Gharama za Afya zinatuua wajenga nchi na walipa kodi

Gharama za Afya zinatuua wajenga nchi na walipa kodi

Santieli

Member
Joined
Apr 30, 2014
Posts
57
Reaction score
75
@(SPEAK LOUD KUELEKEA UCHAGUZI OCTOBER)

Ukweli ni kwamba kuumwa Ni sifa moja wapo ya mwanadamu, kuumwa hukukumbusha kuwa karibu na muumba.
Hutukumbusha pia duniani tu wapitaji... Kuumwa sio dhambi Wala mkosi Wala laana Ni Jambo ambalo hutokea karibuni kwa Kila tabaka, rika, rangi hadi kabila.....

Kuumwa kuna zorotesha maendeleo ya mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, kwa sababu nguvu kubwa huwekezwa kutafuta tiba na kupunguza uzalishaji wa mtu na mtu au taifa kwa ujumla...

Kuna maradhi madogo madogo na marafhi makubwa ambayo upatikanaji wake wa tiba Ni gharama kubwa ambapo hupelekea wale wenye kipato cha siku kuingia katika umaskini au madeni yasiyolipika na kupelekea kuuza radilimali zao na wasifanikiwe kutimiza au kumudu gharama za matibabu....

Baadhi ya gharama kubwa kwa baadhi ya maradhi Ni pamoja na;-

1. Kufungua faili hospital za mkoa zi chini ya 7000/= Tsh

2. Operation za mama wajawazito....

3. Gharama za kulazwa (kitanda)

4.Gharama za vipimo kama:- typhoid, full
blood picture, utra sound, x Ray, sukari n.k

5. Gharama za madawa na vifaa tiba

6. Uhaba wa wataalam katika hospital na zahanati.....

NB:- Kwa kuwa swala la utoaji wa huduma za msingi za kijamii kama afya, maji, umeme n.k Ni wajibu wa serikali ambayo wananchi huichagua kupitia kura na Kisha kushirikiana na sekta binafsi baadhi ya nchi kama USA wakaona ili kumkomboa mtu wa chini, mnyonge, maskini, mtu lengwa Basi kuna haja ya kuwa na Bima ya afya (OBAMA HEALTH CARE) itakayosaidia kushughulikia matatizo ya afya kwa wananchi wa kipato cha chini ambao Ni wengi zaidi na ndio wazalishaji wakubwa hususani Tanzania ambapo wanakadiriwa kufika 65% ya watanzania wote....

Hali hi imesaidia kupunguza idadi kubwa ya wanyonge wanaoshindwa kumudu gharama za afya na hivyo kuongeza uzalishaji kupitia shughuli zao za Kila siku bila kutetereka....

TANZANIA suala la bima ya afya liko chini ya serikali kupitia mfuko wa bima ya afya taifa (NHIF) ambao hutoa bima kwa watanzania wote ili kumudu GHARAMA za afya jatika mfumo jumuishi na shirikishi....

NHIF kwa walio mudu kujiunga nao hawana mashaka juu ya familia zao zinapo pata maradhi kwa kuwa swala la GHARAMA hata kama lipo juu kuliko ulichochangia bado zitakua covered under specific time of your membership na NHIF....

MADA ILIPOJIKITA:-

NHIF hutumiwa na wafanyakazi walio ajiriwa serikalini na taasisi binafsi na mwajiriwa hukatwa kiasi fulani cha pesa Kila mwezi kupitia mshahara wake (sijui Ni % ngapi) na hujumuisha watu Sita katika familia....

Pili kwa wale wasiowafanyakazi wa serikali au taasisi binafsi yaani mama ntilie, boda boda, wamachinga, wakulima, wafugaji n.k hawa huwaza kukata bima ya afya ya NHIF kwa mmoja mmoja au kwa familia .....

TATIZO LILIPO:-
Gharama za NHIF kupitia vifurushi vyake. (Tazama kiambatanisho hapa chini)....
Screenshot_20200731-180623~2.jpg



Gharama hizi kuwa juu kumepelekea 8.5% ya watanzania wote kuwa wanufaika wa mfuko huu na kuacha 91.5% kujihudumia wenyewe au kujiunga katika mifuko mingine kwa kiasi kichache sanaaa....

Hali hii ya kushindwa kumudu GHARAMA za kimatibabu zimepelekea

1. Vifo vingi vya watoto, wakubwa na wazee kwa kukosa huduma....

2. Ulemavu wa kudumu kwa kuchelewa tiba au kupata tiba zilizo chini ya ubora...

3. Kuongezeka kwa watoto wa mitaani kutokana na vifo vya wakezi wao kwa kushindwa kumudu gharama za matibabu...

4. Kusambaratika kwa familia na kutalikiana kutokana na malazi ta muda nrefu na kuongezeka kwa umaskini...

5. Kukithiri kwa rushwa za ngono ili kupata huduma...

6. Kushamiri kwa ushirikina na imani potofu kutokana na gharama kuwa juu...

7. Kuwa na taifa lenye nguvu kazi dhoofu kwa malazi yaliyo komaaa...


HITIMISHO LANGU:-

Kuelekea uchaguzi huu miongoni mwa vipaumbele vyetu watanzania iwe Ni kupaza sauti za kupunguza gharama za afya ili Kila mtanzania aweze kumudu gharama za afya na kuondoa wasiwasi wa maisha yetu linapo kuja swala la afya...

Mgombea au chama kitakacho kuja kunadi sera zake au ilani zake Basi tusiwe wavivu kupitia sera na ilani hizo kujiridhisha kama unafuu wa gharama za afya umepewa kipaumbele......

Mgombea akisimama jukwaani na asiseme hilo Basi aulizwe na atueleze mkakati wake na chama chake juu ya hilo na namna watakavyo litekeleza (impliment) .....

Ni wakati wetu sasa kupigania kuboreshwa na kupunguzwa kwa gharama za matibabu ili Kila mtu anufaike na huduma kupitia Kodi tunazolipa .....

Afya njema huleta maendeleo chanya na taifa lenye furaha.....

2020 Agenda
 
Back
Top Bottom