Ongezeko la asilimia mia (100%)Kuanzia tarehe 1 mwezi januari mwakani nauli ya kuvuka kwenda na kutoka kigamboni itakua shiling mia mbili kwa mtu mmoja,na gari zitatozwa sh elfu mbili!
Walalahoi tujipange kufunga mikanda,
Tunajua sana kubuni model ila kuweka structure i-exist?!
Daraja letu liko mbioni.
utazama wewe!
Wakati ukitafakari kuhusu hili la kivuko,tujiandae kuanzia january 2012 gharama za umeme juux3.Kama mmesoma makala ya Mbwambo kwenye Raia mwema wiki hii ametoa tahadhari ya umma kujiandaa na hali ngumu zaidi 2012 kuliko hii ya sasa kwani serikali imekwama haina tena mbinu mbadala za kujiongezea mapato zaidi ya kuwakamua wananchi.
Jk sijui tukuelewe je kwani kuna vitu havijawahi kupanda zaidi ya miaka 20 iliyopita japo hali ya maisha na kushuka thamani ya hela kushuka kama nauli ya wanafunzi ilikuwa sh. 50 kwa muda mrefu sana ila tangia uingie madarakani imepanda mara 2 kwenda mia na sasa 150 na nahisi mpaka uondoke madarakani 2015 kama waTz wataendelea kuwa wavumilivu yaani wasipokuondoa kwa nguvu ya uma tunategemea itakuwa zaidi ya 300, kivuko kinapanda bei ambayo ilidumu kwa muda mrefu tena inapanda kwakudable, Nishati za mafuta na umeme tunapata kwa mgao, je wanauchumi wako na uchumi uliosomea pale mlimani ndo ulikufundisha kuwa taifa linaendelea pasipokuwa na nishati kama hizi? Yafaa ujiulize na kuchukuwa uamuzi ambao utakuwa na faida kwa taifa na kuwafurahisha wengi kwakujiuzulu kwa manufaa ya taifa mliloliweka rehani mdomoni mwa simba mwenye njaa kali
Daraja letu liko mbioni.
nitaogelea bila nguo.
Nahama Mji Mwema wacha nikajibane na wahindi na kina FF katikati ya mji maana kukaa mbali foleni kero kigamboni niliona ujanja sasa inakuwa kero na kuogelea naogopa kuliwa na samaki mimi.
nitavukaje na demu wangu kuelekea mikadi beach.
Kimsingi sipingi ongezeko la bei za kivuko cha hapo kigamboni kwani garama za uendeshaji zipo juu sana kama ukiwa mdadisi mzuri. ila sasa kwa hao wakusanya ushuru nao wawe ethical isiwe wamepandisha bei mapato yakabaki yale yale
Lishakamilika kwenye michoro mkuu,hicho ndo tunachoweza.Daraja la NSSf litakamilika lini??