Gharama ya kuweka sakafu ya zege/rough floor

Amekupiga parefu sana, mara mbili yake. We agiza lori kubwa la kokoto, agiza roli la mchanga, nunua mwenyewe mifuko ya sumenti, halafu ahirisha kwenda kazini siku hiyo mwambie fundi leo tutafanya kazi pamoja na wewe.

Halafu uone kama hiyo gharama itafika. Mimi kwenye nyumba yangu siku wanafanya vitu vya maana, kuanzia umwagaji wa zege, nilikuwa siendi kazini, navaa nguo za kazi naenda kushinda hapohapo, wakiwa wanakoroga zege na mimi nakoroga, kubeba zege, kila kitu. Nimekuja kujua mafundi ni wezi sana.
 
Mkuu siku zote usiishie kuzungumza na fundi mmoja, jifanye unataka kumpa dili na fundi mwingine na mwingine, kupitia michanganuo yao utapata bei tofauti tofauti kwa kazi yako, hapo utajua ni bei gani usimamie.

Japo usipende kuwagalaliza sana, fundi anaweza kukupa hesabu nyepesi ili umpe tu kazi apate mkate wake.
Bei za mafundi pia hutegemea na eneo husika, fundi anayejenga site za Masaki, Oysterbay gharama zake hazitakuwa sawa na anayejenga Kwa mfuga Mbwa.

Yote kwa yote,gharama hzo zipo juu sana,kuna mdau ameshauri hapo juu,fundi akupe mchanganuo wa idadi ya mafundi na vibarua watakao ifanya hiyo kazi na siku watakazotumia kuikamilisha hiyo kazi then itakua jukumu lako kuupima huo mchanganuo,ila pia utapaswa kujua kupiga plasta per room ni bei gani? Japo ukubwa wa room unatofautiana ila bei hazitaachana sana,Sio fundi akupe tu bei ya jumla ya kazi.

Nawasilisha...
 
Hawa jamaa wanataka kunifanya mimi babu yao.

Kwenye upauaji walitaka kunipiga materials, nikakaba mpaka penalt baada ya kupata mwongozo kutoka humu jukwaani.

Sasa hivi nd'o wananiseti ili wanipige upande wa labour charge,
Ni mafundi wazuri kiujenzi, Ila watakosa kazi kwa kuendekeza tamaa.
Ngastika machale kundesa
 
Yaani rough flour pamoja na skimming ni laki 9 au laki Tisa kwa hiyo kazi moja tu?
Note: Bei ya ufundi itatokana na njaa ya fundi au jinsi alivyo maarufu na si ubora wa kazi.
Huyo fundi yuko juu , mtafute mwingine . Kama uko Chanika na viunga vyake nikuunganishe na mafundi bora wenye gharama nafuu.
Kuna fundi kutoka Bunju kaja Chanika kanitajia bei za ajabu nilimpata fundi aliifanya ile kazi vizuri kwa pesa ambayo ile aliyoitaja za Bunju unazidiaha mara 2 na nusu ndio ifanane
Mimi nipo mkoa wa Pwani mkuu.
Ila ushauri wako nauzingatia kabisa.
Hizi hela za ujenzi hata sisi tunadunduliza na kujinyima sana, Ila ndugu zetu mafundi wanataka kutulalia.
 
Mimi alinichana jamaa kuwa mzee ulivyochomoka kula wamepita na mifuko hapa nmeoma miwili me ilinikata moto kweli

Nikawa nasubiri kuona mwisho wa kazi sikuridhishwa

Akaanza kunipa hesabu za plasta na nini nikamwambia respect yourself hatuwezi fanya lazi za kuchungana kama watoto natafuta fundi mwingine

Hakua amenielewa ila ataona nitakavyoanza plasta vitu vitapita kwake ila kazi hatoiona
Kama fundi amebainika kakuibia vifaa, hafai kupewa kazi tena huyo.

Na itapoanza kazi ya plasta, akija kukuulilza "Boss vipi kuhusu kazi?"
Mwambie ukweli kuwa
"Niliacha vyanzo vya taarifa za kiintelijensia na kubaini wizi wa wazi wa vifaa vyangu na hivyo kuharibu kazi yangu,
Hii imekupotezea heshima na uaminifu wako pia"
 
amekupiga parefu sana, mara mbili yake. we agiza lory kubwa la kokoto, agiza roli la mchanga, nunua mwenyewe mifuko ya sumenti, afu ahirisha kwenda kazini siku hiyo mwambie fundi leo tutafanya kazi pamoja na wewe. halafu uone kama hiyo garama itafika. mimi kwenye nyumba yangu siku wanafanya vitu vya maana, kuanzia umwagaji wa zege, nilikuwa siendi kazini, navaa nguo za kazi naenda kushinda hapohapo, wakiwa wanakoroga zege na mimi nakoroga, kubeba zege, kila kitu. nimekuja kujua mafundi ni wezi sana.
Asante sana mkuu.
Kwenye kipengele cha kuwepo saiti hapo niko vizuri.
Nitakomaa nao liwake jua, inyeshe mvua.
 
