Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,346
- 26,138
Jimbo la Arusha Mjini, kadiri nijuavyo, halikuwahi kuongozwa na chama cha upinzani kwa vipindi viwili. Mbunge wa kwanza wa upinzani alikuwa Mhe. Makongoro Nyerere (aliyekuwa NCCR-Mageuzi) aliyelinyakua Jimbo hilo mwaka 1995 lakini baadaye ubunge wake ulitenguliwa na Mahakama.
Mbunge aliyemaliza kipindi chake cha 2010-2015 ni Godbless Jonathan Lema wa CHADEMA. Tayari ameshawatumikia wananchi wa Arusha Mjini kwa kipindi cha miaka mitano. Uchaguzi wa Arusha Mjini uliahirishwa hadi tarehe 13/12/2015 kufuatia kifo cha aliyekuwa mgombea wa ACT-Wazalendo, Marehemu Estomil Malla.
Mnamo tarehe 13/12/2015, Lema ataingia kwenye rekodi mpya kwa kuwa Mbunge wa kwanza wa upinzani kuiongoza Arusha Mjini kwa vipindi viwili mfululizo. Wabunge wa zamani wengine wa Arusha Mjini ni Mhe. Abdurahman Kinana na Felix Christopher Mrema.
Najua kuwa Mhe. Lema anaendelea kufuata katazo la wananchi wake wa Arusha Mjini waliomtaka asipige kampeni na asubiri tu ushindi wa kishindo. Kimahesabu, kura za Arusha Mjini zaweza kukipa chama kitakachoshinda kiti cha Mbunge wa viti maalum kwakuwa zaweza kuwa nyingi kuliko jumla ya baadhi ya majimbo.
Kila la heri G. J. Lema kwenye uchaguzi wako wa tarehe 13/12/2015.