Ghost phase kwenye maisha ya mwanaume

Umenikumbusha mbali sn miaka 8 nyuma nliwahi fungua biashara mkoa fulan na skuwa mwenyeji wa uko nlifungua banda ndani lina pool table, bonanza 2, play station, vinywaji, tv with azam king'amuzi, nikaweka na mzk mzto sn nlifunga mzk wa gari ukiwa full kbs, vjana wakawa hawakauki mle wenyeji nao wakafungua ila wao waliweka pool table tu tukawa jiran kumbe wakawa wanaumia mi ninavyopata hela wakawa wanapga majungu sn na fitna ili nspate ktu na nfunge biashara ili wao wafanye kama mimi, nlipogundua hlo nikafungua biashara sehem nyngn kmykmy uku nikiwa nao hapo maeneo yao nacheka nao story kwa sn, nlipokamilisha walishtukia tu nahamisha vitu yule jamaa wa mabonanza nae walikuwa kabila 1 akasema bonanza niziache ampe mkabila mwenzie nikaztema nikalala mbele nlifuta namba zao wote skuchagua, uku nyuma wakaanza majungu mengi sn na kutengeneza kashfa mi kimya nikikutana nao sisalimii mtu napta tu, ajabu wao tena wakaanza nisalimia na kujsema waliokuwa wananifanyia fitna sms za umepotea sn mi kmy. Napenda sn ukmya
 
Kwa maisha ya sasa yalivyo race ukiapply ghost phase kwa demu wako ukirudi usishangae kuitwa shemeji na hakuna anayejali 😹😹😹

Tuliza mbupu tu utafute ajira shogaangu..!! 🤣😹
Huyu kwa hayo madini sidhani kama bado anatafuta ajira😁.
 

Sisi tulozaliwa familia za kimaskini kuna muda hua unafika hii hali inakujia automaticaly. Utake usitake utajikuta alone alaf kama dunia imekudondokea hivi.. Na kila ukijaribu kufurukuta basi utaskia watu wanakufariji kwa maneno ya kukukatisha tamaa huku wakikumbushia mabaya yako na mema ulotenda yakionekana yalikua hayana umuhimu. Kwamba hata usinge tenda wewe angetenda mwingine, na hata yasinge tendeka kabisa kulikua hakuna cha kuharibika.

Lakini ndo wakati sahihi wa kuinuka, well said mleta uzi..
 
Makazini na sehemu za biashara sio sehemu za kutengeneza marafiki na wafanyakazi/wafanyabiashara wenzako. Huko unapiga tu kazi unasepa.
 
Ni kweli mkuu. Kama wazazi wako wanakutegemea na familia yako inakuangalia utengeneze njia ya wanaokufuata wapite, kamwe usije ukajaribu kuishi maisha ya watu ambao wanategemea wazazi wao au wamekuta tayari washatengenezewa njia
 
Ni kweli mkuu. Kama wazazi wako wanakutegemea na familia yako inakuangalia utengeneze njia ya wanaokufuata wapite, kamwe usije ukajaribu kuishi maisha ya watu ambao wanategemea wazazi wao au wamekuta tayari washatengenezewa njia
Hatari mkuu. Hiyo imenikuta niliporomoka kiuchumi alafu wale niliowasaidia kuwainua wakawa wako stable, huwezi amini japokua ni familia moja lakini nilisimangwa sana. Kama nilitoka huko nikachukua hela zote na miradi yote nikahonga kwa mara moja.

Kilicho nishangaza kwanini wananisema vibaya na sijafanya kusudi, na huenda nisingetumia kuvu kubwa kuwainua wao ile hali me nisinge ipitia. Na sijawaomba msaada wala nini, nikawa naskia maneno ya chinichini mmoja wao anasema mpaka nimuombe msamaha atanikopa hela kidogo nijikim.

Dunia ngumu sana. Nimekaa kimya nimechanga karata zangu sahzi naanza kurudi kwenye form yangu kwa kasi, watu wamenuna. Wengine wanajichekesha kishoga. This time around nyoka halambi ungi, kila jitu likale lilipo peleke mboga kudadeku.

Kwenye ghistphase i was all alone, compleatly alone. Kuna muda mpaka unaweweseka unahisi dunia ni shimo na umetumbukia pekeako. Noma saana.
 
