agiza china, na ufunge mwenyewe bei rahisi tu
GPS device si inahitaji utaalamu kufunga ndugu au mtu yoyote anaweza kufunga? Je kuagiza toka China gharama zake ni kiasi ghani?agiza china, na ufunge mwenyewe bei rahisi tu
Nimetafuta bila mafanikio ndio maana nimekuja hapa mkuu, ikiwa una taarifa zao ni vyema ukashare nasi.wapo wengi mjini tafuta mtandaoni taarifa zao.
Ahsante kwa ushauri wako Mzuri, Mimi nahitaji kwaajili ya hizi bajaj zangu na si kwaajili ya biashara.Amini hichi nilichowaambia ni gharama nafuu kuliko mtu akufungie, kwanza ufungaji wake ni rahisi tu, pia unachagua wewe ni GPS ya aina gani inafaa kwa mahitaji yako kwa kuna aina nyingi sana na bidhaa zetu nyingi za hapa wanaagiza vitu cheap, sisi tunaagiza mzigo kila wiki, sio GPS ni vitu vingine kabisa ila ni device zinazofanana na hizo vitu, gharama iko chini kama unaagiza mzigo mkubwa, mfano kama ungekuwa unaagiza kwa ajili ya biashara ingekulipa vizuri, mimi siwezi kukusaidia ila naamini wapo watu humu muda si mrefu watakuja na mawazo mazuri zaidi ya haya...mkuu ukifanikiwa agiza za pikipiki za kawaida utapiga hela.
Siyo muda wote unatakiwa hewani ila mda unataka kutrack Ndiyo utatumia net. Ila ukiweka laini ya halotel inasoma sehemu zoteHoi itasaidia hata kwa wenye boda, nisaidie jinsi ya kuagiza na zenye ubora maana wawezapata ila muda wote inataka intermet connection sasa kwa network yetu hapa nchini maeneoengi chenga
Sijaelewa hiyo app itaweza vipi kuitracking hii simu ambayo inakuwa imefungwa kwenye pikipiki mkuu.Ebu fanya haya..
Nunua simu ndogo yenye network eg tecno yenye battery 3000.. kisha download apps ya GPS install ktk simu hiyo na simu nyingine yako..
Kisha, funga hiyo simu ktk bodaboda kwa kuificha, hasa chini ya speedometer ni pazuri, na charging yake una connect kwa USB cable mwizi hatajua haraka akidhania ni music cable tu huku simu umeificha, kila ukiwasha boda boda simu inachaji na inakuwa on kila saa..
Sasa boda boda kokote ikienda, utaiona ktk simu yako hiyo nyingine.. just like marafiki wanavyofanya..
Fanya hivyo fasta..
Sijaelewa hiyo app itaweza vipi kuitracking hii simu ambayo inakuwa imefungwa kwenye pikipiki mkuu.
Ili aweze kuta-track kwa kutumia simu si ni lazima simu iwe na internet connection muda wote? Sasa kama mwizi akiiba hiyo bajaji na muda wa internet ukiisha utaongezaje? Au unaweza kuongeza remotlly?Na ww mgumu sana kuelewa.. haya do this..
Ingia Google play store, download hii apps..
GPS PHONE TRACKER
Kisha unaweka ktk simu zako mbili tofauti, hakikisha una network ktk simu zote..
Simu ikiwa on, itakwambia simu nyingine iko wapi in real time.. na sbb inachajiwa na bodaboda haitazima, utakuwa unaiona inaenda wapi kwa haraka kabisa na mtaa iliyoko hiyo simu, iliyofunga kwenye boda, so utaikamata bodaboda ikiibiwa tu.. haraka kabisa.. accuracy hadi 100feet, hapo unakamata mwizi fasta..
Umeelewa..?