Google yashitakiwa, wajuzi tuelemisheni

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,540
7,452
Kama heading yangu hapo juu mimi binafsi sijaelewa kosa aliloshitakiwa hapo Google, hebu wajuzi nifafanulieni hapo

=========================

GOOGLE YASHITAKIWA KWA SABABU YA ANDROID

Muungano wa Ulaya EU umeifungulia rasmi mashtaka ya kujihusisha na vitendo vinavyozuia ushindani wa kibiashara kampuni ya kuhusiana na jinsi kampuni hiyo ya teknolojia inavyotangaza mfumo endeshi wa simu wa android.

Kamishna wa ushindani wa kibiashara katika umoja wa ulaya, Margrethe Vestager ameishutumu Google kwa kuvunja sheria za EU kwa kuwanyima wateja uhuru wa kuchagua na kukandamiza ubunifu.

Google huenda ikapigwa faini kubwa na pia mabadiliko makubwa kufanyiwa mfumo wake wa kibiashara ikiwa itashindwa katika kesi hiyo.

Mfumo wa android kwa sasa unatumika katika asilimia 80 ya simu za kisasa aina ya smartphone zinazouzwa duniani kote.

Tume hiyo ya nchi za Ulaya inaishutumu kampuni ya Google kwa kutumia vibaya ubabe huo.

Bi Vestager amesema kutokana na uchunguzi uliofanywa, Google imekuwa na tabia ya kuwanyima watumiaji wake uhuru wa kuchagua programu endeshi, yaani app, na pia huduma nyingine, na inaathiri ubunifu wa mashirika mengine.

Tume imeguswa kuona kwamba kifaa cha kutafuta cha Google Search Engine ndicho kinachowekwa katika mfumo wa simu zinazotumia android ambazo zinauzwa barani Ulaya.
Imesema, jinsi Google wanavyofanya biashara, na mikataba inayoingia na kampuni zinazotengeza simu kuhakikisha simu nyingi zinauzwa zikiwa na mfumo endeshi wa android, inadhamiria kuzuia washindani wake kuingia sokoni.

Hii ni kesi kubwa ya pili ambayo Tume ya Umoja wa Ulaya imeibua dhidi ya kampuni ya Google.

Kampuni hiyo tayari inakabiliwa na mashtaka ya kupigia debe huduma yake ya manunuzi ya mtandao, kwa kutumia bidhaa za mahasimu wake wa kibiashara.


Source: BBC
 
Hapa ni sawa eti unamshitaki mtu kwa vile anawatongoza mno wanawake kwa hiyo anakunyimeni uhuru.
Si ukatongoze na wewe!
 
Haya mashtaka hapa kwetu naweza kuyafananisha na anayokabiliwa nayo Lugumi.
Nahisi yanweza kumfit mtu kama Bakresa ambaye anauza mpaka maandazi, sambuza, chapati nk, biashara ambazo zingefanywa na watu wa hali ya kati mpaka chini

Maana haingii akilini mtu anauza kuanzia materails mpaka final products
 
Nahisi yanweza kumfit mtu kama Bakresa ambaye anauza mpaka maandazi, sambuza, chapati nk, biashara ambazo zingefanywa na watu wa hali ya kati mpaka chini

Maana haingii akilini mtu anauza kuanzia materails mpaka final products
Hii niliona nchi fulani kampuni kubwa ya mafuta ilikuwa inamiliki vituo vya mafuta kama 120 hivi, Lakini Sheria ilikuwa inawaruhusu kumiliki malori ya mafuta 5 tu,
Maana yake wenye malori mengine wafanye kazi pale, hii inaitwa kugawana umaskini
 
Back
Top Bottom