Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
“Hatutokuwa tayari kabisa sisi na wananchi walioko nyuma yetu hatutokuwa tayari kwenda kwenye uchaguzi ambao kimsingi sera na taswira yake itakuwa ni tendo la unajisi,” amesema Golugwa.
Amesisitiza kuwa mifumo ya uchaguzi inayoongozwa na sheria, kanuni na Katiba ya nchi ina mapungufu makubwa yanayohitaji marekebisho ya haraka, na iwapo serikali na vyombo vinavyosimamia uchaguzi havitatoa majibu ya wazi, basi CHADEMA haitashiriki uchaguzi huo.
Golugwa ameongeza kuwa msimamo huo haujajengwa kwa misingi ya kisiasa pekee, bali ni sauti ya Watanzania wengi wanaotamani kuona taifa likiendelea kwa misingi ya haki na amani.
“Msimamo huu si wa chama peke yake, ni wa wananchi. Wapo viongozi wa dini, wapo wazee wa taifa, wapo wanachama wetu wanaotutumia maoni kila siku. Tunachosema ni kwamba, bila mabadiliko ya kweli, hatutashiriki uchaguzi ambao hautaleta haki,” amesisitiza Golugwa.