzia hapa na la pili lilitokea mwaka 1983 lilijulikana kama Brink’s-Mat Robbery. Mengine yalikuwa ya kuiba kwenye magari yao ya kusafirisha hela kama la mwaka 1993 huko New York, mwaka 2008 “D .B. Tuber’s” Brinks Roberry- hili nililizungumzia kwenye makala iliyopita, mwaka 2013 huko Brussels Airport ambapo almasi zenye thamani ya €38m zilipigwa na ya mwisho mnamo mwaka 2014 kuna jamaa mmoja kwa majina Joe Cornell alishuhudia gari ya Brink ikidondosha fuko la hela lenye $125k huko Fresno California na kama msamaria mwema aliliokota fuko hilo na kuwarudishia akisema alioona ndio kitu sahihi cha kufanya na wakamzawadia $5k na $5k zilipelekwa Salvation Army anapofanya kazi kwa jina lake.
Turudi kwenye kuzaliwa kwa wazo, mnamo mwaka 1948 kuna jamaa mmoja kwa majina Joseph McGinnis aka Big Joe alikuwa ni mhalifu mashuhuri tu mwenye rekodi za uvunjifu wa sharia jijini Boston huko Massachusetts, huyu jamaa ameshawahi kwenda gerezani mara kadhaa kwa makossa mbalimbali kama umiliki wa silaha kimagendo, wizi wa vurugu hadi mabosi wengi wa jijini hapo walikuwa wameshamzoea na wengine ni washkaji kabisa. Katika historia yake hajawahi kufanya wizi wa kutisha zaidi ya huu tunaoenda kuuona. Wakati anatoka jela mara ya mwisho mwaka 1948 alikutana na jamaa mmoja kwa majina Joseph “Specs” O’Keefe ambaye huyu naye ni mhalifu wa muda mrefu jijini Boston, wawili hawa walikutana kwa mara ya kwanza gerezani na ndipo walipounda urafiki wao na kuja kupotezana baada ya kila mmoja kupatikana na kifungo chake ila mwaka 1948 walikuja kukutana tena ndipo wazo la wizi likazaliwa kwa Big Joe kumwambia O’Keefe wazo lake hilo huku akimsikiliza kwa makini na kulidadavua juu juu maana bado halikuwa kwenye mchoro rasmi (plan) na alichohitaji ni ushirikiano wake maana yeye ni mtaalamu wa kuchezea milango na kengele (alarm system).
Wezi huwa wanajuana wenyewe kuwa mwenzake ni bora kwenye nini na linapokuja wazo lazima aangalie nani anafaa zaidi kwa maana hiyo yeye kukutana na O’Keefe lilikuwa jambo jema sana. Baada ya O’Keefe kuhadithiwa mpango huo akawakumbuka marafiki zake wawili yaani Anthony Pino na Stanley “Gus” Gusciora. Hawa jamaa wawili walikuwa wahalifu wazuri tu jijini Boston na wakawa wamevutwa katika mchoro huu kwa sababu wana uzoefu mkubwa katika wizi na ni wataalamu wa kucheza na alarm sytem pia.
Mpaka hapo wakawa wametimia wanne nao wakakutanishwa na mastermind Big Joe na kuwaeleza wazo lake ambalo awali alikuwa ameshamueleza O’Keefe. Sasa tuangalie mchoro wa wizi baada ya timu kupanuka na kufika wanne na ndipo mchoro ukaanza kutengenezwa, ulianza kwa wazo la Big Joe ambaye alipendekeza wafanye wizi katika kampuni ya Brink ambayo ipo katika jiji lao la Boston nay eye aliona ni sehemu sahihi na inaweza kuingilika. Pia kingine kilichomshawishi Big Joe ni fedha nyingi kuhifadhiwa ndani ya jengo hilo ilipo Brink kwa ajili ya kusafirishwa maeneo mbalimbali pale zinapohitajika na wahusika.
Hizi taarifa Big Joe alizipata kupitia kwa mfanyakazi wa kampuni hiyo ya Brink ambaye alikuwa naye kifungoni kwenye gereza moja kwa kosa la wizi na alipohadithiwa jinsi Brink ilivyo alivutiwa nayo na akaiweka kiporo. Sasa wakaanza kujadiliana mchoro wao utakavyokuwa na walibishana mara kadhaa kuwa eidha waibe fedha zilizohifadhiwa humo ndani ama waibe kwenye gari wakati zinasafirishwa na cha kuchekesha mmoja aliyetoa wazo la kuvamia gari akapendekeza kabisa wavizie kipindi cha mshahara lakini lilionekana wazo hatari sana kuliko kuvamia ndani ya Brink.
