Go goooooo goooooo –nje, nje, nje

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Wasikilizaji C C M wamekosa bao la wazi kabisa.

Alikuwa winga machachari Nap, alivuta akawalamba chenga mabeki wote wawili kwa mpigo akamuunganishia pande captain J ambaye badala ya kuusukuma kimiani akadribble na kurudisha kwa beki Chili.

Priiiiiiiiiiiiiiiiii Na mpira umekwisha ……..

Kwa mara nyingine tunashuhudia timu yetu ikitoka uwanjani wakijigamba kwa chenga nyingi lakini mmmmh. Washabiki wanaonekana wanalumbana, wengine wanafurahia zile chenga hata wanataka kuandamana kwa mchezo mzuri wengine wanasema wao walitaka magoli ili wasonge mbele. Hawaamini kama inatosha kujivunia chenga wakati timu pinzani zinajikusanyia magoli na kupanda chat. Wana hofu ya kushuka daraja na kwenda kucheza na timu za mchangani. Wanasikia viwanja vya huku ni mbigili tupu, sasa fikiri timu za huko zinacheza peku wataweza… wanawaona wenzao wa timu ya kijiji cha jirani tangu warudi mchangani hawasikiki tena.

:panda:
 
Back
Top Bottom