Gharama za kupiga plasta nyumba

Gharama za kupiga plasta nyumba

jengo

Member
Joined
Oct 16, 2012
Posts
75
Reaction score
8
wadau naomba kujua gharama za kupiga plasta nyumba ya vyumba vinne na sebule.
 
Inategemea na hali ya ukuta pia ukubwa wa vyumba vya hiyo nyumba
 
wadau naomba kujua gharama za kupiga plasta nyumba ya vyumba vinne na sebule.

Usituchoshe bure; katafute fundi ujenzi atakuelewesha ukishindwa tafuta quantity surveyors watakuwa wanajua!
 
square meter 1 bei halali ni 2000 mpaka 2200 ss basi pima nyumba yote ukipata vipimo toa madirisha.
 
Ungetaja eneo ilipo nyumba ingekuwa bora zaidi.Bei ya Naliendele ni tofauti na ya Kariakoo au USA.
 
Hizi mada zingine mnatusumbua vichwa tu! Hivi wewe mwenyewe huwezi kufikiri kuwa gharama huwa zinatokana na uwezo wako mwenyewe? Achenini usumbufu wazee!!
 
Unataka gharama ipi?;Fundi tuu au fundi +materials?.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Ukiwa na mifuko 20 ya cement inatosha. Mchanga fuso moja kubwa.
Maji lita elfu 4.
Fundi laki 3.

Utahitaji mbao za majukwaa ambazo sio lazima ununue, umeweza kuazima kwa jirani au mwambie fundi aimprovise.

Kumbuka kuwa mafundi wengi mkikubaliana kazi ya plaster huwa hawahesabii kiuno.
Kwahiyo kwenye makubaliano ya awali hakikisha mnawekana sawa kwenye hilo.
 
Kuna plasta na lipu,kuna niru na white cement kaz ni kwako,kwa vyumba 5 lipu andaa laki6
 
Back
Top Bottom