Godbless Lema: Heri ya Christmas Mahabusu na Wafungwa wote

Godbless J Lema

Arusha MP
Sep 28, 2013
92
2,204
Heri ya Christmas kwa Mahabusu na Wafungwa wote.

Christmas mwaka Jana 2016 nilikuwa nimeshikiliwa kama mahabusu Geraza kuu Arusha kwa kunyimwa dhamana, tukiwa Gerezani tarehe kama hii Mimi na wenzangu tulikuwa tunaandaa sikukuu ya Christmas.

Leo ninawakumbuka rafiki zangu wengi niliokaa nao vizuri, Wengine wamefungwa na wengine bado wako mahabusu , kwa kweli zaidi namkumbuka sana Wakili Median Mwale ambaye amekuwa mahabusu kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita. Siku hiyo ya Christmas baada ya ibada iliyoongozwa na Askofu Lebulu , tulifanya maandalizi ya kula chakula ambacho familia zetu zilituletea , tukiwa tunakula Wakili Mwale alisema, Mh Lema wewe utatoka , na Mimi na wenzangu na muomba Mungu Christmas inayokuja niweze kuwa nje, kwa bahati mbaya Wakili Median Mwale na rafiki zake bado wameshikiliwa Gerezani . Inauma sana kwamba Ofisi ya Dpp na Mahakama kwa zaidi ya miaka sita wameshindwa kumaliza shauri hili.

Kumweka mtu Mahabusu kwa miaka yote hii ni ukatili mbaya sana, kwa kipindi ambacho nimekuwa Magereza nimeweza kuelewa huzuni za familia na watuhumiwa, ndio sababu wakati Mh Rais alipowasamehe Wafungwa hasa wenye makosa makubwa nilimshukuru sana only kwa sababu najua huzuni ya kukosa uhuru.

Wakati Leo nina wakumbuka na kuwatakia heri ya Christmas njema mahabusu na Wafungwa wote Nchini ni muhimu watu wote mlioko kwenye vyombo vya sheria mjue kwamba wajibu wenu unapokosa utu na upendo maana yake ni kuumiza watu na kutesa watu mahali fulani .

Ninamuomba Mh Rais, aingilie kati suala la Wakili Median Mwale, kwa kweli huyu mtu inatosha kuwepo Magereza kwa zaidi ya miaka sita bila kuhukumiwa.

Dpp najua unajua kuna watu wengi wako Magereza kama Median Mwale,nguvu uliyopewa na sheria inapokosa upendo basi nguvu hiyo inakuwa ni ukatili .

Krismas Njema Mahabusu na Wafungwa wote Nchi nzima.

Godbless Lema (MB)
 
Heri ya X mass nawe Mh. Mbunge!

Hongera kwa kuelimika baada ya kuhudhuria mafunzo ya nidhamu na adabu Mahabusu kwa Miezi minne maana tangu utoke 'Mafunzoni' umekuwa Mwanasiasa Mkomavu kwa kuachana na Matusi na hata unapofanya kazi zako za Siasa unatii Sheria bila ya shuruti.

I hope 2018 utakuwa Mwanasiasa bora zaid Mh. Mbunge!
 
hata mimi naomba rais awaonee huruma kaka zangu wapo mahabusu miaka 10 sasa hapo segerea...kila mtu akitumia sauti yake kuombaomba kama hivi hakika wafungwa wote tutaomba watolewe gerezani/mahabusu maana kila mtu anamtu wake anayempenda huko mahabusu/gerezani hata kama mtu huyo yupo gerezani kwa kuua lakini bado kuna mtu huku nje anamtakia mema siku moja atoke gerezani.
 
Acheni kulia lia....wapo mahala salama...ni siku za karibuni tu tangia Mh Rais atoe msamaha kwa baadhi ya wafungwa...lakin kwa taarifa zilizopo...tayar mfungwa mmoja karudia uhalifu na kuuwawa na wananchi...na mwngine kunusurika thn kupewa hukumu ya miaka 15 jela..Mh Lema point yako ni hyo wakili...yupo pale kwa kanun na taratibu za nchi hii
 
Nishukuru kwa niaba ya mahabusu walio gerezani japo mimi nipo uraian, ila kuhusu swala na huyo wakili naona umelalamika tu kueleza kukaa kwake mahabusu for 6 years ila hujasema anatuhumiwa kutenda kosa gani, ungetaja kosa hawa wachangiaji wangechangia kwa busara maana inawezekana katenda kosa ambalo anastahili dhamana au kosa ambalo dhamana hastahili, so kuandika jumlajumla hivi kuna hatari ya wasio reason mambo kuanza kutukana tu kwa hisia
 
Adui mkubwa wa hii nchi ni ccm na mifumo yake mibovu ya kiutawala, kwahiyo huwezi kumuomba shetani mambo yaliyo mema akakusikiliza. Farujohni akisikia mateso ya watu hao hasa wale walio kinyume na misimamo yake hufurahi sana meno yote 32 nje kwa vicheko. Shetani hajawahi kuwa na upendo na mwanadamu kamwe
 
Mkuu mkiendelea kutegemea huruma , upendo na Amani pamoja na utashi WA wanasiasa ambao nyie Ni tishio la madaraka Yao, hata ubunge 2020 mtausikia kwenye radio ,tena 87.5......

Badilisheni "mbinu" za medanii kama wenzenu WA CCM wanavyowashauri.

Pendekeza mbinu ya kutumika hapa sio uchomekee tu huku huna mbinu yoyote.
 
Nishukuru kwa niaba ya mahabusu walio gerezani japo mimi nipo uraian, ila kuhusu swala na huyo wakili naona umelalamika tu kueleza kukaa kwake mahabusu for 6 years ila hujasema anatuhumiwa kutenda kosa gani, ungetaja kosa hawa wachangiaji wangechangia kwa busara maana inawezekana katenda kosa ambalo anastahili dhamana au kosa ambalo dhamana hastahili, so kuandika jumlajumla hivi kuna hatari ya wasio reason mambo kuanza kutukana tu kwa hisia
Anatuhumiwa Kutakatisha fedha.

Lakini vyovyote iwavyo kumuweka mtu mahabusu kwa kisingizio "Ushahidi haujakamilika" ni Ukatili wa Juu mno, nikama anahukumiwa kutumikia kifungo kabla ya Kifungo chenyewe endapo atakutwa na hatia.

Hukumu za makosa ya aina hiyo endapo anatiwa hatiani ni miaka 7 jela, hebu imagine sasa endapo atakutwa Hana hatia unadhani anakuwa amekuwa katika Hali gani?
 
Hatari sana, bado tuko na mifumo ya kikoloni kabisa, DPP anayo mamlaka makubwa mno kiasi kwamba anakuwa mungu mtu kama ilivyo kwa rais wa nchi
Umeona kitu ambacho nasema kila siku karibu mwaka 30 huu. Maana ni km tumebadili rangi tu kutoka mkoloni weupe kuja mkoloni mweusi maana tumerithi sheria na kila kitu cha mkoloni police ipo kwa ajiri kulinda watawala tu mambo ya rc dc ni ukoloni tu
 
Back
Top Bottom