(Germany 6th world Super-Supremacy empire) Ujerumani Dola-Kuu ya ulimwengu katika 1800 - 1945

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
351
866
06ca48dba2fa57f40d14f7679f139f71.jpg

HII NDIO GERMANY (UJERUMANI) ILIYOKUWA DOLA-HIMAYA NA MILIKI KUU YA SITA YA DUNIA "Popular-Super power" (THE 6th WORLD SUPER-SUPREMACY EMPIRE) KATIKA ULIMWENGU WA KIBEBERU NA KIFASHISTI 1800s - 1845 (WORLD OF IMPERIALISM AND FASCISM "The policy of extend power in World of Captalism").

Na, Comred Mbwana Allyamtu.

Mwanzoni Mwa miaka ya 1800 kuliibuka Kiongoz shupavu aliejenga Dola-Kuu ambalo baadae lilitamalaki balani uraya na kutawala Dola nyingine nyingi balani ulaya. Kiongozi Huyo alifahamika kama Otto Von Bismarck ndio anayetajwa kama kiongozi aliyoionganisha taifa la Ujerumani tunaloliona likiishi leo. Katika andiko la Leo kauri hii yake ndio itakayokuwa msingi wa makala hii yangu ambayo kauli hiyo aliyeitoa mwaka 1862 alisema....

da6f7591444b0c3e37528560e7d765fd.jpg

"Not through speeches and majority decisions will the great questions of the day be decided - that was the great mistake of 1848 and 1849 - but by iron and blood" - (Otto Von Bismarck) Kauli hii ilitajwa mwaka 1862 katika bunge la nchi ya Prussia ambapo mataifa yanayotengeneza nchi ya Ujerumani yalitaka kutengeneza muungano kwa njia ya kidemokrasia.

Ikumbukwe hadi kufika mwaka 1871 Ujerumani ilikuwa ni muunganiko wa mataifa madogo zaidi ya 300 ambayo yaliunganishwa kwa mtutu wa bunduki. Katika kauli ya hapo juu ilitolewa na mwanasiasa wa Prussia ambaye alikuja kuwa Waziri mkuu na kansela wa Ujerumani pindi ilipomaliza kuungana. Alisema "Ujerumani kama taifa haliwezi kuunganishwa kwa kutumia njia za kidiplomasia bali kwa damu na chuma." Maneno hayo yalionekana ni ya kishujaa kwa wakati ule na hata kwa vizazi vijavyo. Ujerumani ndiyo taifa pekee duniani ambalo hadi sasa limeweza kupigana vita na mataifa mengi wakati wa muunganiko wake bila kushindwa vita hata moja. Kuanzia miaka ya 1814 baada ya taifa la Ufaransa kupoteza nguvu na ushawishi wa kijeshi baada ya Mfalme Napoleon Bournaparte kushindwa vita ya Waterloo, nchi kama Austria, Denmark na Prussia ndizo zilikuwa na nguvu barani Ulaya.

Ila Prussia iliweza kupigana na mataifa hayo yote mawili yalikuwa na nguvu Ulaya na kufanikiwa kuliunganisha taifa la Ujerumani. Toka kipindi cha mwaka 1871 hadi mwaka 1914 wakati wa vita ya kwa kwanza ya dunia. Wajerumani waliamini taifa lao lina damu ya kipekee hasa ukikumbuka katika historia makabila ya kijerumani yalichangia sana kuangusha dola ya Mrumi. Kauli ya Otto Von Bismarck ilisemwa kwa nia njema sana lakini ilikuja kuleta laana kwa vizazi vingi vya baadae nchini Ujerumani.

Adolf Hitler aliitumia ile kauli kuwaahidi Wajerumani kwamba nchi yao itarudi katika Utukufu wa mwanzo na zaidi kwasababu hawatatawala tu Ulaya bali dunia nzima. Aliwaaminisha Wajerumani kuwa wao ni taifa teule na wahenga wao ndiyo biandamu halisi na mataifa mengine si kitu. Hitler alitamani mambo makubwa mengi, alitaka kutawala kuunganisha madola yote ya Ulaya lakini ikashindikana. Ikumbukwe hata Rumi ilikuwa kubwa lakini haikutawala dunia nzima.

