Gesi asilia kuendelea kumnufaisha mtanzania

wa hapahapa

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
7,455
4,388
Shirika la TPDC limekuwa likisimamia shughuri na miradi mbalimbali inayohusu utafutaji, usambazaji na uzalishaji wa mafuta ya nishati na gesi asilia.

shirika limekuwa na miradi minne ktk kusimamia matumizi ya gesi asilia
- matumizi ya gesi ktk kuzalisha umeme
- matumizi ya gesi ktk viwanda.
- matumizi ya gesi kwa nyumbani,mahotelini.
-matumizi ya gesi ktk vyombo vya moto.

napenda kuongelea matumizi ya gesi ktk vyombo vya moto kama magari, pikipiki, genereta. huu ni mradi ambao ni mpya utakao mnufaisha mtanzania moja kwa moja.

ni wakati na fursa kwa wale wenye magari yanayotumia petrol kuweza kuongeza matumizi ya gesi asilia ktk magari yao.

gesi asilia inapatikana hapa tanzania, ni nafuu na ni mbadala wa mafuta.

source: watalaam wa TPDC ktk kipindi cha RFA.
 
Unaongelea tpdc au tpdf ni vitu tofauti kama mchanga Na sukari halafu kama ni gas ya adili ujue procces ya kuigeuza kuwa LPG bado sana.. Ges tunayotumia majumbani sio Ile ya asilia
 
Gas inayopatikana kwenye mitungi kwasasa kwaajili ya matumizi ya nyumbani sio gas asilia bali ni moja ya zao la usafishaji wa mafuta na inatoka uarabuni nasio mtwara na bei yake inatokana na soko la dunia kama petroleum.
 
Mkuu nifafanulie kwanza, ina maana unaweza acha tumia petroli na badala
yake ukatumia gesi kwenye gari?
 
thibitisha
 
Gesi itatunufaisha vp? Na lini? Mbona hatuoni hizo promises zikimaterialise? Vp kuhusu ile escrow ya bomba la gesi wameitatua vipi au ndio funika kombe mwanaharamu apite? TPDC bado haijapata mtu agressive na anayejua watanzania wanatamani nini!! Magu amulike hii inshu gesi na mafuta kuna ukanjanja mwingi ndani yake,hakuna transparency kabisa.
 
Nchi kuona rasilimali zinamfaidisha mzawa ndo itakuwa bismillah.maana kuna maselfish au maselfie
 
mm toka ile ya mtwara wanatuambia itaondoa tatzo LA umeme nchini na kupotelea kusikojulikana cna hamu tena na maigizo ya nchi hii
 
unaleta mada ambayo haina maelezo ya kutosheleza na wala haiendani na kichwa chake. Ebu dadavua vizuri kile unachotaka kusema.

magari yanayotumia petroli yanawaweza kutumia na gesi asilia inayopatikana hapahapa nchi....

yaani gari litakuwa na mifumo miwili wa matumizi ya gesi asilia na mafuta ya petroli.
 
Mkuu nifafanulie kwanza, ina maana unaweza acha tumia petroli na badala
yake ukatumia gesi kwenye gari?

mkuu.

mfumo wa matumizi ya petrol unaendelea kuwepo. hivyo gari litakuwa na mifumo miwili wa gesi asilia na petroli. ni maamuzi ya mtumiaji kutumia mfumo gani.

huu mradi ni mpya, na unapatikana dar.
 
Gesi itatunufaisha vp? Na lini? Mbona hatuoni hizo promises zikimaterialise? Vp kuhusu ile escrow ya bomba la gesi wameitatua vipi au ndio funika kombe mwanaharamu apite? TPDC bado haijapata mtu agressive na anayejua watanzania wanatamani nini!! Magu amulike hii inshu gesi na mafuta kuna ukanjanja mwingi ndani yake,hakuna transparency kabisa.

ukifuatilia faida ktk gesi asili inakwenda wapi au nani anamiliki haya makampuni ya gesi.... ni pasua kichwa.
 
thibitisha

gesi asilia bado haijaanza kuuzwa kwenye mitungi kwa raia.

kinachofanyika sasa ni kuweka mtungi mkubwa ambao umeunganishwa na vifaa vya matumizi ya gesi asilia. na huo mtungi hujazwa kupitia magari. mfano nyumba za tpdc zinatumia utaratibu huu.
 
Back
Top Bottom