Mkuu siku zote usiishie kuzungumza na fundi mmoja,jifanye unataka kumpa dili na fundi mwingine na mwingine,kupitia michanganuo yao utapata bei tofauti tofauti kwa kazi yako,hapo utajua ni bei gani usimamie.
Japo usipende kuwagalaliza sana,fundi anaweza kukupa hesabu nyepesi ili umpe tu kazi apate mkate wake.
Bei za mafundi pia hutegemea na eneo husika,fundi anayejenga site za Masaki,Oysterbay gharama zake hazitakua sawa na anayejenga Kwa mfuga Mbwa.
Yote kwa yote,gharama hzo zipo juu sana,kuna mdau ameshauri hapo juu,fundi akupe mchanganuo wa idadi ya mafundi na vibarua watakao ifanya hiyo kazi na siku watakazotumia kuikamilisha hiyo kazi then itakua jukumu lako kuupima huo mchanganuo,ila pia utapaswa kujua kupiga plasta per room ni bei gani? Japo ukubwa wa room unatofautiana ila bei hazitaachana sana,Sio fundi akupe tu bei ya jumla ya kazi.
Nawasilisha...
Nimekusoma mkuu,
Baada ya kununua mchanga na kokoto,
nitafanya maulizo kwa mafundi kadhaa kabla ya kuanza kazi.
 
Kama fundi amebainika kakuibia vifaa, hafai kupewa kazi tena huyo.

Na itapoanza kazi ya plasta, akija kukuulilza "Boss vipi kuhusu kazi?"
Mwambie ukweli kuwa
"Niliacha vyanzo vya taarifa za kiintelijensia na kubaini wizi wa wazi wa vifaa vyangu na hivyo kuharibu kazi yangu,
Hii imekupotezea heshima na uaminifu wako pia"
Nitakapoanza tu najua atajileta maana ni karibu na eneo la ujenzi ataipata habari yake.

Me huwaga navunga tu mtu akifanya ujinga/wizi nikajua ila akija kujizima data hapo ndio nakua mkali.
 
Asante sana mkuu.
Kwenye kipengele cha kuwepo saiti hapo niko vizuri.
Nitakomaa nao liwake jua, inyeshe mvua.
Uwe makini lakini, unaweza kuwepo hapohapo wakakuibia vilevile, mimi sumenti niliweka kwenye kapikapu kangu, ikatulia, wanachana mfuko mmoja, nawapa mwingine hadi ilivyoisha. Mabaki ya mifuko nakuwa nayo na nahakikisha hawanibambikii. Wanao uwezo ukiwa umeenda washroom wakaleta mfuko uliochanwa wakauweka pale na mfuko mzima wa sumenti wakapeleka nyumba ya jirani.

Unaona kama hela ni ndogondogo lakini wakifanya hivyo kwa watu kadhaa wanapata mifuko mingi tu, same applies kwenye nondo. Mmoja aliwahi kuniletea dili la nondo karibia 20, badala ya 24k kila nondo anataka aniuzie 19. Nilimuuliza umetoa wapi, akasema kuna jamaa zake walikuwa wanajenga ghorofa sehemu sasa zimebaki, ni za kwao wala sio za wizi nisiogope. Nikajiuliza, huyu tajiri mjenga ghorofa wanamuibia huko sijui ni nani?
 
Kwa ufupi plaster chumba kimoja ni kati 50,000-70,000 na rafu 30,000-50,000 kwa ndani. Sebule, dining na jiko hesabu kama chumba kila kimoja.

Korido na vyoo inategemea na ukubwa unaweza vichanganya vikawa chumba kimoja. Pia bei inategemea na eneo na hadhi ya fundi.
 
Nyumba ina ukubwa wa mita 14 kwa 12.5,

Ina vyumba 3, Sebule 1, Dinning room na jiko.

Fundi ameniambia labor charge ya kuweka zege/rough flow ya inchi mbili nyumba nzima ni 500,000/-,

Na ya kupiga plasta (ndani tu) ni 900,000/-.

Kwa uzoefu wenu, ni bei stahiki au anataka kunipiga?

Kama kawaida, ni lazima nilete kesi na changamoto zote zote za ujenzi katika jukwaa hili mpaka hitimisho lipatikane.

Weka total square meter za floor
Weka total square meter za ukuta wa ndani tukusaidie
 
Back
Top Bottom