Stanley Gus kusikia hivyo akadakia basi kazi imeshaisha kwani nitaenda kufukua silaha zangu, huyu jamaa ni maarufu jijini Boston kwa kuuza silaha za magendo. Big Joe akamkatisha Stanley kwa kumwambia wizi huu hauhitaji matumizi ya nguvu bali ni wa akili nyingi kwani anajua fika athari za kutumia silaha kwani wanaweza kufeli ama kufaulu ila wakaishia kujeruhi au kupoteza maisha ya watu na kuvikasirisha zaidi vyombo vya dola.
Big Joe alitaka tukio lisilohusisha umwagaji wa damu kwani alipata dondoo za jengo hilo kutoka kwa yule ex-staff wa Brink aliyekuwa naye gerezani na aliwapa mchoro ambao iliwabidi wafuatilie na kuusanifu vyema. Baadaye waliachana huku kila mmoja akiumiza kichwa chake katika utengenezaji wa plan ya pamoja ili wakikutana tena waweze kuunganisha mawazo na mchoro kukamilika. Pia Big Joe alisisitiza suala la kutojihusisha na uvunjifu wowote ule wa sharia kwa kipindi hicho ni muhimu ili wasijetupwa korokoroni na kupunguza nguvu kazi yao, maana hawa usipowatahadharisha faster wanaweza kuzingua na kutupwa nyuma ya nondo.
Wakati wakiwa wamepeana timeline ya kuja na plan ya pamoja, bahati mbaya Brink ikahama mjengoni pale! Ina maana vyote Big Joe alivyoelekezwa kule jela havina maana tena. Nuksi iliyoje! Na hatua zote alizowapa wenzake hazina maana tena kwasababu vyote viliangaza wakati Brink ikiwa katika eneo hilo la zamani, maanake yake ni kila kitu kuanza upya tena na ugumu wa wizi huo unakuwa maradufu ikizingatiwa ilipohamia Brink ni jengo la kisasa lenye mifumo ya maana ya ulinzi hasa kwenye alarm system tofauti na jengo hilo la zamani n ahata wale wataalamu wa mifumo ya kengele hapo hawakuwa na jipya tena ikabidi kubaki kuilamu teknolojia tu.
Big Joe ndio alikuwa wa kwanza kujua Brink inahama na kuita wenzake kukutana tena, maana kila walichokubaliana awali kitabadilika yote hayo ni juu ya Brink kuhama. Hivyo wito huo ni kwa ajili ya kupanga mikakati mipya. Agenda ilikuwa ni namna gani wataweza kuiba, basi kwa pamoja wakakubaliana waongeze kikosi na Anthony akakabidhiwa jukumu la kuongeza watu ili kuweza kukidhi mahitaji ya wizi huo, Pino akaanza kupitia orodha ya wahalifu anaowafahamu na wazoefu.
Wahalifu aliowakumbuka na kuamini wanaweza kuingia kwenye mchoro huo walikuwa ni shemeji yake Pino Vincent Costa, Michael Vincent "Vinnie" Geagan, Thomas "Sandy" Francis Richardson, Adolf H. "Jazz" Maffei, Henry Conan D., James "Guillemets" Faherty na Joseph Banfield. Hao wezi wapo saba ukijumlisha na wale wanne wa awali jumla wanakuwa kumi na moja.
Sasa hapa kikosi kazi kikamilika kwa ajili ya kwenda kuweka historia jijini Boston na Marekani kwa ujumla na wote kwa pamoja walikutana kupanga mikakati ya wizi huu. Sababu ya kwanini mchoro huu ulichukua muda mrefu takribani miezi 18 ndipo ukakamilika inahitaji moyo kuvumilia huo muda na nidhamu ya hali ya juu kwa wezi hao ili wasije wakatupwa jela kwa makosa mengineyo ya uvunjifu sheria na kukwamisha mpango wao wa wizi.
