kitengo cha dharura Muhimbili, wagonjwa wamepungua kutoka 80 - 100 kwa siku hadi 25 kwa siku taarifa kutoka kwa Meneja wa kitengo, Dr. Siland Optatus imeripotiwa na Tanzania Daima
Je nini nini athari za punguo hilo kipesa na kiafya?
Pinda anajua
Idadi ya vifo toka mgomo kuanza: Hospitali ya Rufaa mbeya 22, Bugando mwanza 25, temeke 19, amana 15, mwanyamala 20, muhimbili 57, Uwazi Ukurasa wa 2, trh 31.
Ingawa taarifa hizo hazisemi ni vifo vingapi kwa siku na ongezeko la vifo hivo nikiasi gani toka mgomo kuanza. Kwahiyo inakuwa vigumu kuelewa umuhimu wa namba hizo
Je kuna kuna data zozote ambazo tunaweza kupata kujua gharama na athari za mgomo ni kubwa kiasi gani. Nadhani imefika wakati tunahitaji kuanza kuongea na viongozi wetu kwa namba, na kuwashitaki na uhalisia wa madhara wanayosababisha. Labda tuanze kujua majibu ya maswali haya
1. Je namba ya vifo toka mgomo uanze ni ngapi? na inatofauti gani na vipindi vya nyuma?
2. Wagonjwa wangapi wanahudhuria hospitali kwa siku? na namba hii inatofauti gani na ya awali?
3. Wangojwa wangapi wanatibiwa kwa siku? na namba hii inatofutiana kiasi gani na watu walikuwa wanapata tiba kabla ya mgomo?
4. Mapato ni shilingi ngapi kwa siku toka mgomo huu uanze? na mapato hayo yanapishana vipi na mapato ya kila siku kabla ya mgomo kuanza?
5. Watoa huduma za chakula na vinywaji, madereva taxi na pia wenye maduka mauzo yao kwa siku yamepata athari zipi?
6. Je hospital and zahanati za karibu wanamaongezeko ya wagonjwa? na madhara yake nini?
so what!