BENACO CAMP
Member
- Jul 19, 2011
- 12
- 14
Wapendwa wana JF natambua ni masaa machache yamebakia kwa Mh.Lema kufikishwa mahakamani. Nikiwa kama mdau wa JF nimefanikiwa kuona video zote zilizowekwa humu jamvini. Pamoja na hayo toka kukamatwa kwake nimefanikiwa kusoma taarifa mbalimbali zilizotolewa na watu tofauti na hata zile za CDM kanda ya kaskazini. Naomba nikiri kwamba sina upande wowote katika hili bali kusimama kwenye kweli na kweli ndiyo ninayoiamini. Hii ndiyo sala yangu. Eeeh Mungu wangu..Naipenda Nchi yangu Tanzania na ninapenda amani yake na watu wake. Nipo kinyume na hali yeyote itakayoleta hofu na ufunjifu wa amani Arusha na Tanzania kwa ujumla. Hakika wewe ni Mungu na ninajua fika kuwa hakuna hakimu wa haki zaidi yako wewe. Naomba kweli yako Mungu itawale juu ya jambo hili. Kwa jinsi nilivyoona video zote Mimi sioni kosa la Lema. Naliita jina lako Mungu wangu nakuomba kama ni visasi au chuki binafsi ingilia kati na uhukumu kwa haki. wabaya waonyeshe ubaya wao na uonyeshe wazi wenye hila waaibishe. Futa udhalimu huu na onyesha kwamba wewe ndiye mtawala wa haki. Nakukabidhi Arusha, nakukabidhi maisha na amani ya wana Arusha. Shetani ashindwe!!!. God bless Arusha. God bless Tanzania. God bless Hon.Godbless Lema.