Mastermind Big Joe alikuwa akiwasikiliza kwa umakini mkubwa wataalamu wa kucheza na kengele ili kuona ni jinsi gani watakabiliana na na teknolojia hiyo ya kisasa, basi O'Keefe akasema inabidi upatikane mchoro mzima wa kengele wa hilo jengo jipya la Brink. Sasa wanaupataje huo mchoro? Mtihani unaanzia hapo, na hata wakiupata kazi itakuwa kuusoma na kuufanyia mazoezi ili wauelewe vizuri. Big Joe akamwambia O'Keefe lazima huo mchoro ukaibwe kutoka kwa waliousanifu na kuweka kwenye hilo jengo jipya! Wezi wote wakapumua kwanza na wakaona huo wizi balaa maana hapo ni wizi ndani ya wizi.
Bila ya kufanywa wizi wa mfumo wa kengele hakuna kitakachofanikiwa, na je, wakikamatwa ndiyo itakuwa mwisho wa kila kitu? Ilikuwa ni changamoto ila hakuna namna ya kukimbia huo msala kama kweli wanataka wizi wao ufanikiwe na kubidi Big Joe na O'Keefe watengeneze mchoro wa kampuni iliyofunga mfumo wa kengele kwenye jengo jipya la Brink, katika mchoro huo ilitakiwa O'Keefe na wa wezi wengine ndio watakaoenda kuiba mfumo huo na ilifanyika hivyo.
Baada ya mchoro kuandaliwa, kuingia haikuwa kazi ngumu sana O'Keefe na mwenzake walizama ndani ya kampuni hiyo usiku mwingi na kupekua mafaili mbalimbali mpaka wakakutana na mchoro wenyewe na kuanza kuukariri na ndio maana walienda wawili ambao wana kichwa chepesi na chenye kunasa na kuelewa mambo upesi yaani walimeza mchoro bila kuondoka nao, kwani ilionekana itakuwa hatari endapo wataondoka nao kisha kampuni kugundua mchoro huo umeibiwa na wangeshtuka ya kuwa kuna tukio linaloenda kutokea kwa mteja wao huyo hivyo wangetoa taarifa/tahadhari mapema na wizi wao ungefeli.
Baada ya kumeza mchoro huo sasa ikabidi uhamishiwe kwenye makaratasi na kuanza kupitiwa kwa pamoja na wataalamu hao wa kucheza na kengele waligundua kulikuwa na mabadiliko kidogo tofauti na walivyokuwa wakifikiria hivyo hata wangefeli kuupata mchoro huo isingewaathiri sana kwenye wizi wao.
Sasa kazi inayofuata ni kusoma jengo la Brink jinsi linavyoendeshwa siku zote za wiki, wafanyakazi wake, ulinzi na njia za kufikia vault yake na mengineyo. Hapa palichukua muda sana maana waliweka kambi kabisa pembezoni mwa jengo hilo kwa kazi moja tu ya kusoma kila hatua na walikuwa wakipeana zamu mchana na usiku.
Baada ya kipindi kirefu cha kulisoma jengo hilo, wakatambua mambo muhimu ya kuwasaidia kama ifuatavyo;
Mosi, ghorofa ya pili ndipo kunakohifadhiwa fedha zote na ndipo kuna vault. Hapa ni tofauti na jengo la zamani ambapo vault ilikuwa chini kabisa yaani underground kwa hiyo suala la kuchimba na kutokea kwenye vault halipo ila kwa jengo la zamani plan zilikuwa hivyo na teyari mfumo wa kengele walikuwa wanaujua hivyo kilikuwa ni kitendo cha kuchimba na kutegeua mfumo wa kengele na kuingia ndani kiulaini kabisa. Hii ndiyo sababu iliyofanya Brink wahame hapo ili kuongeza usalama wa mali za wateja wao.
Pili, njia ya kufika mpaka ghorofa ya pili ambapo ndipo kwe ye vault kulikuwa na changamoto kidogo, kwani njia yake mpaka unafika inabidi uvuke milango sita na ukitegemea aina ya wizi wao inakuwa kitendawili kwani wanataka wizi usiotumia nguvu na vurugu za hapa na pale hivyo hawawezi kuvunja hiyo milango mpaka kufika wanapotaka kwani wakifanya hivyo basi watawashtua walinzi hivyo basi inawalazimu kutumia akili nyingi kufikia watakapo lakini kwa vile walijipanga vilivyo na nia wanayo basi hakuna lisilowezekana chini ya jua.