Mfalme Alexander Mkuu wa Ugirki na Mfalme Napoleon wa Ufaransa walijaribu lakini hili halikuwezekana. Hitler aliamini kwamba yeye angeweza kufanya mambo ambayo wafalme wa dunia hii walishindwa huko nyuma. Kitu kimoja cha kukumbukwa na ambacho hata kwenye madarasa ya historia huwezi kukisoma ni kwamba Hitler pamoja na ukorofi wake wote aliwachukulia Wafaransa na Waingereza kama ndugu zake wenye damu moja . Wote hawa walikuwa ni Saxons au Makabila ya Kijerumani.

THE AGE OF APPEASEMENT AND FUTILE PEACE.

"With two lunatics like Mussolini and Hitler you can never be sure of anything. But I am determined to keep the country out of war" April 1936 yani ...“Huwezi kutegema chochote kutoka kwa wendawazimu kama Mussolini na Hitler. Lakini ninatakiwa kuiepusha nchi yangu na vita” April 1936. Hii ilikuwa ni kauli ya Aliyekuwa Waziri Mkuu wa Uingereza kwa wakati huo, bwana Stanley Baldwin. Baada ya Hitler kuchukua madaraka Ujerumani alijenga mazingira ambayo yatamfanya awe na ushawishi mkubwa Ulaya kuliko taifa lingine lolote. Ulaya ilikuwa imeharibika kiuchumi na hawakutamani vita kwasababu waliona madhara ya vita ya kwanza ya dunia.

Hitler alitumia hofu hii pamoja na huruma kwamba Ujerumani ilionewa kwenye Mkataba wa Versailles huko Ufaransa mwaka 1919 ili kufanikisha mambo yake. Ukweli unaoshangaza ni kwamba baada ya mkataba kuisha mwaka 1919 huko Ufaransa Mkuu wa majeshi ya Ufaransa Marshal Ferdinand Foch alinukuliwa akisema “ Huu siyo mkataba wa Amani, bali ni mkataba wa kusitisha tuu mapigano kwa miaka 20” Alitabiri hivi akijua kwa mwenendo wa nchi za Ulaya vita nyingine lazima ingetokea tu, na kweli hakukosea. Aliamini Ujerumani itakuja kuinuka tena na kuleta madhara hivyo aliwaonya sana mataifa ya Ulaya kwamba huu mkataba ni adhabu ndogo sana kwa taifa jehuri kama Ujerumani.

9598e4428e912ec68665303cb989ac8c.jpg

Ferdinand Foch aliichukia Ujerumani kwasababu ilikuwepo kwenye Vita ya mwaka 1871 ambapo Mfaransa alipigwa na kunyang’anywa majimbo mawili muhimu. Tena kwenye vita ya kwanza alishuhudia jinsi Ufaransa inapata kipondo kutoka kwa Mjerumani. Ukiangalia kwa undani haya mambo, utagundua tatizo lilikuwa si Ujerumani wala Hitler tatizo lilikuwa ni mfumo wa kibepari ambao mataifa ya Ulaya yalijijengea. Wazungu walijisikia utukufu sana pindi wakiona taifa lao ni tajiri kuliko jingine.

Frantz Fanon mwanazuoni mweusi wa Ufaransa anasema chanzo cha vita siyo Mjerumani bali ni mfumo wa kibepari. Ukiangalia katika masuala ya kiuchumi hasa katika ngazi za kimataifa utakuja kugundua kwamba mbali na sababu za kisiasa, kiutamaduni na kijamii vita za dunia zilisababishwa na mvutano wa kiuchumi huko Ulaya. Mfano mzuri hadi mwaka 1870 kulikuwa hakuna taifa la Ujerumani, uchumi ulikuwa chini ya Muingereza, Mfaransa na Austria. Ujerumani ilivyoinuka basi hii ikapelekea kuongezeka kwa changamoto za kimasoko huko Ulaya.

Mwaka 1933 Hitler aliitoa Ujerumani kwenye Umoja wa mataifa. Ambao ulikuwa na mkataba kwamba kila jambo litafutiwe suluhu bila vita. Aliamini kwenye kauli ya Bismarck “Through Iron and Blood”. Hakuishia hapo mwaka 1934 Hitler alipeleka vikosi vyake vya kijeshi kwenye mpaka wa kaskazini mwa Ufaransa maeneo ambayo Mkataba wa Versailles uliinyang’anya Ujerumani. Sasa ili kumtuliza Hitler kwa kuogopa vita mataifa ya Ulaya yakiongozwa na Uingereza yalianzisha sera maarufu iliyoitwa "APPEASEMENT POLICY".

