kaburungu
JF-Expert Member
- Mar 9, 2011
- 3,952
- 7,524
Takribani wiki nne mfululizo eneo la stendi ya mabasi madogo almaarufu vipanya ni chafu na linanuka. Eneo linalotia kichefuchefu zaidi kutokana na hewa iliyochanganyika na uvundo wa taka zilizochanganyikana na maji taka ya mfereji, ni stendi ya vipanya kueleke Usa river. Harufu hiyo ni matokeo ya kufurika kwa mifereji ya majitaka kulikosababishwa na utupaji wa taka katika mitaro hiyo. Je ungozi wa jiji haulioni hili? Naomba kuwasilisha.