ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Sayansi na teknolojia ndiyo hiyo Ndugu zanguni!
Tanzania yetu na miaka 51 ya uhuru!
Google ni ulimwengu wa uvumbuzi wa bidhaa na majaribio ya teknolojia, katika baadhi ya mawazo na uvumbuzi ambao Google wanaendelea kufanyia kazi kuna mambo ambayo sio ya kufirika, gari inayojiendesha na kompyuta ya kuvaa kama miwani ni miongoni mwa teknolojia hizo, kwa mtazamo wa haraka unaweza kudhani kuwa itachukua miaka zaidi ya 10 Google kuweza kuziuza bidhaa hizo kwa watu wa kawaida.
Ukweli ni kwamba Google imeshatangaza kuwa Google Glass itaanza kuuzwa mwaka huu wa 2013. Google Glass ni kompyuta ambayo huvaliwa kama miwani na ina uwezo na matumizi mbali mbali kama vile kurekodi video na kupiga picha. Katika ongezo jipya la Google Glass ni kwamba kompyuta hiyo itaweza kutumia amri za sauti (voice command), kuanzisha amri ya sauti unatakiwa kuiambia miwani hiyo OK Glass na miwani itaanza kukusikiliza unataka ifanye nini kabla ya kuipa amri kama vile record video. Pia Google wameonyesha baadhi ya matumizi ya miwani hiyo ambayo ni ya kawaida kabisa mbali na yale ya kuchupa na parashuti kutoka kwenye ndege.
Chanzo na Makala kwa Ukamilifu: http://www.gajetek.com/2013/02/google-kutoa-kompyuta-ya-miwani-mwaka.html#more
Ilikuwa mwaka jana morphine kwenye Developers Conference Google I/O walipotoa Nexus 7 na Nexus Q iliyofeli (mpaka sasa)