Kwamba Hitler na mataifa mengine yaliyo makorofi yapewe tu maeneo watakayovamia ili tu kuzuia vita na kumridhisha Hitler. Hili lilikuwa kosa kwasababu lilimfanya Hitler ajiamini sana kwamba anaweza kufanya chochote kwasababu mataifa mengine yanamuogopa. "Appeasement policy" ilikuwa sera ya hovyo kabisa kwasababu Waingereza na Wafaransa walikuwa radhi kuyagawa mataifa mengine ili mradi tu kujilinda wao na maslahi yao. Mfano mzuri ni katika sehemu ya mkataba huo .

Mwaka 1936 Hitler alivamia maeneo ya RHINE ambayo yaliwekwa yawe huru. Lakini waziri Mkuu wa Uingereza Stanley Baldwin mwaka 1935 akasema Ujerumani apewe tu ili kuzuia vita. Ikumbukwe maeneo ya RHINE ni mpaka wa Kaskazini mashariki wa nchi ya Ufaransa. Hitler alituma vikosi ili kuwapima Wafaransa na akasema ukiona majeshi ya Ufaransa yamejibu mapigo basi rudini. Lakini kwa bahati mbaya ufaransa hakujibu mapigo basi wajeumani wakaka pale na kuzidi kujijenga huku wakijua wanaogopwa.

Mwaka 1936 tena ililipuka vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Hispania na Ufaransa walitaka kwenda kuisaidia serikali ya Hispania lakini waziri mkuu wa Uingereza aliwashawishi sana wasihusike ili kuzuia matatizo na Ujerumani. Mwaka huo huo mataifa yakaitwa Uingereza ili kusaini mkataba ambao utayafanya yasihusike na vita mkataba ulio itwa "NON- INTERVENTION PACT". Mataifa 27 yalisaini huo mkataba yakiwemo yale makubwa ya Ulaya.

Lakini chini kwa chini Hitler na Mussolini walipeleka msaada mkubwa wa kijeshi nchini Hispania ili kuwasaidia waasi wanaopinga serikali. Hivyo serikali ya Hispania ilivyopinduliwa basi Hitler na Mussolini walikubaliana na Serikali ya Jenerali Francis Franco kwamba ikitokea vita na Ufaransa basi waruhusiwe kujenga kambi za kijeshi nchini humo.

Italy ilipeleka silaha nyingi sana huko Hispania. Ndege 130, Mabomu tani 2500, Mizinga 500 ya kuvuta(Canon), Bunduki Mizinga(Mortars) 700, Bunduki 12000, vifaru vidogo 50 na Magari 3800 ya kivita. Ili kuhadaa dunia silaha zote walizipitishia nchini Ureno. Kambi ya Hitler ilizidi kuwa kubwa na kwa Upande wa pili Japan ilivamia Uchina mwaka 1931. Na serikali ya China ilienda kupeleka madai umoja wa mataifa wa wakati huo The LEAGUE OF NATIONS lakini hawakusikilizwa.

Hitler na Mussolini wakawa Marafiki wa watawala wa Japan. Mwaka 1936 Mussolini alivamia Ethiopia na kuitawala kwa muda lakini dunia nzima ikanyamaza huku Mafashisti wakiendelea kujitanua kwa nguvu * Mwaka 1938 Hitler alivamia Czechslovakia akisema anaenda kutuliza ghasia na kulinda haki za binadamu zisivunjwe. Hapa napo Waziri mkuu mpya wa Uingereza Neville Chamberlain alienda hadi Ujerumani kumsikiliza Hitler akisema wamuachie Czechslovakia yote bila ubishi. Hitler baada ya kupewa Czechslovakia........

Itaendelea toleo linalofuata..........

Ndimi: Comred Mbwana Allyamtu.

copy rights reseved
written by Comred Mbwana Allyamtu
•Napatika kwa mawasliano
Comred Mbwana Allyamtu
Kwa Tanzania
+255679555526.
+255765026057.

Kwa Rwanda
+250733153930
+250788214234

Kwa DRC
+243 977 860 824
Email- mbwanaallyamtu990@gmail. Com

...............Vicktoria Venit..........

791a0cf1c8269c7df0f5206e11d20c55.jpg
 
wajeruman ni watata sana had Leo bado ulaya huwa wanawaangalia hao jamaa kwa jicho la kipekee . ila hongera yao still ndiyo superpower had sasa hiv hapo ulaya kiuchumi wapo vizur
 
Hata ugali haupatikani kirahisi hivyo,ila hao jamaa wanagawa ardhi kama pumvi vile yaani bure bure tu Leo hii hata mto tu unaweza ukaanzisha vurugu.
 
Back
Top Bottom