Gesi yaanza kutumika Tanzania

Gesi yaanza kutumika Tanzania

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,037
Reaction score
34,741
141023150122_gas_pipeline_640x360_getty_nocredit.jpg

Mitambo ya gesi

Shirika la maendeleo ya Petrol nchini Tanzania limesema kuwa Mradi wa Gesi iliyogunduliwa kusini mwa nchi hiyo mkoani Mtwara umefikia asilimia 94 na tayari gesi hiyo imeanza kutumika katika baadhi ya maeneo.

Hadi sasa kuna baadhi ya viwanda, na mashirika ambayo yameanza kutumia gesi hiyo asilia hatua inayodaiwa kupunguza gharama za upatikanaji wa Nishati kwa baadhi ya wakazi ambao wamekuwa wakitumia gharama kubwa ili kupata Nishati .

Gesi yaweza kuwa ni mkombozi na rafiki kwa mwanamke kwa kumkomboa kutokana na matumizi ya mkaa na kuni kwa muda mrefu, hasa upande wa kuni, miaka kadhaa baadaye wanawake huwa na macho mekundu na hivyo kuhiziwa kuwa wachawi hasa

kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza Nchini Tanzania na kushuhudia mauaji ya vikongwe yasiyokwisha.
Gesi ikiuzwa kwa gharama nafuu itamkomboa mwanamke na hatari ya kifo,kutokana na matumizi ya nishati ya jadi ,kuni yenye

madhara maishani kutokana na dhana potufu ya ushirikina kwa mwanamke mwenye macho mekundu kudhaniwa ni mshirikiana.

Nishati ya mkaa huharibu mazingira kutoakana na ukatwaji miti hovyo bila ya kupanda miti,lakini nishati hiyo imepanda bei hadi

kufikia tshs elfu tisini kwa gunia lla lumbesa, na kuni nazo ni adimu mjini, lakini kijijini nafuu kiasi kama hakuna uharibifu mkubwa wa misitu.

Suala la miradi mikubwa kama wa gesi hutawaliwa na rushwa na hivyo kuongeza bei ya nishati hiyo na kusababisha watu wa hali ya chini kutomudu kunufaika na nishati hiyo na kuonekana ni nishati ya baadhi ya watu.

Chanzo:
BBC
 
Juzi si nimemsikia mkurugenzi mkuu wa ewura akisem kuwa mradi wa gesi umekamilika kwa asilimia 78? Na akasema kuwa hadi mwezi june mwaka huu utndazaji wa bomba utakuwa umekamilika?au gesi hii gesi gani? Ni kiwanda gani kimeanz kutumia hiyo gesi? Ya mnazibay?au
 
Mi nijuwacho TBL wanatumia gesi ... sasa imetoka upande upi hapo sijui..
 
Ngoja tuvumilie mpaka hiyo june tuone mambo yatakuwaje!
 
Mitambo ya gesi

Gesi yaweza kuwa ni mkombozi na rafiki kwa mwanamke kwa kumkomboa kutokana na matumizi ya mkaa na kuni kwa muda mrefu, hasa upande wa kuni, miaka kadhaa baadaye wanawake huwa na macho mekundu na hivyo kuhiziwa kuwa wachawi hasa

kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza Nchini Tanzania na kushuhudia mauaji ya vikongwe yasiyokwisha.

Gesi ikiuzwa kwa gharama nafuu itamkomboa mwanamke na hatari ya kifo,kutokana na matumizi ya nishati ya jadi ,kuni yenye

madhara maishani kutokana na dhana potufu ya ushirikina kwa mwanamke mwenye macho mekundu kudhaniwa ni mshirikiana.

Hapo kwenye blue, ni uongo mtupu...
Hao TPDC mpaka sasa hawajashusha bei ya mafuta ya petrol na diesel, huku bei za bidhaa hizo zikiwa zimeshuka nchi jirani zetu.
Kwenye gesi asilia hali itakua kama ilivyo kwenye mafuta, bei itakua juu, na watu wataendelea kutumua kuni na mkaa.
 
bado haijaanza kutumika wana uza nje toka mwaka jana.
 
Hapo kwenye blue, ni uongo mtupu...
Hao TPDC mpaka sasa hawajashusha bei ya mafuta ya petrol na diesel, huku bei za bidhaa hizo zikiwa zimeshuka nchi jirani zetu.
Kwenye gesi asilia hali itakua kama ilivyo kwenye mafuta, bei itakua juu, na watu wataendelea kutumua kuni na mkaa.

kWENYE blue pale wamesema ... gesi yaweza kuwa mkombozi.... yaani kwenye lugha inaitwa hali isiyotimilika...... na hawajasema gesi imekuwa mkombozi...... na hapo kwenye lugha inaitwa hali iliyotimilika....

Hivyo yawezekana baadaye hali zitakuwa bora kwa habari ya nishati ya gesi......
 
Hadithi za alfu lela ulela hizi... gesi haiwezi kua mkombozi tanzania hii yenye panyabuku wenye uchu wa kutafuna rasilimali zetu bila huruma
 
Back
Top Bottom