Goli la mkono la Nape Nnauye

Goli la mkono la Nape Nnauye

The Don

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2011
Posts
3,499
Reaction score
1,172
Goli la mkono ni kauli yenye kumaanisha ufungaji wa goli ktk mpira wa mguu usio halali kwa kutumia mkono kinyume na kichwa au mguu kama sheria za miguu zitakavyo,kauli hii ilitolewa na Nape Nauye wa C.C.M akimaanisha ushindi kwa njia yoyote hata zisizo halali kama itambulikavyo na sheria za uchaguzi,kauli hii imeimarishwa na mwenyekiti wake J.K aliposema hadharani ushindi wa C.C.M uko pale pale huku akifananisha upinzani kama moto wa mabua unaoisha haraka,turudi kwenye goli la mkono litakavofungwa kama ifuatavo,

1. Kabla ya zoezi la uandikishaji wenyeviti na makada wengi wa C.C.M walihamasisha wanachama wao kujiandikisha kwa wingi kama haki yao na watz kiujumla.

2. Baada ya wapinzani kushtukia janja hii wakapita ktk majimbo kuhamasisha kujiandikisha katika daftari la kupigia kura,zoezi lililoamsha watanzania wengi.

3. Watanzania wengi wenye vyama na wasio na vyama walijitokeza zoezi la uandikishaji lilipoanza ambapo tulishuhudia mwamko mkubwa tofauti na tulivotarajia na zoezi kuhitimishwa kukiwa na mazuri na madhaifu yaliyojitokeza.

4.UHAKIKI WA VITAMBULISHO,hapa ndipo goli la mkono linapofungiwa kwani vituo vingi vya uandikishaji baada ya kumaliza zoezi la kuandikisha vimetoa majina kuhakiki taarifa za vitambulisho ambapo kumeonekana udhaifu mkubwa kwa majina mengi kutokuonekana mf.kituo kilichoandikishwa watu elfu moja kuonekana na majina 50 tu,au vingine kuonekana majina mapya kabisa.

5. Baada ya majina mengi kutokuonekana ktk vituo vya kujiandikishia huku mengi ya yale yaliyoonekana ni dhahiri sasa ambao hawajaonekana hawataweza kupiga kura kwa kukosa sifa na vigezo.

6. Uboreshaji wa taarifa utafanyika baadae ukizingatia makosa madogomadogo pia kuwapa fursa wale waliohama vituo na majina kuonekana mwanzo kuboresha taarifa zao ili ionekane demokrasia kutendeka ambapo watu wengi tena watashindwa ktk zoezi hili.

7. Kutumia vitambulisho viwili(kitambulisho cha utaifa na kile cha kupigia kura kilichoidhinishwa) ktk kupiga kura ktk vituo vyenye upinzani mkubwa ambapo watu wengi hapa watakosa haki yao ya msingi ya kupigia kura.

8. Kutangazwa matokeo ya kura ambapo matokeo yatawekwa wazi ktk vituo na kura zilizopigwa.

9. Mwisho zoezi la upingaji wa matokeo yaliyotangazwa na tume mahakamani ambapo pia halitofanikiwa kutokana na taarifa za uandikishwaji na upigaji kura tangu mwanzo.
 
Hivi Edo akipata 70% na yule wa kupiga mbizi akipata 28% hapo nami atatangazwa mshindi???????LENGO LETU NI KUMTOA CCM HATUNA SHIDA NA MAGUFURI NA WALA EDO SIO MSAFI SANA.TUMEAMUA KWA PAMOJA NA KUKUBALIANA KUWA CCM MWAKA HUU CHALIIIIIIIIIIIIIII
 
Sema yote rakini lazima tupige kura majina yawepo yasiwepo ilimradi Nina kitambulisho mambo ya jina haripo sio Kazi yangu walinipa kitamburisho cha nini?
 
Sina mda wakwenda kuhakiki tena...nachijua kitambulisho ninacho nakura ntapiga wala hakuna wakunizuia...asante.
 
Msiwe na shaka soon raisi lowassa analitaftia ufumbuzi
 
ccm inaangaika kutengeneza timu za kampeni hv unawezaje kumuingiza mtu mzima uliyemuaibisha kwenye uteuzi wa urais ili apige kampeni hali iko wazi kwamba mwenyekiti alikuwa na majina yake matano huku watu wazito kama akin a sitta ,pinda ,bilal ,mwandosya wakitupwa nje huku vijana wadogo wakiingia tano bora.Hivyo basi kikwete anawachezesha watu wazima kama karanga kwenye ungo.Daima ukikosa akili na msimamo unaweza kuchezewa kama zezeta.CCM Imekufa kabisa mnaounda timu za kampeni mnasumbuka bure.
 
Hatimaye Majigambo Na mbwembwe za Magufuli Na makada Wa CCM juu ya Ushindi in Mbinu Chafu zinazofanywa Na Time ya Uchaguzi ya Kuandikiza Baiskeli Majengo Wachina Wazungu ktk Daftari la Wapiga Kura..Madudu hayo ni ya jumbo moja tu.Ni matarejio yetu kuwakuna majina mengi sana ambayo yataendana Na Takwimu za watu milioni 28 aliowataja Mwenyekiti Wa CCM akitofautiana Na za Tume yenye watu milioni 22.Inaonekana Goli la Mkono in Watu Milioni 6.Wapinzani kuweni making Na uchafu Wa Daftari limefanywa hivyo sio kwa bahati mbali no MKAKATI MAALUMU
 
hivi huwa mnalala mnaota au hamna mengine ya kuandika?mjifunze hata kuandika pambaf!
 
Back
Top Bottom