Gharama hizi za maziko lengo lake nini hasa?

Fortilo

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
5,008
15,611
Habari wakuu,
Kuna wakati mwingine ukifikiria namna gani watanzania tuliowengi tunavoishi, kichwa kinauma na unatamani hata usiwe miongoni mwa jamii hii..... kwakuwa hata usipopenda, chain of reaction lazima ikufikia na lazima uumie kwa kiwango chako....

Ni jana tu tumetoka kumpumzisha mfanyabiashara mmoja, Milionea aneingiza makampuni kadhaa ya madawa hapa nchini alieuwawa na watu wasiofahamika, kabla ya hapo tulimpumzisha mwingine tena ambaye alifariki kwa kifo cha asili( sio lengo la uzi huu kuzungumzia vifo hivyo)

Nimetiwa faraja sana na namna miili hiyo ilivopumzishwa a hasa ukiangalia gharama zake hadi mwisho wa maziko...(Kumbuka hapa nazungumzia mamilionea)
Kwanza watu waliojitokeza inatia moyo, pili ni gharama za waliomsindikiza hadi kuhifadhiwa kwenye nyumba zao za mwisho....

Gharama zisizoelezeka kwa ndugu wa walioondokewa kwa wapendwa wao
Kama kawaida
1. Matarumbeta na kwaya za haja....
2. Miziki ya nguvu kubwa na maspika makubwa
3. Watu wakiwa na sare zenye picha za alieondoka..(Kumbuka msiba wa mamilionea)
4. Mavyakula ya kula na kusaza, kusambaza..ma bieere na masoda kwa kwenda mbele na mapilau na viazi ya kutosha...(Millionea mwenye mali ndio alieondoka)
5. Wachungaji/Viongozi wa dini wengi..kusalisha(Kama kawaida tulivyozoea wenye pesa tena)
6. Nyama za kutosha..wanasema kufa kufaana bwana
7. Rambi rambi za kukata na shoka...... michango hadi pomoni.....(Mamilionea hadi wazungu na wachina niliwaona)

Kilichonishangaza
1.Hakuna cha tarumbeta wala uniform wala miziki wala chakula kwa yeyote pengine ili kupendezesha msiba, (Kumbuka msiba ni jambo la huzuni)
2. Hakuna magari wala msururu wa magari yakusindikiza msiba, ni ambulance moja tu iliyoleta mwili bas...... magari private yalipakiwa ngambo kabisa
3. Hakuna cha wachungaji wanaoomboleza msiba wa matajiri na ule wa mafukara wakaachiwa viongozi wadogo wa sehemu za ibada.
4. Hakuna mbwembwe, ni sala moja tu basi, mwili unapumzishwa unapostahili
5.Hakuna rambirambi za kuwalipa waongoza ibada..hakuna
6. Hakuna camera na picha zisizo na kichwa wala miguu wakati wa maziko..hakuna....
Kwa kweli imenishangaza sana..... wao mamilionea wameshindwa nini? sisi tunaweza nini na michango isiyoisha kuibebesha familia mzigo mwingine wasio ustahili?

Ikumbukwe pia kuwa tayari ndugu wana uchungu kwa kuondokewa na mpendwa wao. kinachoumiza zaidi ni gharama wakati wa maziko ambazo nazo kwa ujumla wake hubebwa na ndugu hao hao.... yani msiba mara mbili.....
Hivi kuna ulazima wowote kwenye hili kweli?
Uniform zenye picha za rangi na majeneza ya gharama, hivi kuna umuhimu wa vitu hivi kweli?
Hivi aliefariki anajali kuwa amezikwa kwenye jeneza la namna gani? au nani alivaa nini?
Kama jamii hatuna haja ya kubadili mtizamo huu potofu kweli?
Imefika mahali watu wanaogopa kwenda kwenye maziko kukwepa gharama...
Huu utamaduni wa hovyo hivi tumerithi wapi?
Mbona biblia haisemi hayo? au hata Quran haina mambo ya namna hiyo....
Jamii yetu ni maskini sana, kwanini tunapenda mambo ya sifa za kijinga ingali hatujiwezi kabisa kiuchumi...?
Nirudi kwa hao mamilionea, yani baada ya maziko ndugu wa karibu wa alieondoka... walijipanga tu kwenye viti na kutakiana mkono wa pole na ukawa mwisho wa habari ya maziko na watu kutawanyika.....
Hivi kweli walishindwa kuweka ma camera, mafualana, ma robot ya kubeba jeneza n.k.....
Hivi jamii yetu inafikiri sawa sawa kweli?
Tunaiga utamaduni wa wamerikani na wazungu, hivi kweli tunafanana na watu hao kwa lolote kweli? kwani lazima tuendeleze utamaduni huo?
Najiuliza tu kwa sauti.
(Image za google hapo ni mifano tu, na haina nia ya kusababisha usumbufu kwa yeyote....BTW nimetumia picha za misiba maarufu huko marekani)

Wasalaam,
BIG FUNERAL.jpg
10-of-the-most-expensive-caskets-and-coffins-in-the-world-2.jpg
Mohamed Alii Funeral.jpg
 
Bora matajiri waanze kujishusha maana watu wa vipato vya kawaida hujitutumu ili kugh'arisha shughuli ili hali hawana pumzi.
Na harusi zishuke bei jamani!
 
Nawakubali sana waislamu japo mimi sio muislam.. ..kwenye misiba yao wala hakuna mbwembwe za maandamano, cjui matarumbeta, cjui suti, cjui upuuuz gan.... Hawana mazoea ya kipuuz, kufa saa 2, ikifika saa 10 upo kaburini, jaman wakristo tuacheni sifa za kijinga jaman
 
Bora matajiri waanze kujishusha maana watu wa vipato vya kawaida hujitutumu ili kugh'arisha shughuli ili hali hawana pumzi.
Na harusi zishuke bei jamani!
Mkuu unadhani zaidi ya michango isiyohitajika kuna lolote kweli?
Hivi lazima watu wale msibani?
Hilo la harusi ndio balaa zaidi.
 
Kipindi ninakua niliwahi kuwaza labda nitafute hela niwe nazo nyingi ili siku ninakufa badala ya watu kulia waje kunisindikiza tu wacheze playlist ya miziki ninayoipenda wanywe wale nikapumzishwe....ila hio ilikua ni imagination tuuu.....
 
Back
Top Bottom