Tatu, ratiba ya wafanyakazi wa Brink hasa wale walioko kwenye eneo la fedha waligundua wafanyakazi wake ni wanaume watupu hivyo swaga za kutumia ulaghai wa mapenzi hapo hakuna na kati ya wafanyakazi hao kuna ambao wanakuwa na silaha ndogo (bastola) kiunoni mwao kwa ajili ya usalama humo ndani na wanakuwepo hasa mida ya usiki mpaka asubuhi. Waligundua pia ulinzi nyakati za jioni mpaka muda wa chakula cha jioni ulinzi unakuwa umelegea kidogo tofauti na saa zingine katika kampuni hiyo pia ndipo kuna harakati chache za wafanyakazi wa Brink kwasababu wengi wao ndio wanakuwa wameenda makwao na kubaki wafanyakazi wachache tu ambao wengi wao ni wale wa chumba cha kuhifadhia fedha.
Nne, muda ambao fedha zinahesabiwa ni nyakati za jioni na kupangiwa ratiba kulingana na mahitaji ya wateja wao, kisha wale wafanyakazi wanaoingia mchana wanakuwa na kazi ya kuzipakia kwenye magari kwa ajili ya kuzisafirisha. Ina maana muda ambao fedha zinahesabiwa na kupangiwa route zake kwa mujibu wa wateja wao ndio muda ambao vault inafunguliwa na mara baada ya zoezi hilo kuiisha vault inafungwa hivyo basi maamuzi ni juu yao kuwa ni muda upi ni sahihi zaidi kwao.
Tano, ilitakiwa kuwepo na usafiri kwa ajili ya fedha watakazoiba na ilipangwa kuwa gari iibwe karibia na siku ya wizi wao na ifichwe bila kutumika kwa shughuli yoyote ile mpaka siku ya wizi maana litakuwa limetafutwa na vyombo vya usalama na kuripotiwa na mmiliki wake kuwa ameibiwa gari.
Sita, kuvaa nguo zinazofanana na za wafanyakazi wa Brink, hapa wanataka wafanane na wafanyakazi hao siku ya tukio ila wao wataongezea gloves na vinyago vya kuficha uhusika wao.
Saba, fedha watakazoziiba hawatazitumia mpaka ipite miaka sita! Hii ilileta vuta nikuvute kwasababu waliopendekeza hivi ni Big Joe na Pino wakati wengine wanataka wakiiba wagawane kila mtu na fungu lake ila walisisitiza lazima iwe hivyo kwani baada ya miaka sita kupita kwa mujibu wa sheria za nchini humo hawawezi tena kufunguliwa mashtaka kutokana na wizi huo ndani ya Brink. Ila wengine waliona nongwa kuvumilia kwani unaweza kudanja na wengine wakafaidi fungu lako ama pengine kupigwa pingu huku hujafaidi chochote!
Nane, waliruhusu wachache wao wabebe silaha ndogo (bastola) kwa ajili ya dharura na itatumika endapo watakutana na mazingira magumu sana ambayo yatahatarisha maisha ama wizi wao.
Tisa, kutengeneza mazingira ya ushahidi wa uongo kuelekea kwenye tukio hili, hii ilikuwa muhimu sana kwasababu wao ni wezi wazoefu na wanajulikana sana na vyombo vya usalama maana tukio likishatokea lazima watasumbuliwa wezi wote wa jijini Boston na hivi ndivyo inavyokuwa pale wizi mkubwa unapotekea. Wapelelezi huwa wanaanza kuwahoji wale manguli wa wizi eneo ambalo wizi huo umetokea kwa kutaka kujua siku ya tukio ratiba zao nzima na ikionekana kuna dalili zozote za kuhusika basi watasaidia uchunguzi hata kama siyo wao. Imani yao ni kuwa wanaweza kuwa wanajua waliohusika na wizi huo ni wakinani ila wezi hawa walijipanga kwa hilu kwasababu ni wazoefu na wanajua mbinu zitumikazo na FBI katika chunguzi zao.
