Kuamini uwepo wa Mungu/akili iliyotokeza huu ulimwengu sio mpaka upate msaada fulani wa kimiujiza.
Kadhalika nje kabisa ya vitabu vyote vya dini mimi na wewe ndio vitabu vikuu zaidi kuliko hivyo vya maandishi.
Jiulize kidogo tu wewe hapo ulipo una miaka mingapi na hujawahi kupoa japo umeishi mazingira yenye baridi kali?
Umeshawahi kufikiri namna DNA inavyofanya kazi kwa usahihi na kuhifadhi taarifa zote sahihi kuhusu kiumbe kuliko mashine yoyote iliyowahi kubuniwa na mwanadamu?
Umeshawahi kufikiri vile mwili wako unavyofanya kazi za ajabu na za kuogofya?
Je, Ulishawahi kufikiri namna kuna magimba makubwa huko angani mara elfu kadhaa ya dunia, huku yakijiendesha kwa usahihi kabisa kuliko vyombo vyote vya usafiri vilivyowahi kutengenezwa na mwanadamu, tena magimba hayo yamejiendesha kwa miaka bilioni kadhaa bila kukosea?
Je, ulishawahi kufikiri namna mapenzi yalivyo matamu?
Wewe unadhani maada zilizojitengeneza zenyewe zinaweza kupanga zikakutane alafu zifanye kwichikwichi huku zikipata utamu unaoupata?
TAFADHALI KAMA UPO NA MTU YEYOTE HAPO HEBU MTAZAME KWA SEKUNDE KADHAA AU DAKIKA KADHAA.
Umeona nini?
Bila shaka umemwona mtu mwenye macho mawili mazuri sana yenye maajabu ya kuona na kutambua kwa kupitia ubongo ambao unatenda kazi kwa kutegemea kemikali nyingi sana ambazo hupatikana kwenye vyakula tunavyokula, pua yake inayovutia ambayo inaweza kutambua hadi aina ya chakula kilicho karibu au kinyesi na nk kwa kutegemea ubongo huohuo.
Pia umeona nywele zake nzuri, ngozi safi yenye hadi vinyweleo vya kutolea jasho.
Nyuzi zake ambazo zipo juu ya macho kidogo ambazo wanadamu wote tunazo na hazijawahi kubadilika zikaota mgongoni au nyuma ya shingo.
Kama unaweza hebu mwambie atembee, kisha jiulize tena kama kuna mashine tata kama tulivyo sisi ambayo inaweza kujileta tu yenywe pasipo na muundaji wake aliye na maarifa makubwa sana!
Je, ni jambo linalopatana na akili kwamba sisi tulitokea tu kwa kemikali kujikusanya zenyewe hadi kututokeza tukiwa na macho, masikio yenye kutambua hadi sauti ya adui yako, pua iliyokaa palepale, miguu yenye kucha zenye amri ya kuwa vilevile kupitia DNA ya mwanzo?
Mambo hayo yaweza kutokea tu kwenye kiwanda cha kisasa kilichoandaliwa na mbunifu makini
Kemikali zisingeweza kujikusanya zenyewe ziweke na amri au sheria ya upatikanaji wa mtoto kwa kungonoka watu wa jinsia tofauti huku DNA ikijigawanya pande zote mbili kwa kutembea na taarifa sahihi za pande zote kuanzia kwenye ngozi mpaka kwenye kucha, miguu, sauti kwa kiasi na mambo mengine mengi.
Hata kama inawezekana jambo hili lingekuwa vipi kwa viumbe tofautitofauti?
Tukubali tu kuna wajanja au mjanja aliyefanya haya hata kama hatumjui.
Mimi sio muumini wa dini yoyote ila siwezi sema haya mambo yamejiunda yenywe tu! Hapana
Kwahiyo maada zilijitokeza zenyewe, zikaunda magimba kila moja kwa namna yake huku zikijiunda zenyewe hadi kutokeza viumbe tata kama sisi?
Tena maada hizohizo zikaweka na sheria za kudumu kwenye mambo tata yanayoendelea ndani ya miili ya viumbe na kwenye ulimwengu kwa ujumla?
Kunae mtaalamu wa haya ila hatujui nae katokea wapi.
Kuuliza mtaalamu wa haya yote alibuniwa na nani ni sawa siku moja tutengeneze robot lenye uwezo wa kuhoji, alafu lituhoji nini chanzo chetu/yaani tulianzaanzaje hadi tukawepo hapa duniani....bila shaka hatutoweza kumpa jibu la uhakika robot wetu. Hivyo swali hilo tunapaswa tukae kimya kwanza mpaka tutakavyojiongeza zaidi kimaarifa mara makumi kadhaa!
Tuujue kwanza ulimwengu A-Z, tumjue muundaji wake vyema ndipo tumuulize kwa upole alipotokea
Sitaki maswali kwakuwa hata mimi nina maswali kuhusu uwepo wetu na vitu vingine humu ulimwenguni.