Gharama ya Tsh 53,000 ya check up kwa wafanyabiashara wa vyakula ni kubwa sana, wengi hawaimudu

Gharama ya Tsh 53,000 ya check up kwa wafanyabiashara wa vyakula ni kubwa sana, wengi hawaimudu

Emanueli misalaba

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2016
Posts
2,912
Reaction score
3,899
Wanajukwaa ni matumaini yangu kwamba ni wazima wa afya njema,

Ikiwa kuna miongoni mwenu hajisikii vizuri kiafya, Mungu Muumba, Mponyaj akujaalie uponyaji thabiti.

Kuna kitu nimekiona kwa muda mrefu, mimi naona hakipo sawa, kinaumiza sana, kundi la Mama Lishe, Wauzaji wa Chips, wanye Butcher, wauzaji wa Kachori, Makabaisa na Ulojo mitaani na kwenye Skuli mbalimbali.

Hawa watu kila baada ya miezi sita (6) wanatakiwa waende Migombani kwenye maabara iliyoamriwa kufanya MEDICAL CHECK UP Kwa wafanyakazi wote wa Umma na wale wa sekta binafsi, ambapo kwenye kundi la wafanyabiashara wadogo wadogo gharama zake ni elfu 53,

Na hapo hapo wafanyakazi wa kwenye makampuni ya Hotel za kitalii upande wa idara ya jikoni bei yao ni hiyo hiyo elfu 53 sawa na muuzaji wa Ulojo na kachori mitaani,

Hii si sawa, walio karibu na Mh Rais Dr Hussein Mwinyi nina wasihi hili jambo (Suala) walifikirie sana na wamshauri Mhe Rais elfu 53 kwa miezi sita na kwa mwaka ni laki moja na elfu 6, kwa hawa mama zetu na vijana wetu ni kubwa sana,

Hapo baadhi yao hawajalipia leseni, usafi wa takataka, kodi ya fremu (Mlango) umeme nk nk
Ninamsihi rais ashushe bei japo iwe elfu 20 au imepanda sana 25, then kwa mwaka iwe 40 au 50,

Na wenye mahoteli ya kitalii wenyewe ibaki hiyo hiyo elfu 53, kwa sababu mahoteli mengi hiyo hela huwarudishia wafanyakazi wao,

Nimewasikiliza mama lishe, wauza Kachori, Makabaisa, urojo, chips, Butcher kadhaa, hiki kitu kinawauma sana na hawajui waanzie wapi ili tu dukuduku lao alisikie Mh Rais na kuweza kulitatua,

Wanaomba ktk ile kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais "yajayo ni neema tupu" basi na kwenye shughuli zao za kuendesha maisha yao ya kila siku neema hiyo neema iakisi.

Shukurani sana
 
Mtoa mada pamoja na hiyo changamoto binafsi nimekuelewa vilivyo;
Huku bara tuliambiwa kila mtu ale kutokana na urefu wa kamba yake, kwa mantiki hiyo ukiona kwenye urojo unapunjwa ingia kwenye hotel za kitalii,
Lkn jamani, serikali ilione hilo, umesahau wahudumu wetu wa bar, the same quality of beer, mtaani elfu mbili, ukienda kwenye hizo hotel zao the same beer shilingi elfu 12, lkn kwenye vipimo vya afya tuko sawa, huenda hata kwenye kodi mko sawa,
THIS IS NOT FAIR
 
Back
Top Bottom