Gharama za kwenda na kurudi Afrika kusini

OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,459
2,000
Naomba mwenye uelewa kuhusu gharama ya kwenda Afrika kusini zikoje ukizingatia nauli ya kwenda na kurudi,kulala siku mbili hotelini je,kwa kukadiria inaweza kuwa shilingi ngapi za kitanzania.maana nataka niende huko kikazi wiki ijayo ila sijajua gharama zikoje?
 
50thebe

JF-Expert Member
Mar 10, 2011
2,886

Ukitumia South African Airways ni Rands 4600/-. Hii ni return ticket. Unatumia jumla ya masaa sita angani. kwenda masaa matatu na kurudi vivyo hivyo.

Kwa basi nauli andaa wastani wa laki 5 hivi.

Usisahau yellow fever vaccine card.

Hotel unapata kuanzia TZS 50,000 hadi laki 5 kwa usiku mmoja. Google bed and breakfast za Jo'burg, Pretoria, Gauteng. Ama mji wowote unaotaka kufikia. Utapata taarifa.

Angalizo: Maambukizi ya VVU ni zaidi ya 20%. Pia kuna high rates za multi-drug resistant TB.

Nakutakia heri.
 
OME123

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,459
2,000
Naenda Johanesburg je nikiandaa milioni moja kwa siku mbili zitanitosha kwenda na kurudi kwa hizo siku mbili?
 
G'taxi

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
4,829
2,000
Naomba mwenye uelewa kuhusu gharama ya kwenda Afrika kusini zikoje ukizingatia nauli ya kwenda na kurudi,kulala siku mbili hotelini je,kwa kukadiria inaweza kuwa shilingi ngapi za kitanzania.maana nataka niende huko kikazi wiki ijayo ila sijajua gharama zikoje?
Unaenda kikazi na haujajua gharama?rafiki acha basi masihara.tumefanya wote kazi za kuajiliwa na zilipokua zinakuja safari za hivyo kulikua kuna mchanganuo mzima wa gharama ili uchukue per diem yako,na unapewa hizo gharama kutoka huko huko uendako.sasa wewe ni mfanya biashara au ni vipi mpaka uulize huku jf?
 
BilioneaPATIGOO

JF-Expert Member
Jun 23, 2012
12,204
2,000
Ukitumia South African Airways ni Rands 4600/-. Hii ni return ticket. Unatumia jumla ya masaa sita angani. kwenda masaa matatu na kurudi vivyo hivyo.

Kwa basi nauli andaa wastani wa laki 5 hivi.

Usisahau yellow fever vaccine card.

Hotel unapata kuanzia TZS 50,000 hadi laki 5 kwa usiku mmoja. Google bed and breakfast za Jo'burg, Pretoria, Gauteng. Ama mji wowote unaotaka kufikia. Utapata taarifa.

Angalizo: Maambukizi ya VVU ni zaidi ya 20%. Pia kuna high rates za multi-drug resistant TB.

Nakutakia heri.
Duuh maambukizi % ngap?
 
segito wa kalenga

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
604
1,000
Nakushauri Upande Ndege Kama Una Mpango Wa Kurudi.Napendekeza Ndege Ya Rwandair Na Utalipia 4000 ZAR Return Ticket Au Chini Ya Hapo Ukibook Mapema.Usafiri Toka OR Tambo To Jozy Panda Gautrain Au Uber Utalipia 55 Rands.Hotel Bed Alone Pale Bree Kuanzia 150 Mpaka 300.Hope Nimesaidia
 
segito wa kalenga

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
604
1,000
Naenda Johanesburg je nikiandaa milioni moja kwa siku mbili zitanitosha kwenda na kurudi kwa hizo siku mbili?
Panda Taqwa Hadi Lusaka.Ukifika Panda Shalom Bus Hadi Joberg.Utalipa Kama Laki 2 Na Nusu.Mkononi Uwe Na Rand 1000 Show Money.Omba Dereva Akubukie Pa Kulala Pa Bei Rahisi.Ukifika Jobeg Wenye Basi Watakupeleka Hotel Mchezo Umeisha
 
cleokippo

JF-Expert Member
Dec 21, 2014
989
500
bado hujasaidia segito sababu hujaeleweka bado. ww unatutajia mambo ya 4000 ZAR na rand 150 mpaka 300 sisi tunayajua ayo? we tueleze gharama za kulala ni tsh flan na return ticket ni tsh fln apo kwel utasema umesaidia
 
Norton82

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
677

1 ZAR(South African Rand)= 170 Tanzanian Shillings, kwahiyo ni kuzibadilisha hizo rand zije kwenye pesa ya kitanzania.
 
Ntate Mogolo

JF-Expert Member
Jun 5, 2016
331
1,000
Nakushauri Upande Ndege Kama Una Mpango Wa Kurudi.Napendekeza Ndege Ya Rwandair Na Utalipia 4000 ZAR Return Ticket Au Chini Ya Hapo Ukibook Mapema.Usafiri Toka OR Tambo To Jozy Panda Gautrain Au Uber Utalipia 55 Rands.Hotel Bed Alone Pale Bree Kuanzia 150 Mpaka 300.Hope Nimesaidia
Msaada mkubwa sana kwangu. Umenifungua upeo wangu. Nitakuwa nasafari ya huko mwezi mei kuelekea Pretoria na kurudi nyumbani. Ahsante kwa uelewa wako.
 
segito wa kalenga

JF-Expert Member
Aug 28, 2014
604
1,000
bado hujasaidia segito sababu hujaeleweka bado. ww unatutajia mambo ya 4000 ZAR na rand 150 mpaka 300 sisi tunayajua ayo? we tueleze gharama za kulala ni tsh flan na return ticket ni tsh fln apo kwel utasema umesaidia
kama una nia ya kysafiri utagoogle exchange rate boya wewe.sio kila kitu utafutiwe.vingine jiongeze alaaah
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom