adriz de mbusii
JF-Expert Member
- Sep 2, 2017
- 16,786
- 37,803
💯Anguka mara 7 simama mara 1, ukitupa kete gizani japo zinakosa, amini ipo kete moja tu ni lazima italenga tundu.
Yeahman
View attachment 3539227
#Kukata Tamaa ni sawa na Kukubali kuwa wewe ni maiti
Tupo site uwanja wa vita tunapambana bila kukata tamaa tukishindwa tunainuka tena na kufanya tathimini wapi tulipo kwama na kurekebisha Kisha kuja na nguvu mpya mpaka tone la mwisho Triumphantly..View attachment 3539229
Faida za kukata tamaa
1 . Kuna okoa mda.
2. Kuna Linda afya ya akili.
3.kuna okoa upotevu wa nguvu.
4. Kuna fungua milango ya fursa mpya
Hiki ni nini mkuu?
Kuna vitu na vitu na Kuna scenarios sio kila misimamo au kanuni itatumika na kufanya kazi kila sehemu na katika kila hali.Faida za kukata tamaa
1 . Kuna okoa mda.
2. Kuna Linda afya ya akili.
3.kuna okoa upotevu wa nguvu.
4. Kuna fungua milango ya fursa mpya
Jeneza shambaniHiki ni nini mkuu?
Kukaa ndani, sio kukataa tamaa mtu anaweza amua kulala mwaka mzima tu na bado hajakata tamaa , ila kapumzisha fuvu anatafakari njia mpya na nzuri za kufanya .Kuna vitu na vitu na Kuna scenarios sio kila misimamo au kanuni itatumika na kufanya kazi kila sehemu na katika kila hali.
Mfano mtu umejiajiri biashara zijaenda kombo na ukajaribu kutafuta kazi ukakosa sasa utamshauri akate tamaa akae ndani asuburi kifo tu ?
Siri ya never give up, iko hivi..kuwa ukiona kuna wazo limeingia kichwani mwako ujue kuna uwezekano mkubwa unauwezo wa kulitelekeza.Binadamu sio wajinga huwezi ukawa umelala kitandani mwako huna hata baiskeli ukatamani kumiliki milki meli: mtu aliye na baiskeli atatamali awe na boxer, ukipata boxer utatamani ICT, ukipata ICT, mtu ataenda Toyota Hilux n.k...Kuna baadhi ya mambo katika maisha ni impossible hata usipo give up! Hayatimii, Hutayakamilisha.
Solution pekee niku give up!
Huu msemo wa "never give up" upo kinadharia zaidi lakini kiuhalisia si rahisi kiivyo.