Baada ya kuona mambo muhimu yanayozunguka wizi huu mzima sasa ni muda wa wezi kuingia mzigoni ila kabla ya hapi ilihitajika kufanyika namna ya kufumbua milango ile ili waweze kufika kwenye vault. Pino alitoa maelekezo ya namna watakavyotatua suala hilo alisema, inabidi kwanza atafutwe mchonga funguo ambaye itabidi wampange kuwa awachongee funguo nyakati za usiku mwingi hivyo asilale na watamlipa zaidi ya gharama halisi ya kazi hiyo. Wakati huo wao wanawaza namna ya kuvamia Brink usiku na kwenda kukusanya mfumo wa vitasa vya milango hiyo ili wampe mchonga funguo.
FBI walisema kitendo hicho cha kwenda kuiba mifumo ya milango ilikuwa ndiyo hatari zaidi katika wizi wao maana ilikuwa raisi kushtukiwa ila iliwabidi kutumia akili na ujanja wa hali ya juu kujifanya ni wafanyakazi wa Brink ili wasishtukiwe na walinzi na muda mwingine walihitaji kuingia usiku sana ambapo hakuna wafanyakazi ili kufanikisha zoezi hilo kwasababu walikuwa wanafanya kwa siku tofauti zoezi hilo kwa milango yote mitano na kukwama kwenye mlango wa mwisho.
Wezi hao walikuwa wakiingia na mfumo wao wa mlango kwa kuchomoa original na kuweka wa kwao halafu wanapeleka kwa fundi wao wa funguo ili kuweza kutumia huo mfumo kutengeneza funguo bandia halafu kabla hapajakucha wanarudisha mfumo original na kuondoka na ule wao wa geresha. Japokuwa ilikuwa kazi hatari mno kufanya hayo yote ila hawakushtukiwa na kumaliza milango yote mitamo na kubaki huo mmoja wa kuruhusu wao kuingia kwenye vault kwani ulikuwa tofauti na hiyo mingine ila baadaye walifanikiwa kuushughulikia.
Huyu mchonga funguo hakuwa sehemu ya wezi hao, alikuwa akifanya tu kazi bila kujua anasaidia wizi flani kufanyika ingawa FBI walimng'ang'ania sana mwanzoni kabla ya uchunguzi haujakolea na kutoa majibu sahihi. Mpaka hapo wakawa wameshamaliza hatua zote za kuelekea huo wizi na kilichobakia ni kuiba gari la kwenda kufanyia wizi huo. Ilifanyika hivyo kwa wao mwezi mmoja kabla kwenda kuiba gari aina ya lori.
Tuangalie sasa utekelezaji wa wizi huu:
Mwisho wa maandalizi yote ya wizi huu ulikuwa umeshawadia mwaka 1950, na ukipiga mahesabu toka wazo linazaliwa hadi kufikia hapo takribani miaka miwili imepita halafu bado unaambiwa tena wanatakiwa kukaa miaka sita bila kutumia hata senti. Tarehe ya wizi huu ilipangwa kuwa Januari 17, 1950 kwa gari mbili kuwepo huku gari ya kwanza itakuwa na wezi tisa na ya pili itakuwa na wezi wawili na ndiyo ile iliyoibwa na ndio itakayobeba fedha hizo wanazotarajia kuiba.
Siku ilipowadia gari mbili zilifika eneo la tukio ila gari ya kwanza kufika ilikuwa ile yenye wezi wawili ndai yake ambao waliwahi kufika ili waangalie usalama wa eneo upoje na walikuwa na jukumu la kuwashtua wenzao kuwa muda wa tukio umewadia. Gari hii ilifika saa mbili kabla ya tukio kufanyika ambapo ilikuwa saa kamii na moja jioni na walichagua muda huu baada ya kuona ndio muda ulinzi unalegea kwenye kampuni ya Brink na wanatakiwa ndani ya nusu saa wawe wameshakamilisha wizi wao kwani ulinzi unakuwa umeshaanza kuimarika.
Inamaana ni nusu saa pekee ilionekana ulinzi unakuwa legelege maana ndio muda wa kupata msosi wa jioni na story kadhaa. Saa moja kasoro usiku gari ya pili ilisogea maaeneo ya karibu na Brink na walikuwa wanawasikilizia wenzao wawape ishara ili waanze uvamizi na ilipofika saa moja kasoro dakika tano wakawashtua kuwa teyari ulinzi umeshapwaya na wanaweza kuja kukinukisha.
ITAENDELEA...Sehemu ya Mwisho #90