JUSTIN MPOTWA
Member
- Jan 16, 2013
- 16
- 11
Tunaendelea na majadiliano juu ya hoja ya wenzetu wa Mtwara na Lindi kulilia gesi iliyopatikana kwao iweze kuwanufaisha kwao.
Nilifuatilia vizuri taarifa iliyotolewa na wizara ya nishati na madini kwa vyombo vya habari. Iliandikwa kisayansi sana na ilikua ni ya kitaalamu sana.
Jambo linalonifanya niachangie mjadala huu ni sentesi moja katika moja ya aya za taarifa hiyo. Nigependa niinukuu sentensi hiyo ili wasomi wote tui "judge" kulingana na ilivyoandikwa. Sentensi yenyewe inasema, "Hatutarajii mikoa hii nayo ifanye maandamano ya kutaka kuhodhi raslimali za Gesi Asilia na Mafuta zitakapogunduliwa mikoani mwao."
Sentensi hiyo ni mwendelezo wa "paragraph" iliyokuwa inaelezea baadhi ya mikoa ambayo inadalili ya kuwa kunauwepo wa Gesi asilia na Mafuta. Hebu tuitazame mikoa ambayo imetajwa na Taarifa:Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Manyara, Kigoma, Mbeya, Njombe, Rukwa, Katavi, Morogoro na Tabora.
Hapa naanza kuuliza maswali kwa aliyeiandaa taarifa
1. Je wizara, kila itakapokuwa inagundua hazina ya gesi asilia au mafuta katika kila mkoa uliotajwa kwenye taarifa, itafanya kama inavyotaka kufanya huko lindi na Mtwara?
2. Wizara iseme ni nini kinachoshindikana kuweka mitambo ya kusambazia gesi tokea pale inapopatikana?
3. Endapo kutatokea Majanga ya kiasili huko katika jiji la Dar es Salaam ambayo mara nyingi huaribu miundombinu , Wizara ituambia imejipanga vipi kukabiliana na yatokanayo?
kwa mtazamo wangu: tutoke katika kufanya mambo yetu kwa mazoea! Tumefika katika umaskini uliodumaa kwa kutafuta kutatua matatizo yale yale, kwa njia zile zile huku tukitegemea kupata matokeo mapya!
TUBADILIKE, NA SASA WIZARA YA NISHATI NA MADINI IWE MFANO!