Utalipa transfer fee ya 1% ya gharama ya kununua gari( mkataba wa mauziano utaonesha), plus stamp duty Tshs.10,000 na kuna shs. 60,000 nyingine (sikumbuki inaitwaje) so simply Tshs.70,000 plus 1% ya gharama ya kununua gari.
Uende na tin number,mkataba uliosainiwa na hakimu,kadi original, fedha tasilimu si chini ya laki moja kutegemeana na fefha uli;nunulia gari yako(iliopo kwenye mkataba).
Kumbe ni hakimu mie najua kuwa mkataba wa mauziano ambao umesainiwa na mwanasheria anaye tambulika na serikali au kiongozi wa serikali labda niongezee elimu hapo mkuu
Bila shaka, kwa sababu TRA wanasema:-
"Kodi ya kubadili umiliki wa chombo cha moto inalipwa wakati chombo kinapobadili mmiliki kutoka mtu mmoja kwenda mwingine. Kodi ya kuhamisha inalipwa na mmiliki mpya na ushuru wa stempu 1% unalipwa na muuzaji. Kodi hizo zinalipwa benki."