GeoPoll yatoa ripoti inayoonesha usikilizwaji na utazamwaji wa Redio na Tv nchini

brave one

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
4,879
7,382
Kampuni maarufu kwa utafiti wa vyombo vya habari, Geo Poll, imetoa ripoti ya robo ya nne ya mwaka 2016 inayoonesha usikilizwaji na utazamwaji wa redio na TV.

IMG_20170125_135041.JPG


Ikitumia taarifa ambayo huikusanya kila siku, Geo Poll imebaini kwa upande wa redio Clouds FM bado inaendelea kuongoza mbali kwa kusikilizwa sana nchini huku ikiwa na usikilizwaji wa juu zaidi kuanzia saa nane mchana hadi saa kumi jioni.

Nayo Radio Free Africa imekamata nafasi ya pili kwa kusikilizwa zaidi hususan kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 2.

“Kuna ushindani mkali baina ya vituo vya redio wakati wa mchana,” imesema
ripoti hiyo.

IMG_20170125_134822.JPG


Katika vituo 10 vya redio, Clouds FM imeendelea kuchukua sehemu kubwa ya wasikilizaji, ifikayo 23.6% ikifuatiwa TBC Taifa yenye 7.5% na Radio
Free Africa yenye 7.3%.

Kwa upande wa runinga, licha ya Clouds TV kwa ujumla kuwa kituo kinachotazamwa zaidi nchini, saa 2 usiku hadi saa 3 usiku (muda wa taarifa
ya habari) ITV ndiyo inayotazamwa zaidi.

IMG_20170125_134800.JPG


Clouds inachukua 19.6% ya utazamwaji ikifuatiwa na East Africa TV ikiwa na wastani wa 17.2% na kufuatiwa na ITV yenye 17.0%, huku TBC1 ikishika nafasi ya 4 kwa wastani wa 10.8%.

Chanzo: Bongo5
 
Luge anaendelea kuwashikisha adabu japo watu wanampiga sana majungu huu mchezo hauitaji hasira
 
Sio kweli, huu utafiti ni wakinafiki, kukosekana kwa redio iman, kwanza huu utafiti umefanyika kwa nchi nzima ama mkoa 1?.
 
"imetoa ripoti ya robo ya nne ya
mwaka 2016
" watu wanatakiwa kuelewa hapo kwenye red na blue.

Mimi nawapongeza sana E-FM kwani wana frequence moja lakini bado wameshika nafasi ya juu kabisa.
Watu wanatakiwa kujua hii ni report ya robo ya nne ya mwaka 2016 na sio ya mwaka mzima kwa hiyo siyo lazima kituo kizima kiongoze kila mwezi..... lakini ingekuwa ni mwaka mzima ITV inekuwa inaongoza.

Napengine kilicho waongezea credit Clouds ni ile ziara ya Makonda ambayo ilikuwa inatazamwa sana na watu wengi kipindi hicho........
 
Hii tafiti imechukua coverage ipi? nchi nzima? Au Dar pekee?
 
Back
Top Bottom