Unaweza kufanya maendeleo bila kujitenga. Zingatia kuwa na kiasi kwenye mienendo yako. Binadamu ni viumbe wa kijamii hawawezi kuishi kwa kujitenga.
Kuna watu motivation yao wanaipata kwa kujitenga, sio kujitenga kabisa ila kujitenga kutoka kwa wale anaofahamiana nao like mahusiano yake ya karibu, Ndugu, jamaa, marafiki, mpenzi, wazazi etc.

Mfano: Kuna siku niliandika humu kuna mtu alikuwa ananipaga 30k-50k kwa siku kila siku kipindi tuna date. Mtu mwenyewe yuko humu, Haikuwa hivi hivi, ukweli ni kwamba tulifahamiana tukiwa wadogo akajaona hajajipa sijui alionaje mwenyewe, kuna kipindi akaniaga kuwa hatokuwa available, Alienda kuhustle kwa about 3 years karudi ana elimu nzuri, kazi nzuri na hela anayo ndio hapo akawa ananipa hizo hela. (hili si la muhimu sana) la muhimu ni kusema kuwa kuna watu no contact inawasaidia kuwa motivated.

Nilikuja kuelewa maisha ya wanaume yana mambo mengi sana, nadhani ndio hii ghost mode anayoizungumzia mleta mada.
 
Ukisha kuwa mtu mzima muda wa kudeal na upumbavu hakikisha kuwa unaukosa , deal na mambo ambayo ni potential only na watu ambao ni potential, Ukibaini tu kwamba Kuna watu ni fake stay away from E'm haraka sana
 
Sasa mfano umetokomea huko umerudi unakuta wale uliokuwa ukiwa-'ghost' hawakuhitaji tena. Itakuwaje?

Naona kama lengo la kuwa ghost ni kuja kuwatambia watu kimtindo.
 
Exactly, 🎯📌

Siku zote mwenye future plan Blue print Vision ya maisha Huwa Haoni shida kuanza Moja au Haoni tabu kujitenga na watu ambao Wana mchukulia poa ,,

Ukiona kwamba unafanya mambo makubwa Yaliyo beba maono ya kuwakomboa watu halafu still watu hao Wana kuchukulia poa , Jiweke nao mbali kabisa hakikisha unapambana kivyako na kutimiza ndoto zako ili waweze kujua kwamba wewe ndiye uliye kuwa mbeba maono Wa maisha Yao na kuwa poteza wao wewe hujapoteza kitu Bali wao ndio walio poteza
 
I feel you

Nimepitia hiyo situation Kmmk

Nimewabeba watu Nika wanyanyua wakaja wakakaa sawa kimaisha then hao hao ndio wana niattack like I have done nothing niliuza roho yangu ili watu wote tufanikiwe kumbe I was mistake myself,

Haya mambo ya kuwabeba beba watu Haya nimejifunza nikitu kibaya sana it will ruin your career, halafu hao hao mwisho wa siku wana kucheka , now i have lean a lesson,, Never going back again ni mbele Kwa mbele tu , Kila mtu apambane kivyake
 
Yeah inasaidia sana Mimi ninao hiyo wisdom Huwa nikipitia msoto mkali Huwa najitenga kabisa hata social network Huwa sitaki kutumia Huwa nataka kupambana na maisha like die hard Ile Ile, mitandao Huwa naona inanifanya nipoteze concentration pia Huwa napunguza circle ya watu kabisaaa Huwa nabaki na watu wachache and hiyo plan Huwa inanifanya niibuke mshindi
 
Sasa mfano umetokomea huko umerudi unakuta wale uliokuwa ukiwa-'ghost' hawakuhitaji tena. Itakuwaje?

Naona kama lengo la kuwa ghost ni kuja kuwatambia watu kimtindo.
It’s for personal development, sidhani kama unarudi kuwatambia. Kurudi ni reconnect.

Kama hawakuhitaji pia ni sawa, probably walikuwa hawakuhitaji toka mwanzo.
 
Sasa mfano umetokomea huko umerudi unakuta wale uliokuwa ukiwa-'ghost' hawakuhitaji tena. Itakuwaje?

Naona kama lengo la kuwa ghost ni kuja kuwatambia watu kimtindo.
Usiishi kwa kutafuta validation and acceptance ya watu. Watu wanaokuja kwenye maisha kuna wengine wataondoka na wengine watabaki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…